Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Mwananyamala ni moja kati ya maeneo ya Dar ambayo ukiishi kwenye nyumba ya kupanga utalazimika kodi kuigawanya hata mara 4 ili uwape watu tofautitofauti. Nyumba nyng ni za urithi, watoto ni mateja na akipokea kodi yote mtu mmoja tu bas wengine wote inakula kwao na watakuja kukutolea vyombo nje ww mpangaji [emoji23]
 
Hivi unakumbuka kulikua kuna mwalimu wa kike mwalimu mshana ana undugu nae ninii hassan alikua anakaa manjunju au Hassan yupiii halaf nae si alifariki
 
Ninachokumbuka ni kwamba walihamisha mwili baada ya wahuni kuvamia kaburi na kufukua
 
Kuna mzee mmoja alikuwa anaitwa mzee madai yupo hapa km unakwenda kwa kina sisiter P kuna eneo linaitwa torabora( panavutwa bangi 24hours ukiona mtu ameva begi mgongoni sio denti wa tution ila ni pusha) mzee madai alikuwa mganga wa kitapeli kipindi icho simu za kufunua zimeingia simu yake ikiita ring tone ni "mzee madai mzee madai" mtoto wake mmoja alikuwa anajita mbongo halisi (bongo fleva)
 
He he umenikumbusha sister p alivyokua mchafu chafu shule hapendi siku ya siku namuona kwa TV kheee huyu si happy tadei huyu
 
[emoji23] [emoji23] [emoji119] [emoji119]

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Ninachokumbuka ni kwamba walihamisha mwili baada ya wahuni kuvamia kaburi na kufukua
Kumbe walifanya yao wahuni? Ila siku kaburi linafukuliwa nilikuwepo maana eneo lote mwanyamala na viunga vyake walipata taarifa mpaka kinondoni studio watu walikuwa ni wengi sana na siku ile ndio james ngomero alipopata KIKI maana kaburi lilikuwa na zege juu mwanaume alipiga kazi balaa
 
Mbongo halisi yupo hadi leo. Profile yake fb anajitambulisha kama 'She' Tolabola uvutaji nangi umepungua nahisi ubrazamen unachangia.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Those beautiful moments are gone forever

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…