Nimesoma almost kila comments nimecheka sana na nimekumbuka mengi,nimeishi Mnyamala long ago, darasa la kwanza nimeanza Mnyamala B primary ila memory haipo kwa sana what only nakumbuka tulivyokuwa tunachanja mitaa matumbo wazi tukienda Dampo Tabata au Mikocheni beach kwa miguu kutokea mitaa ya Mama Zakaria!nakumbuka ngoma za madogori na process za kuwatoa watu uchawi pia mdundiko kila siku Nakumbuka nyumba tuliyoishi 80s nakumbuka hotel moja maarufu ilikuwa yaitwa Motel Villa kipindi hicho weekend ilikuwa ni disco hakuna siku disco lilipita bila ugomvi, nakumbuka ilitubidi tuhame baada ya wazazi wangu kugungua tulikuwa tunarogwa /tunawangiwa tukqhamia Sinza,wazazi wangu wana miliki nyumba mitaa ya bondeni nyuma kwa mama Zakaria,uwa nikipataga nafasi naenda mara moja moja kuangalia panaendeleaje ingawa ni almost gofu na hakuna mtu kati yetu mwenye interest napo kwa ajili ya vituko vya maeneo hayo including uchawi.
Huwa najaribu kui locate baa moja ilikuwa yaitwa Matimila nafikiri Remy alikuwa anafanyia mazoezi sipapati napenda nipafahamu nakumbuka nilikuwa natoroka shule naenda kuchungulia hayo mazoezi Mshana utanisaidia maana wewe ni mwenyeji kiasi.