Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Buguruni nako palikuwa kiboko kwa uporaji labda kama kumebadilika siku hizi. Hasa maeneo ya Ghana na Malapa
 
Hawa wadudu bado wapo. Kwasasa bao ni bei gani ?
 
Mwananyamala hasa Mwananyamala kisiwani..! Kuna watu wanafuga mpaka swala sasa jiulize kuna mbuga...wanga kinoma...hasa maeneo ya uwanja wa Alaska ...marehemu MZEE makuka....sikinde...na zoni aisee ...sijasahau maduka matatu...kwanza kuna watu wanauza komoni noma.....mwananyamala paka wanalia kama watoto ....

Harafu huko miaka ya 93-94 ndiyo kuliongoza kuwa na makomando yosi(wahuni enzi hizo) staki hata kupasikia hukooo....
 
Ukiwa na mke au watoto. Sehemu hizi sio nzuri kuishi nayo:-
Mwananyamala
Magomeni
Keko
Buguruni
Ilala
Vingunguti
Bonde la msimbazi
Msasani bonde la mpunga
Iyo mieneo mtoto kudata ni kitu cha Kawaida sana

Mkuu vipi hizi

1: Yombo Dovya
2: Yombo Vituka
3: Kigogo
4: Mburahati
5: Tandale​
 


Mkuu,

Hii topic nimeikubali sana. Watu wa Mwananyamala wametupa fundisho. Niko page ya 59 ya thread hii na nitahakikisha nafika hadi mwisho.

Kama Mwananyamala iko sawa na KIGOGO, TANDALE, KEKO, MBURAHATI basi watu tuliokulia mitaa mingine hapa nchini tunatakiwa pia kuanzisha thread zetu ili tujue phsychology yetuimeundwaje.

Mimi nimekulia mitaa mnayoita uzunguni. Wajomba zangu mmoja amekaa MWANANYAMALA KISIWANI kuanzia 1976 hadi 1994. Mwingine kakaa MAGOMENI karibu na DDC MAGOMENI pale shuleni kuanzia mwaka 1975 hadi 1988.

Nimetoka Chuo Kikuu wameshahama na wana familia zao, wameshahamiz Sinza, tena yule wa MWANANYAMALA ana mabinti watupu. Nimeanza maisha kwa mwaka mzima nikaishi kwa mmoja wa hao wajomba na hivi wako karibu kama mita 50 hivi nikawa yaani naishi nao wote.

Amini usiamini, haikupita hata miezi sita tayari nikawa nimeingia mgogoro ambao umedumu hadi leo, na hii ni kutokana na tabia za mabinti za mjomba yule wa MWANANYAMALA. Baadaye haikupita miaka miezi 15 nikaingia mgogoro na yule mjomba aliyehama MAGOMENI.

Ilibidi nihame mapema kuanza maisha yangu maana sikuwez kabisa tabia zao. Kwanza ni watu ambao wanaona ugomvi ni kitu cha kawaida, wakati maeneo niliyokulia kugombana ilikuwa ni kituko.

Kutukana matusi ya nguoni hawaoni shida, wakati nilipokulia ukitukana mtaa mzima unakujia juu.

Sasa tuna miaka 18 tangu tumetengana na wale wajomba kwa ugomvi ule maana. Inavyoelekea hadi vofo vyetu hatutakuja kurudiana, ugomvi ulikuwa mkubwa.

Jambo ambalo sikulitafakari wakati ule ndilo ninaloliona humu kwenye uzi huu. Kumbe pamoja na kwamba walikuwa ni wajomba zangu ukweli ni kwamba mimi na wao tulikuwa ni watu wawili tofauti tusiofanana.

Kwamba kama umekulia MIKOCHENI halafu mtu amekulia MWANANYAMALA basi hawa ni watu wasiofanana.

Tabia mnazosema humu ndizo typical za wale watoto wa wajomba wale.

Hivyo, kila ninapopata muda kutafakari historia yangu na ugomvi ule ninaona kwamba haikuwa busara kuanza maisha na wale wajomba ilhali mimi na wao tumekulia maeneo tofauti.

Hii nimekuja kuona mnapoyajadili haya.

Cc:
mshana jr
 
Hahaaa...pole. Unanikumbusha kisa kimoja tungali tunaingia ujanani. Mshkaji wetu mmoja ilibidi atoke Mburahati aende akaishi masaki kwa ndugu zake kwa muda. Sasa inshu ilikuwa ktk msosi yaani walishazoea kuwa chakula lazima kibaki cha na mara nyingi akina dada ndo huwa wanajua kuwa kuna msosi wananywea chai. Sasa baada ya kuingia kamanda hali ikabadilika. Kwanza msela baada ya kuona aibu kujisevia msosi mwingi mbele ya watu mezani akawa anakuwa was mwisho kula. Baada ya utafiti wa muda mfupi tuu msela akajulikana ikabidi wshauriane kuongeza kipimo wapate kiporo cha chai maana jamaa alikuwa anawapeleka dry
 

Mkuu,

Hii post yako ina akili sana na utaielewa mtu ukiisoma hadi mwisho.
 
Hivi si ndiyo huko kuna mkandarasi mmoja alijifungia chooni na mfanyakazi wa ujenzi wa barabara, alipobainika na kuulizwa kwanini alijifungia chooni, akasema alimwomba akamfanyie shaving!!!
 

Ha ha ha ha noma sana
 
Hivi si ndiyo huko kuna mkandarasi mmoja alijifungia chooni na mfanyakazi wa ujenzi wa barabara, alipobainika na kuulizwa kwanini alijifungia chooni, akasema alimwomba akamfanyie shaving!!!
[emoji15] [emoji15] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…