Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

Mkuu sio maiti zile,wala sio viungo halisi vya binadam.Ni teaching aids zinaitwa cadaver!.Yaan unatengenezwa mwil wa mtu kwa plastic ili kufundishia masomo ya udaktar katika vyuo.Hakukuwa na kiungo halis.

kweli wewe hamnazo
 
Mkuu hivi unaelewa unachokiandika?

Nakubaliana na wewe unaposema unatengenezwa mwili kwa plastic.

Natofautiana na wewe kwa scenario hii ya bunju unapong'ang'ania kuwa hakukuwa na kiungo halisi.

Ina maana hata hizo picha tunazoonyeshwa ni viungo vya plastic? Kuna mdau amesema kaona viungo vingine vinatoa damu, je plastic inatoa damu?

Nimesoma bandiko lako kule juu, umetoa ufafanuzi huu huu kwamba ile sio miili halisi, kitu ambacho si kweli kwa scenario hii ya bunju. Sasa kama ni plastic kwa nn watu wapanic na ma_toy?

Karibu.
 
kweli wewe hamnazo

Mkuu nimemuuliza maswali, binafsi nimetofautiana nae kabisa, amekomaa kwamba hakuna mwili pale zile ni plastic!!

Aiseeee!

Mkuu Eiyer em njoo huku usome maandishi ya kijana wako FREEideas!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sio maiti zile,wala sio viungo halisi vya binadam.Ni teaching aids zinaitwa cadaver!.Yaan unatengenezwa mwil wa mtu kwa plastic ili kufundishia masomo ya udaktar katika vyuo.Hakukuwa na kiungo halis.

ooooh! Sasa nimeelewa, nashukuru mkuu kwa kuniweka sawa, ila na baadhi ya vyombo vya habari vimeiwasilisha hii habari vibaya. Nilikuwa na hofu. Sasa hawa baadhi ya wanajamvii wenzangu wanaongea mambo ya "damu" na kidogo ilinichanganya. ASANTE kwa kunijuza.
 
kauli bado iko palepale pale the clear information nilizonazo ni viungo vya binadamu na wala sio maiti zaidi ya 100.

tuelewane kwanza, wapo wagonjwa wakisukari wanakatwa miguu hata mikono na bodaboda wengi pia hukatwa miguu.

hapa tunasubili sasa clear statement ya polisi na wizara ya afya why this? na ni nani anawajika au kuwajibishwa.

Clear statement kutoka polisi wa nchi gani?
 
ooooh! Sasa nimeelewa, nashukuru mkuu kwa kuniweka sawa, ila na baadhi ya vyombo vya habari vimeiwasilisha hii habari vibaya. Nilikuwa na hofu. Sasa hawa baadhi ya wanajamvii wenzangu wanaongea mambo ya "damu" na kidogo ilinichanganya. ASANTE kwa kunijuza.

Mkuu kwa hiyo na wewe umeelewa vile ni viungo vya plastic?
 
Hahahah,mkuu kila kitu kina wakati wake wa kutumika na hata ku-expire.Kuna haja gani ya kutumia Teaching-Aids mfululizo miaka 5/7,wakati zipo zingine?.Muda wake uliisha na zilitakiwa kubadilishwa ziletwe nyingine ama zitupwe kwenye tanuru kama ilivo kawaida.

Kwan mkuu hujasoma hata sayansi form2 ?.Zile chemicals zikikaa sana kuna wakati hata uchanganye vipi hafanyi reaction yoyote maana zimepitwa muda na zinahitaji kubadilishwa.Hiyo ni kawaida na sio mara ya kwanza kutokea sema mara zote huwa wanachoma katika tanuru sio kutupa hadharan kama hivi.

Mkuu naelewa yote hayo na elimu niliyonayo ni zaidi ya Sayansi ya form two; na hata sasa niko nje ya Tz nikipata elimu zaidi. Ni kweli chemicals zinabadilishwa kwa sababu ya expiry period. Sasa vipi kuhusu miili ya binadamu mabaki/residual aka cadaver za binadamu kama teaching aids, zinapotupwa ina maana miundo/mifumo (anatomy) ya binadamu imebadilika na sasa madaktari wanatakiwa kusomo mifumo mingine. Just kidding lakini, nataka utumie nafasi hii kutoa elimu kwa Umma kuhusu tiba ya binadamu, ingekuwa kule SUA jamii ingeona cadaver za wanyama ama sivyo ????

Anyway, najua maiti zinatumika na hata kuazimwa kutoka mabara mengine, lakini ni siri ila kwa sababu ya uzembe na kutowajibika uliopo nchni mwetu siku hizi ndio maana haya yamegundulika na jamii za kawaida na kuanza kushangaa. Lakini vle vile afadhali limetokea na kutmika kama sehemu ya elimu kwa umma kuhusu taaluma ya matibabu. Mtu anapoenda hospitali, Daktari akafanyia operation na kushona au anaposafishwa kidonda ina maana Daktari au Muuguzi alishazoezwa kuona vitu kama hivyo, mtu wa kawaida kuona maiti tu ndani ya mortuary ni kazi,
 
Hili suala si dogo. Linahusu ubinaadamu wetu. Ile ni miili ya ndugu,jamaa na marafiki zetu.Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,bado haikupoteza thamani yake kama ni miili ya binaadamu na hivyo heshima,staha na taratibu zilipaswa kufuatwa. Majibu kuhusu wapi imetoka miili ile ya Bunju hapa hayatakuwa na uzito bila ya kwanza kukubali kuwa kulikuwa na makosa juu ya kushughulika na miili ile.

Kwa majibu yoyote, hali ile haivumiliki. Iwe imetokea IMTU au kwingineko, yupo mtu au wapo watu wa kuwajibika. Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,zipo taratibu za kushughulikia miili ile ikiwa ni pamoja na namna ya kuiteketeza.Mifuko ya rambo si namna ya kuiteketeza hata kama mimi si mwanasayansi. Kuitupa si jambo linalokubalika. Kwanza,kuitupa kiholela vile,kulihatarisha amani.Yangekosa mabomu ya Polisi,muda huu yangezungumzwa mengine.

Nitoe rai kwa wahusika wote wa sakata la jana la miili ya Bunju kujipima na kuwajibika. Tasnia yoyote ina miiko yake. Ya sayansi jana ilikiukwa. Yupo wa kuwajibika. Atambuliwe au ajitambue na kuwajibika haraka iwezekanavyo.
 
Kweli yupo wa kuwajibika ila hakuna atakaye wajibika!
Huu ni upepo tuu!
 
mbona tutasikia mengi mara cadaver cadaver cadaver ..................

huu sio umakini unfikiri mtu wa kawaida ataelewa hapa?
 
hapo juu kuna mdau anapotosha kuwa watu wanafanya anatomy kwa kutumia viungo vya plastiki SIO KWELI

Huwa wanajifunzia miili ya binadamu ya kweli

mie sipo eneo la tukio lakin katika hali ya kawaida maiti ya binadam ina harufu mbaya sana...hiyo imewekewa dawa ya kuhifadhia (formalin) au nyingine inayofanana na hiyo so haiharibiki wala kutoa harufu kali.

Kuwa uwezekano kweli hiyo miili ilikuwa ikitumiwa kama darasa kwa madaktari wetu wa hapo baadae.

kosa ni poor management ya waste...wameenda kuitupa kusikostaili...na inawezekana kama alivyosema mdau mmoja hapo juu kuwa kulikuwa na ukaguz wa kushtukiza eneo husika.

Tusipende tuonekane tupo perfect kwa kuficha uozo....bora wangeziacha hukohuko zilipokuwa ili wakikaguliwa watoe kero yao huenda wangepewa msaada......AU WALIOGOPA KUFUNGIWA KAMA ILE HOSP YA KARIAKOO?
 
Ndani ya CCM kuna mtu yeyote mwenye ujanja wa KUWAWAJIBISHA Wahindi?
Ile miili imetupwa na uongozi wa Chuo cha matibabu kinachomilikiwa na Wahindi IMTU
 
Hili suala si dogo. Linahusu ubinaadamu wetu. Ile ni miili ya ndugu,jamaa na marafiki zetu.Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,bado haikupoteza thamani yake kama ni miili ya binaadamu na hivyo heshima,staha na taratibu zilipaswa kufuatwa. Majibu kuhusu wapi imetoka miili ile ya Bunju hapa hayatakuwa na uzito bila ya kwanza kukubali kuwa kulikuwa na makosa juu ya kushughulika na miili ile.

Kwa majibu yoyote, hali ile haivumiliki. Iwe imetokea IMTU au kwingineko, yupo mtu au wapo watu wa kuwajibika. Hata kama ilikuwa ikitumika kisayansi,zipo taratibu za kushughulikia miili ile ikiwa ni pamoja na namna ya kuiteketeza.Mifuko ya rambo si namna ya kuiteketeza hata kama mimi si mwanasayansi. Kuitupa si jambo linalokubalika. Kwanza,kuitupa kiholela vile,kulihatarisha amani.Yangekosa mabomu ya Polisi,muda huu yangezungumzwa mengine.

Nitoe rai kwa wahusika wote wa sakata la jana la miili ya Bunju kujipima na kuwajibika. Tasnia yoyote ina miiko yake. Ya sayansi jana ilikiukwa. Yupo wa kuwajibika. Atambuliwe au ajitambue na kuwajibika haraka iwezekanavyo.
Taifa hili sasa linalazimishwa kuonekana kama la MAJUHA, YAANI CHIBI KUMEOZA, KATI KUMEOZA NA JUU AMBAKO NDIO KUNA RUNGU LA MAAMUZI KUMEOZA
 
Taifa hili sasa linalazimishwa kuonekana kama la MAJUHA, YAANI CHIBI KUMEOZA, KATI KUMEOZA NA JUU AMBAKO NDIO KUNA RUNGU LA MAAMUZI KUMEOZA
Maana yake ni kwamba hakutakuwa na wa kuwajibika wala kuwajibishwa, subiri uone watakavyosukumiana lawama na kila mmoja kujaribu kukwepa kadhia hii.
 
Mkuu naelewa yote hayo na elimu niliyonayo ni zaidi ya Sayansi ya form two; na hata sasa niko nje ya Tz nikipata elimu zaidi.
Bravo,tuwakilishe vyema!
Ni kweli chemicals zinabadilishwa kwa sababu ya expiry period. Sasa vipi kuhusu miili ya binadamu mabaki/residual aka cadaver za binadamu kama teaching aids, zinapotupwa ina maana miundo/mifumo (anatomy) ya binadamu imebadilika na sasa madaktari wanatakiwa kusomo mifumo mingine. Just kidding lakini, nataka utumie nafasi hii kutoa elimu kwa Umma kuhusu tiba ya binadamu, ingekuwa kule SUA jamii ingeona cadaver za wanyama ama sivyo ????
Ndo mana nikasema ni uzembe katika uwajibikaji!Hawakutakiwa kutupa mahala pale maana huwa kuna tanuru maalum la kuteketeza vitu hizo.
Anyway, najua maiti zinatumika na hata kuazimwa kutoka mabara mengine, lakini ni siri ila kwa sababu ya uzembe na kutowajibika uliopo nchni mwetu siku hizi ndio maana haya yamegundulika na jamii za kawaida na kuanza kushangaa. Lakini vle vile afadhali limetokea na kutmika kama sehemu ya elimu kwa umma kuhusu taaluma ya matibabu. Mtu anapoenda hospitali, Daktari akafanyia operation na kushona au anaposafishwa kidonda ina maana Daktari au Muuguzi alishazoezwa kuona vitu kama hivyo, mtu wa kawaida kuona maiti tu ndani ya mortuary ni kazi,

Ndo maana yake.
 
Back
Top Bottom