Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Kumbe wanaenda kununua kwa mwamposa mm nikajua labda wananunua msikitini,, sio waislam hao, zuga tu ili wakuvutie kama wewe apo
Hawanunui Msikitini ndio, ila wewe jamaa unaonekana ni mtu uliyeifunga sana akili yako isione, kusikia ama kujifunza tofauti na mazoea yako.
 
Hawanunui Msikitini ndio, ila wewe jamaa unaonekana ni mtu uliyeifunga sana akili yako isione, kusikia ama kujifunza tofauti na mazoea yako.
Point yangu ni kwamba,, uongo wa kitoto msikitini hakuna kama, kuuza vitambaa,mafuta etc. We una uthibitisho gani kama hao wanaonunua maji kwa mwamposa waislam? Usiniambie majina.
 
Loooo shusho nae ana kanisa lake kaanzisha!! Ndio naisikia hapa ila sibishi.
Unamshangaa huyo?kama unamkumbuka Dada Dotinata aliyekua ktk mabendi ya muziki ya dansi maarufu ktk tv enzi zile nae ni mtume ana kanisa lake nasikia itakua pande za ukonga au mbele huko moshi bar
 
Unamshangaa huyo?kama unamkumbuka Dada Dotinata aliyekua ktk mabendi ya muziki ya dansi maarufu ktk tv enzi zile nae ni mtume ana kanisa lake nasikia itakua pande za ukonga au mbele huko moshi bar
Aisee nampata ana weupe flani hvi wa kujikoboa nae ni mtume!!!! Mungu atuhurumie.
 
Siku asimame shekhe msikitini aseme kaoteshwa na mungu kwa hiyo kuna maji ya upako anauza kikombe Jero, huyo shekhe kama akitoka salama humo msikitini sijui,,,, lkn upande huu pili sijui kwanini mnaongopewa kizembe, yani masanja nae mchungaji achilia mbali yule wa kuitwa nabii frola[emoji1]
Yupo Shehe Majini mbona anauza sijui maji ya shajarat, Dini ni uzwazwa
 
Kanisa lingine wana fomu maalumu unajaza kueleza kipato na mali zote ulizo nazo kama ni kuku unao wangapi, kama ni mbuzi na kama ni msharahara unapokea kiasi gani na kama ni biashara ni mtaji wa kiasi gani na inaingiza shilingi ngapi kwa siku....lengo wakuopangie kiasi cha zaka unachopaswa kupeleka kila wiki na Kila mwezi...Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Mungu anawaona
 
: Mwanzo2:2
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

: Mwanzo2:3
Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

: Kutoka20:8
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

M: Kutoka20:9
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;

: Kutoka20:10
lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.

: Kutoka20:11
Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

: Isaya66:22
Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa.

: Isaya66:23
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.

Luka 23:50-56
Luka23:54
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.

Luka23:55
Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa.

Luka23:56
Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.

Waebrania 4:9​

'Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.'

Kama wewe si mtu wa Mungu endelea kudharau sabato
 
Anauzia msikitini hayo maji yake? Au kwenye mkusanyiko wowote unaohusu ibada? Ikiwa hivyo sivyo huyo ni mganga kama waganga wengine na wala haiusiani na kinachojadiliwa hapa
Aache kujiita Shehe na mihadhara Yake ya uponyaji asiwatumie viongozi wa uislam na waislam. Stuka, Dini zote ni miradi ya watu
 
Baba mmoja mkewe alikuwa anasali kanisa moja la kilokole ,ulokole ukamuingia kweli kweli yule mama,jumatatu hadi jumapili yeye ni kanisani akikosa kanisani anaenda nyumbani kwa mchungaji asubuhi anadamka anapika chakula cha kushinda nacho mpaka jioni muda ataokuwa kanisani,baba mwenye nyumba ile tabia ikamchomsha jumapili akaamka akaenda kanisani akawakuta wako kwenye maombi mchungaji yuko mbele,akamchukua mke wake mpaka mbele akawa anawagonganisha vichwa na mchungaji anawaambia eti "oaneni sasa"[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😹😹😹
 
Siku asimame shekhe msikitini aseme kaoteshwa na mungu kwa hiyo kuna maji ya upako anauza kikombe Jero, huyo shekhe kama akitoka salama humo msikitini sijui,,,, lkn upande huu pili sijui kwanini mnaongopewa kizembe, yani masanja nae mchungaji achilia mbali yule wa kuitwa nabii frola😄
Jumapili iliyopita tarehe 27.06.2021 alikuwa Temeke Kata 15, yalitolewa Maji ya Bluu na PILAU DAWA na wikendi hii sijui itakuwa wapi,,,,, na Shekhe yupo salama mpaka leo.....
 
Kanisa lingine wana fomu maalumu unajaza kueleza kipato na mali zote ulizo nazo kama ni kuku unao wangapi, kama ni mbuzi na kama ni msharahara unapokea kiasi gani na kama ni biashara ni mtaji wa kiasi gani na inaingiza shilingi ngapi kwa siku....lengo wakuopangie kiasi cha zaka unachopaswa kupeleka kila wiki na Kila mwezi...Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Mungu anawaona
Inakuaje watu wanatoa maelezo yote hayo?
 
Back
Top Bottom