Vituko jikoni, Let us share and have fun

Vituko jikoni, Let us share and have fun

kuna siku niliachiwa jiko niandae cha jioni kipindi hicho ndo nimeanza kuaminiwa kidogo kuandaa chakula cha familia si unajua mziwanda tena full kudeka basi nikaamua kupika pilau na mchuzi wa nyama pembeni nikapika pilau safi limechomoka eti nikasahau kuweka chumvi kabisa basi nikaamua kuzidisha chumvi kwenye mchuzi ifidie iliyokosekana kwenye pilau baada ya hapo nikamwita my kaka(tunafatana) nikamwambia akaandae mezani mi nahisi nina homa naenda kulala nae hakujua nn kimetokea akapeleka hotpots mezani mi nikaenda room nikajifunika shuka nasikilizia huko kitakachotokea lol wakajisevia mwanawane baba kupiga vijiko viwili vitatu akaamuru niitwe akapewa jibu nina homa lol wacha wavunjike mbavu wakajua janja yangu
 
Story za kuboroga nnazo telee maana ikiwa mtu kaboronga tunamchekaa siku ya pili anakua na ari mpya lol.....


Cousin yangu last year alipika kachori aliziunga vizuri sana tu sasa wakati wa kuchoma sasa ule uji kafanya mwepesi na mafuta hayajapata moto vizuri akazitia kachori kabla ya hapo nlikua namuambia umekosea hiki nkaambia nifunge bakuli langu, weeee kachori zilitumbuka zote akabaki kukaanga uji wenziwe walimchekajeee na mie mmoja wapo lol

Hahahah... Hio ht mm ilishawahi nikuta mara yangu ya kwanza kupika kachor ramadhan hakuna ilotoka ila now ni mtaalam mzur sana na natumia unga wa dengu badala ngano
 
Na vile viungo vingine ambavyo inabidi uweke kwenye pilau, vingine inabidi utwange. Nikifikiria zoezi lote hili basi hata ile tamaa ya kujaribu inapotea


Sio lazima kutwanga ht vizima unaweka tena inakuwa tamu balaa
 
Yani mpaka nimejua kusonga ugali...nyumbani nishawalisha masotojo ya kila aina....mpaka leo nikitaka kusonga ugali bro wangu ananambia uji ukichemka nimuitee....hawaniamini....!

Ila siri ya ugali mzuri uji uchemkee uive na usiwe mwepesi sanaaa!

Kuna wasukuma niliwasikia wanadai ugali wa kuanzia uji 'unatumbukia', kwa hiyo unawashinda kula. Sikuwalaumu, si unajua ugali wa msukuma?
 
hahhahahh...
mi siku ya.kwanza napika pilau I was 12,nliivisha wali vizuri then nkaeka pilau masala kwa juu nkaongeza na maji ya baridi nkakoroga na kuwasha jiko upya....hhehehe lilitokea bokoboko hataree lenye harufu ya pilau,ilibidi tule hvohvo kesho yake mama ndo akanifundisha kupika pilau

Hahahahahahaha, umenichekesha sana.
 
Niliwahi kupika wali nikajaza sufuria maji ili uchemke na kuiva vyema!!!! Kilichotokea ni matope halafu siku hio nikaachiwa nyumba, kidume nikaamua nijipikie chips nifaidi duh! Hadi leo nimeachana na biashara ya kupika naona sio fani yangu

Umenikumbusha na mi kuna siku nlipika wali ukawa bokoboko hatari.Mama alivofika mezani kufunua hotpot kabla hata hajaeka mdomoni akaniambia, siku nyingine nikipika ivo nieke kwenye thermos kabisa wajue ni uji wanakunywa.Nkikumbuka ayo maneno uwa nacheka.
 
Umenikumbusha na mi kuna siku nlipika wali ukawa bokoboko hatari.Mama alivofika mezani kufunua hotpot kabla hata hajaeka mdomoni akaniambia, siku nyingine nikipika ivo nieke kwenye thermos kabisa wajue ni uji wanakunywa.Nkikumbuka ayo maneno uwa nacheka.

Lol, uji wa mchele sio?
 
Siku nilipojaribu kupika egg chop, duuh sitasahau, si zikaanza kuachia ndani ya mafuta zikawa zinatawanyika tu, yaani nilicheka mpaka basi, sijajaribu tena!
 
kuna sku nilikwenda kumtembelea ma friend when i was in primary, na nilikiwa sijajua kupika ugali vizuri, basi mama wa rafiki yangu akapata emergence akahitajika kuondoka akauliza km ninaweza kupika nikaitikia, basiii tena ndio tukaachiwa jiko, ilipofika kupika ugali process ya maandalizi ya uji ikakamilika ilipofika kupika ugali nikamimina unga kama namwagilia maji kwa mchicha, duuh ugali haukusongeka ukawa unga tupu, basi nikaipua sufuria alafu nikasepa kimyakimya bila kuaga, kilichoendelea nyuma wanajua wenyewe
 
sku nyengine nlieka limau kachumbari ikawa chungu ka mwarobain. afu skuonja, hadi saa ya kula ndo kizaizai kikawa

Ha ha haaaaaaaa, umenikumbusha na mie kuna siku nilipika chukuchuku, bahati mbaya kukawa hakuna kiungo. Kulikua na achari ya ndimu, si nikasema niweke hio. Mchuzi ulikua mchungu haukulika. Lol
 
Siku ya kwanza najaribu kupika chapati, mweeh! ile kitu ilikuwa hailiki kabisa. Nilibugi stepu mbaya maana chapati zilikuwa kama kaukau..Uzuri nilikuwa najifunza na sikuwa na wageni au watu wakisubiria kuzionja, ningeumbuka vibaya mno.
Pilau nayo siku za kwanza nishai tupu..job true true!!
 
Back
Top Bottom