Vituko kutoka kwenye Makanisa ya Kilokole -Tupia chako

Wana macho lkn hawaoni a.k.a wamepigwa upofu na ndumba za machungaji
 
Huwa siamini ujinga. Ila nilishsngaa na waislam nao wameanza usanii
[emoji2][emoji1][emoji2][emoji2][emoji23][emoji23]ndio maana Mimi niponipo tu siendi church Wala masjid Mungu wangu namuomba chumbani kwangu tu
Yatosha
 
Mchungaji alipokua akiomba nilishuhudia muumini mmoja ninaemjua akiongea kiingereza fasaha wakati namjua kabisa hajuagi kiingereza.
Maana yake pepo la kizungu lilipanda.hii sio chai Ni kweli kabisa.

We ndo uliekuwa ukimlipia ada mpaka useme alikuwa hajui Kiingilishi
 
Dah kaka umeandika kwa uchungu sana asee
 
Na Kuna mijanamke mingine inapendwa kweli na waume zao lkn Ni mibishi balaa mpka inaboa yaani
Tena umkute mwanamke anasali makanisa ya kilokole yanayochipuka kila siku,wabishi kweli sijui wanalishwaga sumu gani huko kanisani?halafu kila kitu kwao ni shetani, mfano huyo mama alikuwa anaambiwa na mume wake aende kanisani siku tatu katika wiki siku nne afanye mambo mengine yeye ndo kwanza anafunga na kusali anaona mumewe kaingiliwa na shetani !!!
 
Hii michango lukuki Roman Catholic imenifanya mpagani na sijutii wacha nikaonane na Mungu tu.
Kuna KKKT, hii imekuwa kama vikoba...thamani yako inategemea na fungu unalotoa, haswa kwenye ujenzi ambao wanajali sana mahekalu ya kifahari kuliko usafi wa mioyo ya waumini.

Unaweza kuwa mzinzi,mlevi,mwizi na uchafu mwingine wowote ulio kinyume na imani, lakini kama unatoa mzigo wa maana basi wewe ni mtakatifu machoni mwa hawa viongozi.
 
Watu wanacheza na imani za watu.
 
πŸ˜€ πŸ˜€ Tena na uzee wa kanisa wanakupa.
 
Walimalizanaje hao Mme na mke au waliachana?
 
Acha chuki binafsi dogo, mbona wanaogombania sadaka na kuongoza misikiti huwasemi wale wavaa vipedo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…