Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Siwezi kanyaga kwenye hayo makanisa saizi imekuwa stile ya watu kujiajiri, kuna mchungaji mmoja alimchukua binti kanisani mbele ya waumini kutokana na binti huyo kuishi katika mazingira duni na alikuwa kafauru kwenda form one na hivyo alienda nae mjini akakaa nae wikend yote akamla na hata hizo uniforms hakununua taarifa baada ya kufika kanisani waumini wanasema kuna watu wana nia mbaya wanamchafua mchungaji, wakati hapo wanapoishi kinapatikana kila kitu kuna haja gani kumpandisha basi kwenye umbali mrefu eti kununua uniform wakati wanapoishi kuna kila kitu na kwanini hakuchaguliwa mwanamke mwenzie amsindikize.
Wana macho lkn hawaoni a.k.a wamepigwa upofu na ndumba za machungaji
 
Huwa siamini ujinga. Ila nilishsngaa na waislam nao wameanza usanii
[emoji2][emoji1][emoji2][emoji2][emoji23][emoji23]ndio maana Mimi niponipo tu siendi church Wala masjid Mungu wangu namuomba chumbani kwangu tu
Yatosha
 
Mchungaji alipokua akiomba nilishuhudia muumini mmoja ninaemjua akiongea kiingereza fasaha wakati namjua kabisa hajuagi kiingereza.
Maana yake pepo la kizungu lilipanda.hii sio chai Ni kweli kabisa.

We ndo uliekuwa ukimlipia ada mpaka useme alikuwa hajui Kiingilishi
 
Dini ya kikristo imeyeyuka sana na imeshuka thamani michango mingi.

Saivi hakuna uhuru ukisali agrican wewe mroma unapigwa madongo, ukiwa mlokole ukihama kanisa unapigwa madongo, ukisali roma wewe ni kkt utapigwa madongo saa zingine unaonekana ni kondoo uliepotea hakika kwa sasa ubinafsi mkubwa wa kuona kila mmoja ana thamani tumekua wakujipenda wakati sisi wote kilio chetu ni kupitia mwana wa adam aliekufa msalabani,sisi ni watoto wa abraham, isaka na yakobo ila ukisema umeungana nao wanakupokea na kusema karibu ila ukiwa umeenda kujisalia vijembe vingi kuliko neno lenyewe.

Ubaguzi kama huna jumuiya kanisani utaisoma namba utasemwa sana, kuna watu tunataka kusali na kuondoka ila mwishoni makanisa mengine mnapigwa madongo jamani kwa biblia inalazmsha hayo kuna maeneo huwezi kuta kanisa lako.

Michango imekua mingi wakati hali hairuhusu kila kukicha ni kujenga makanisa likikamilika ujenzi mwingine sijui unatokea wapi Hakuna Amani Ya Kusali tena.

Kwa kweli hizi zama ni za mwisho tunasali kufuata ratiba lakini tumekosa uhusiano na Mungu kupitia kristo tunasali kutimiza wajibu ila ndani hakuna kitu kabisa.


All in all makanisa ya kilokole madhabahu zao wanaweka mazindiko mazito sana haiwezekani tulazimshwe kuzizunguka na kuomba wakati unaweza omba ukiwa hata umekaa kwenye siti yako.

Kuna kanisa moja hapa kati kati ya tz dodoma watu walipangwa kufanya ibada asubuhi kumbe kuna ng,ombe kachinjwa toka saa kumi usiku kufika saa kumi na mbili kisha iva wakaambiwa kuleni lakini mifupa kusanyeni sehemu moja, ilivyofika saa kumi na mbili wakiwa wamemaliza kula walianza ibada alitua tai mkubwa mida ya saa kumi na mbili na madakika wakaambiwa wamzunguke waombe wakiwa wamefumba macho.

Walivyomaliza watu walibaki mdomo wazi wakuhama walihama wakuendelea waliendelea.


Nimepita makanisa Mengi kwa sababu sio kila eneo utakuata kani lako mfano KKKT, AGRICAN na T.A.G lakini ROMAN CATHOlIC wamejipanga mpka vijiji ambavyo huwezi tegemea lakini wapo.
Dah kaka umeandika kwa uchungu sana asee
 
Na Kuna mijanamke mingine inapendwa kweli na waume zao lkn Ni mibishi balaa mpka inaboa yaani
Tena umkute mwanamke anasali makanisa ya kilokole yanayochipuka kila siku,wabishi kweli sijui wanalishwaga sumu gani huko kanisani?halafu kila kitu kwao ni shetani, mfano huyo mama alikuwa anaambiwa na mume wake aende kanisani siku tatu katika wiki siku nne afanye mambo mengine yeye ndo kwanza anafunga na kusali anaona mumewe kaingiliwa na shetani !!!
 
Hii michango lukuki Roman Catholic imenifanya mpagani na sijutii wacha nikaonane na Mungu tu.
Kuna KKKT, hii imekuwa kama vikoba...thamani yako inategemea na fungu unalotoa, haswa kwenye ujenzi ambao wanajali sana mahekalu ya kifahari kuliko usafi wa mioyo ya waumini.

Unaweza kuwa mzinzi,mlevi,mwizi na uchafu mwingine wowote ulio kinyume na imani, lakini kama unatoa mzigo wa maana basi wewe ni mtakatifu machoni mwa hawa viongozi.
 
Wakuu, ni dhahiri kuwa kuna makanisa yanaibuka sasa kama uyoga. Sioni shida kuibuka kwa makanisa kila kukicha, kwasababu hata baa mpya zinaibuka kila siku.

Pamoja na yote, haya makanisa kuna baadhi yana vituko sana, yaani Mtumishi anaweza kuwa Mtume, Nabii au Mchungaji lakini mambo wanayofanya ni vituko na ajabu! Cha kushangaza bado waumini wapo.

Nianze mimi.
1. Hichi kituko kinaendelea kutokea kanisa moja Arusha, mtumishi kaacha familia Dar, kaenda kutumika Arusha kapachika muumini mimba, mke Kaenda Arusha, kulalamikia kanisa kuwa amefunga ndoa na huyo mtumishi, kituko Kanisa linamtetea Mtumishi kuwa wao hawakujua kama ameoa. Hivyo ataendelea kutoa huduma kanisani, can you imagine!!

2. Jamaa yangu huyu kaanzisha kanisa lake, kapata waumini wakutosha! Kaoa mke November, February mwaka unaofuata mke anaondoka na kila kitu, kwa madai mume wake ni mzinzi, shutuma zinafika kanisani, waumini wanaungana na mchungaji wao kukemea 😂😂😂. hii ni Kilimanjaro.

3. Christina Shusho anaanzisha kanisa baada ya kutalakiana na Mume wake na ana waumini wakutosha. Ya kujifunza ni mengi hapa.

Tuendeleze vituko vingine....
Watu wanacheza na imani za watu.
 
Kuna KKKT, hii imekuwa kama vikoba...thamani yako inategemea na fungu unalotoa, haswa kwenye ujenzi ambao wanajali sana mahekalu ya kifahari kuliko usafi wa mioyo ya waumini.

Unaweza kuwa mzinzi,mlevi,mwizi na uchafu mwingine wowote ulio kinyume na imani, lakini kama unatoa mzigo wa maana basi wewe ni mtakatifu machoni mwa hawa viongozi.
😀 😀 Tena na uzee wa kanisa wanakupa.
 
Tena umkute mwanamke anasali makanisa ya kilokole yanayochipuka kila siku,wabishi kweli sijui wanalishwaga sumu gani huko kanisani?halafu kila kitu kwao ni shetani, mfano huyo mama alikuwa anaambiwa na mume wake aende kanisani siku tatu katika wiki siku nne afanye mambo mengine yeye ndo kwanza anafunga na kusali anaona mumewe kaingiliwa na shetani !!!
Walimalizanaje hao Mme na mke au waliachana?
 
Acha chuki binafsi dogo, mbona wanaogombania sadaka na kuongoza misikiti huwasemi wale wavaa vipedo
 
Back
Top Bottom