Miss Neddy
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 14,681
- 8,736
kuna siku niliachiwa jiko niandae cha jioni kipindi hicho ndo nimeanza kuaminiwa kidogo kuandaa chakula cha familia si unajua mziwanda tena full kudeka basi nikaamua kupika pilau na mchuzi wa nyama pembeni nikapika pilau safi limechomoka eti nikasahau kuweka chumvi kabisa basi nikaamua kuzidisha chumvi kwenye mchuzi ifidie iliyokosekana kwenye pilau baada ya hapo nikamwita my kaka(tunafatana) nikamwambia akaandae mezani mi nahisi nina homa naenda kulala nae hakujua nn kimetokea akapeleka hotpots mezani mi nikaenda room nikajifunika shuka nasikilizia huko kitakachotokea lol wakajisevia mwanawane baba kupiga vijiko viwili vitatu akaamuru niitwe akapewa jibu nina homa lol wacha wavunjike mbavu wakajua janja yangu