Viva Lissu, Viva! Pamoja nawe ukombozi utapatikana!

Viva Lissu, Viva! Pamoja nawe ukombozi utapatikana!

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Imepita miaka 30 ya mahangaiko na watu wenye kununulika. Bado tu nini hakijaeleweka? Kwamba ni ubinafsi kwenda mbele hoja zero?

Yaliwakuta kina Mrema na pia kina Maalim Seif. Hao wakalazimika kushusha na kupandisha tanga. Zilizokuwa NCCR na CUF zikageuka Chausta.

Kwamba binadamu ni viumbe wa ajabu?

Laiti kina Mabere au yule mwingine wangejua. Kwa hakika wasingethubutu.

Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Kwamba tulipo yatupaswa kuelezana ukweli, sasa hadharani kwa sababu kuna waliotupia masikio ya kenge? Si bure!

Lisemwalo lipo, kama halipo linakuja:

1. Lissu aongezewe ulinzi. Kwa sasa, dhidi ya maadui wa ndani na nje.
2. Kuondoka chadema siyo option, tuna banana hapa hapa!
3. Kama busara haitamalaki, demokrasia na ichukue mkondo wake sasa!

Kwamba vyama vya siasa si mali binafsi, tusitishane wala kupeana ushauri au kuchagizana awaye yote kuondoka.

Waondoke wao na COVID-19 wao ikiwapendeza.

Wengi wape ndivyo demokrasia inavyotaka.

Kwa hakika "the majority will not miss them!"
 
Mkuu nani asiyejua?

Ni Proved, JokaKuu, Retired, imhotep au Economist, Erythrocyte, Mshana Jr wasiojua shida Iko wapi?

Kwamba chadema liability ni nani?

Kwamba hatuna matumaini ya kupata katiba mpya?

Mzigo ni nani? Lissu au Mwamba?

..wanaozuia Katiba Mpya ni CCM.

..wanaozuia Tume Huru ni CCM.

..CCM ndio wanaosababisha migogoro ktk vyama vya upinzani.

..wengine mambo haya tumeyashuhudia kwa Nccr, Cuf, na sasa Chadema.
 
..wanaozuia Katiba Mpya ni CCM.

..wanaozuia Tume Huru ni CCM.

..CCM ndio wanaosababisha migogoro ktk vyama vya upinzani.

..wengine mambo haya tumeyashuhudia kwa Nccr, Cuf, na sasa Chadema.

CCM azuie vipi kama wenye kupigania kitu ni hawa wa aina ya washirika wa COVID-19?

CCM wasababishe mgogoro vipi kama si yale ya kumlaumu shetani kwa kutenda dhambi?

Ni CCM wa kulaumiwa kwa kukosekana demokrasia chadema?

Ni CCM wa kulaumiwa kwa sisi kuwaendekeza chawa wenye kutaka kutamalaki ndani ya chadema ya leo?

CCM wa kulaumiwa kwa chadema kuacha misingi yake?

CCM wa kulaumiwa kwa wanachadema uchwara kuendekeza mahaba kwa kiongozi yeyote anayeajiri chawa mitandaoni?

Unadhani wanayosema kina Msigwa ni uongo?

Si kuwa huu ukondoo wetu chamani ndio unaotugharimu?

Si kuwa kina Economist walipoandika uzi huu labda hata wewe ulihusika kuwatisha waka retract?

Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Kwamba misingi mingi ya chama imeachwa na kuwa Mbowe Yuko kwenye kung'ang'ania madaraka Kwa sababu zake binafsi nani asiyejua?

Kwamba kumekuwa na lengo la kumvuruga Lissu kama vipi aondoke, nani asiyejua?

Proved, imhotep hatuwezi kufika mahali tukawa wakweli kwetu wenyewe?

Wako wapi wale wa aina za kina Erythrocyte, denoo JG, Retired, Mshana Jr au wale wakitutafutia "bans" kama ikibidi kwa kuandika tunayoamini ila tu ati kuwa wao ni wasiyoyapenda?

Ukweli mchungu:

"Mgogoro huu chimbuko lake ni kukosekana demokrasia na Mbowe hawezi kujivua uwajibikaji!"
 
CCM azuie vipi kama wenye kupigania kitu ni hawa wa aina ya washirika wa COVID-19?

CCM wasababishe mgogoro vipi kama si yale ya kumlaumu shetani kwa kutenda dhambi?

Ni CCM wa kulaumiwa kwa kukosekana demokrasia chadema?

Ni CCM wa kulaumiwa kwa sisi kuwaendekeza chawa wenye kutaka kutamalaki ndani ya chadema ya leo?

CCM wa kulaumiwa kwa chadema kuacha misingi yake?

CCM wa kulaumiwa kwa wanachadema uchwara kuendekeza mahaba kwa kiongozi yeyote anayeajiri chawa mitandaoni?

Unadhani wanayosema kina Msigwa ni uongo?

Si kuwa huu ukondoo wetu chamani ndio unaotugharimu?

Si kuwa kina Economist walipoandika uzi huu labda hata wewe ulihusika kuwatisha waka retract?

Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Kwamba misingi mingi ya chama imeachwa na kuwa Mbowe Yuko kwenye kung'ang'ania madaraka Kwa sababu zake binafsi nani asiyejua?

Kwamba kumekuwa na lengo la kumvuruga Lissu kama vipi aondoke, nani asiyejua?

Proved, imhotep hatuwezi kufika mahali tukawa wakweli kwetu wenyewe?

Wako wapi wale wa aina za kina Erythrocyte, denoo JG, retired, Mshana Jr au wale wakitutafutia "bans" kama ikibidi kwa kuandika tunayoamini ila tu ati kuwa wao ni wasiyoyapenda?

Ukweli mchungu:

"Mgogoro huu chimbuko lake ni kukosekana demokrasia na Mbowe hawezi kujivua uwajibikaji!"

..basi tuseme Ccm ni malaika.

..Na Chadema ni mashetani.
 
..basi tuseme Ccm ni malaika.

..Na Chadema ni mashetani.

Wapi nimesema lolote kuwahusu CCM?

Kwanini jitihada za kutafuta visingizio?

Kuna kibanzi machoni petu wewe unatafuta boriti CCM?

CCM anahusika vipi na demokrasia chadema?

Ila Mwamba humwoni?
 
Wapi nimesema lolote kuwahusu CCM?

Kwanini jitihada za kutafuta visingizio?

Kuna kibanzi machoni petu wewe unatafuta boriti CCM?

CCM anahusika vipi na demokrasia chadema?

Ila Mbowe humwoni?

..sio kwamba sioni tatizo la Mbowe.

..lakini CCM ni tatizo kubwa zaidi.

..Mbowe anaweza kuwa mlarushwa.

..lakini walarushwa wakubwa zaidi wako CCM.

..juzi Tanzania imepigwa bilioni 120 kwa kesi iliyotokana na upumbavu wa viongozi wanaotokana na CCM.

..kuna kesi nyingine imefunguliwa Tanzania inadaiwa Trillion kwa maamuzi mengine ya kipumbavu ya viongozi wa CCM.

..Sasa katika mazingira hayo unataka Watanzania tushughulike na Mbowe kwanza, au tushughulike na CCM?
 
Ndugu jikite kwenye hoja.

Kuna tatizo si dogo chadema.

Mvunja nchi mwananchi. Mvunja chadema ni mwana chadema.

Kulikoni mbaazi kukosa maua na kusingizia jua?

Hata kama CCM anahusika kwenye mgogoro chadema, mjinga hapo ni nani CCM au chadema?

Kwani hujui wajibu wa mshindani? Au kwa mawazo yako ni kukushangilia?

Ya kwamba tuna mawazo duni hivi kweli? Kwamba nchi tunategemea kupewa au kuchukua?!
 
Kwamba Economist alitishwa, uwepo wa chawa, au agenda ya kutofautiana bans? Au kwamba chimbuko ni kukosa demokrasia chamani?

Au wewe Kila kitu ni sawa isipokuwa COVID-19 tu? Au Msigwa kuondoka sawa na kama vipi Lissu naye akafie mbele ila Mwamba na afanye lolote atakalo?

..Na CCM kubaki unaona ni sawa.
 
..Na CCM kubaki unaona ni sawa.

CCM kubaki wapi ndugu? Kama ni madarakani kama wapinzani wajinga, ungetaka wawasaidie kuwang'oa madarakani?

Hudhani demokrasia ingetamalaki chadema, CCM hata kama angekuwa adui angepitia wapi?
 
Ndugu jikite kwenye hoja.

Kuna tatizo si dogo chadema.

Mvunja nchi mwananchi. Mvunja chadema ni mwana chadema.

Kulikoni mbaazi kukosa maua na kusingizia jua?

Hata kama CCM anahusika kwenye mgogoro chadema, mjinga hapo ni nani CCM au chadema?

Kwani hujui wajibu wa mshindani? Au kwa mawazo yako ni kukushangilia?

Ya kwamba tuna mawazo duni hivi kweli? Kwamba nchi tunategemea kupewa au kuchukua?!

..wewe unataka tupambane na " dalili. "

..mimi nakwambia pambana na " ugonjwa. "

..CCM inatafuna nchi wewe unataka kutupotezea muda tupambane na Mbowe?
 
Back
Top Bottom