In short ukiwa kama ni Mkristo, unapaswa utambue hakuna kanisa ambalo halina mwanzilishi (mwanadamu mmoja au kikundi cha wanadamu) na hiyo ipo hivyo kwa kanisa kongwe au la sasa...
Hivyo kama kuna udhaifu wowote, hayo ni matokeo ya uwepo wa wanadamu kama viongozi au waumini...
Sisi wanadamu tumekuwa wepesi sana wa kuona watu wengine wasio na msimamo sawa na sisi kama wanakosea, aliye mlokole ataona asiye mlokole kapotea na kinyume chake pia...
Kama kuna mwanadamu wa imani yoyote aliye kamili kwa kila idara, basi na anyooshe kidole...
Na kama wewe ni Mkristo kweli (kwa kufuata maandiko), inasemwa huko kwamba mwenzako akipotoka wewe muombee arejee kwenye mstari na sio kuanza kumsimanga (usihangaike kutoa kibanzi kwa mwingine, ingali una boriti)
Lk 6:41-45 SUV
Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako. Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Sent using
Jamii Forums mobile app