Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

In short ukiwa kama ni Mkristo, unapaswa utambue hakuna kanisa ambalo halina mwanzilishi (mwanadamu mmoja au kikundi cha wanadamu) na hiyo ipo hivyo kwa kanisa kongwe au la sasa...

Hivyo kama kuna udhaifu wowote, hayo ni matokeo ya uwepo wa wanadamu kama viongozi au waumini...

Sisi wanadamu tumekuwa wepesi sana wa kuona watu wengine wasio na msimamo sawa na sisi kama wanakosea, aliye mlokole ataona asiye mlokole kapotea na kinyume chake pia...

Kama kuna mwanadamu wa imani yoyote aliye kamili kwa kila idara, basi na anyooshe kidole...

Na kama wewe ni Mkristo kweli (kwa kufuata maandiko), inasemwa huko kwamba mwenzako akipotoka wewe muombee arejee kwenye mstari na sio kuanza kumsimanga (usihangaike kutoa kibanzi kwa mwingine, ingali una boriti)


Lk 6:41-45 SUV
Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako. Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unaweza kuniambia kwa ushahidi mwanzilishi wa Kanisa Katoliki nje ya Yesu mwenyewe? Just a direct answer kama tunavyoweza kusema makanisa mengine yote!

Mtu mwingine yeyote anaweza kusaidia lakini isiwe hadithi tulizozoea iwe na utafiti binafsi ili tukiuliza maswali yajibiwe!

Pia naomba nitajiwe jina la Kanisa ambalo lilikuwepo kabla ya mwaka 1000 nje ya Kanisa Katoliki! Nitafurahi pia kujua kiongozi yeyote aliyekuwepo wakati huo.
 
Siwezi kanyaga kwenye hayo makanisa saizi imekuwa stile ya watu kujiajiri, kuna mchungaji mmoja alimchukua binti kanisani mbele ya waumini kutokana na binti huyo kuishi katika mazingira duni na alikuwa kafauru kwenda form one na hivyo alienda nae mjini akakaa nae wikend yote akamla na hata hizo uniforms hakununua taarifa baada ya kufika kanisani waumini wanasema kuna watu wana nia mbaya wanamchafua mchungaji, wakati hapo wanapoishi kinapatikana kila kitu kuna haja gani kumpandisha basi kwenye umbali mrefu eti kununua uniform wakati wanapoishi kuna kila kitu na kwanini hakuchaguliwa mwanamke mwenzie amsindikize.
Yaani makanisa haya ni utoporo mtupu!! Mchungaji anaaminiwa kuliko kuliko hata Bible...huyo binti atakuwa alibakwa masikini mweeh!!
 
IMG-20210604-WA0124.jpg
 
Nina mjomba mmoja alitia mimba mwanafunzi. Daaa!! Sasa Ile heshima ya sutisuti na majoho marefu marefu wakamtetea sana. Baba mtu hakukubali, akaamua kugharamia DNA, laaa!! siku mbili tati tunasikia yuko Congo anatoa mapepo kule.
 
kUna watu wametekwa akili na hao manabii/makasisi wasio hata na elimu juu ya thiolojia 🤣 🤣
Kuna mahali walileta mkutano wao mkoa flani na sehemu hiyo ni kiwanja cha mpira tunapiga tizi pale kila siku baada ya kazi
Katika kuzushiana nao kwamba wahame basi DC/Mkurugenzi wakaingilia kati tukaachana nao
Mombi ya kelele yalipigwa kwa week moja na rumba kali sana hasa masaa ya jioni. Baada ya week sasa kasisi anamaliza mktano wa mwisho waumini wakaambiwa wamtolee mungu chochote kama zawadi kwakweli fwedha alipata pale
Watu walileta vitu mbali mbali pale ila hii sijaisahau . Yupo mama mmoja addicted kichizi na hii michongo ya mikutano na bwanake ni mpasua mbao
Yule mama alichukua mbuzi wanne nyumbani kwake akapeleka kwenye mkutano. Baadae kidogo mme wake kapigiwa simu kwamba mbuzi wanapelekwa maombi nae fasta akaunga pale pale ikawa noma kweli kweli akidai mbuzi wake 🤣🤣🤣
Basi akarudishiwa na laana kibao wakimpiga. Yule mama hakuwahi rudi kwa bwanake mpaka wa leo
 
Mkuu unaweza kuniambia kwa ushahidi mwanzilishi wa Kanisa Katoliki nje ya Yesu mwenyewe? Just a direct answer kama tunavyoweza kusema makanisa mengine yote!

Mtu mwingine yeyote anaweza kusaidia lakini isiwe hadithi tulizozoea iwe na utafiti binafsi ili tukiuliza maswali yajibiwe!

Pia naomba nitajiwe jina la Kanisa ambalo lilikuwepo kabla ya mwaka 1000 nje ya Kanisa Katoliki! Nitafurahi pia kujua kiongozi yeyote aliyekuwepo wakati huo.
Yesu alianzisha kanisa katoliki?Proof?
 
Nlikua naenda kuombewa sasa shida mguu.naenda kwa bodaboda.siku hiyo bahati mbaya nkajigonga kwenye mfupa was mguu na China Fulani nipo pale unapoegesha mguu kwenye pikipiki.
Basi lufika Mda wa maombi mchungaji akawa ananipiga Kofi la nguvu kwenye miguu huku anakemea..nlikua napata maumivu makali.
Baadae naulizwa unajiskiaje..nkawaleza hamna kitu.nlikua naumia tu sehemu wanayonipiga kofi sana kuna jeraha.wakaanza kudakia ooh ni upako huo..NI upako.
Me be like what?nivimbe mbali halafu upapige ngumi maumivu we unasema upako.
 
Nilipewaga mualiko na mpangaji mwenzangu(mdada mlokole) kanisa I kwao(makongo ukipita ardhi)kuna seminar ya wanaume wote Tanzania!!!!

Nikamuuliza tutaenea wanaume wote?siku ilipowadia (jumamosi) nikajongea mpaka kanisani,nilipoingia ndani nikakuta nabii bado hajaingia kuanzia seminar.

Tukawa tunatangaziwa kuwa nabii haiwezi ingia mpaka wanaume wote muse mmevaa kofia(kapelo nyeupe ina picha ya njiwa) issue ikaja kwenye Bei!!!!

30,000/!!!!mfukoni nina 5000 ya sadaka nilinyanyuka nikatoka nikazuiwa kuwa seminar itaanza!nikajibu kuna wenzangu wamepitiliza makongo unaenda wafuata.....sikurudi Tena.

Kesho yake dada mpangaji ananiuliza kama nilienda nikajibu ndio.akasema muongo kaka nikamwambia kofia 30,000akaaema eeeh kweli ulienda,umenunua?

Nikajibu siwezi ninja kofia 30,000mwanangu lake njaa wadada wote uami waliangua kicheko.
 
Acha kujisahaulisha...
Mbona mnauza miti shamba huko misikitini?
Msikiti gani unauzwa mitishamba? Na shehe yupi anaesimama ndani ya msikiti kuwaambia waumini kaota kwa hiyo wanunue hiyo mitishashamba. Lkn tambua ya kwamba hata hiyo mitishamba ukikuta wanauza lkn si kwa kisingizio cha upako na wala si ndani ya msikiti, na kama ulivyosema mitishamba ni dawa iyo mbona inafahimika mfano muarobani,muarovera etc.
 
Mbona shehe yahaya majini anauza vichupa vya maji ya baraka kutoka uarabuni.

Siku hiyo ndio niligundua kuna mashehe hama mitume na manabii. Vimaji vinanguvu maana alipofungua kamoja tu uwanja mzima wanawake wakalipuka mapepo.
Acha uongo,,, aliyekuwa anatangaza hayo maji ni aliyekuwa mchungaji anaitwa kessy,, alikuwa akiwaonyesha watu jinsi gani mnavyopigwa. Huyo shekhe yahya tangu lini umesikia anauza maji acha fiksi bana, kwanza waislam hawadanganyiki kizembe na hilo unalitambua usijitoe ufaham, yani uote afu uwatangazie watu ww mtume 😄
 
Back
Top Bottom