Vivutio vya utalii Tanzania na faida za utalii wa ndani

Habari mkuu!!!!
Hongera kwa kuanzisha uzi mzuri sana unao tukumbusha kutembelea vivutio vyetu
NIngependa tu kuongezea tu yakua kwa sasa Tanzania Bara ina jumla ya hifadhi 22 ambazo zipo chini ya mamlaka ya usimamizi wa hifadhi Tanzania yaani TANAPA na hii ni kutokana na ongezeko la hifadhi sita (6) mpya ambazo zilikua mapori ya akiba na sasa zimekua hifadhi za taifa.

Hifadhi zilizoongezeka ni
1. Burigi chato National park
2. Nyerere National park
3. Ibanda-kyerwa National park
4.Rumanyika-Karagwe National park
5. Kigosi National park
6. Ugalla river National park.

Pia Tanzaia tumebarikiwa kuwa na bonde la Ngorongoro ambalo lenywe linasimamiwa na (NCAA) yaani Ngorongoro Conservation Area Authority lilianzishwa mwaka 1959 ikiwa lengo lake kubwa ni kulinda lasilimali za wanyamapori pamoja na kuulinda utamaduni wa kimaasai. Hii ni sehemu pekee kwa Afrika ambayo wanyama pamoja na binadamu jamii ya kimaasai huishi kwa pamoja.

Pia Taznzania tumebahatika kuwa na maeneo yanayojulikana kama Game Reserve.
Haya ni maeneo yaliyo anzishwa kwa lengo kubwa la kuhifadhi na kulinda Wanyamapori na mazingira.
Katika maeneo haya ndo sehemu ambapo uwindaji wa wanyamapori hufanyika lakini ni kwa kibali maalumu.
mfano wa sehemu hizo ni Moyowosi game reserve, Usangu game reserve nk.

Pia tuna sehemu za kuvutia zijulikanazo kama Marine park and reserve.
Haya ni maeneo yyalianzishwa kwa sharia ya Marine park and reserve act no.29 of 1994 ikiwa na lengo la kulinda maeneo haya hasa kwakua ni maeneo muhimu kwa uzalianaji wa samaki, kulinda matumbawe, kulinda mikoko, kulinda mazalia ya ndege na viumbe vidogo vidogo vya majini.
Maeneo haya ni
1.Bongoyo island marine reserve
2.Mbudya island marine reserve
3.Pangavini island marine reserve
4.Funguyasini island marine reserve
Hivo vyote vinapatikana dar es saalam

Pia vipo
1. Mafia island marine park-Mafia pwani
2.Mnazi bay Ruvuma estuary marine park-Mtwara


Nikipata mda ntaeelezea kuhusu Wildlife management areas,Game controlled areas,Forest reserve na Historical sites.
 
Naaam! Vizuri sana, hivi karibuni natia nanga na kutumia mfumo wa "Kata Funua, 323 by 8" katika kuelezea na kuonyesha masuala mbalimbali ya kitalii na historia tanabiha.
 
Asante Sana Kiongozi.
 
Y
Hivi ndo lile ziwa wanalosema watu huruhusiwi kuoga...!
Haswaa japo niimani zauongo tu watu wanadai wengi wanaenda kuogelea japo sio sehemu zote maana ni ziwa lililotokana na mlipuko wa volcano (historical theories).

Ukija kwa wasafwa ambao ni wenyeji wanakwambia, lilimeza mtu likakimbia na kwenda kujifisha pale juu ya mlima.
 

Gharama ni kubwa sana kufanya utalii kwa mtu wa kawaida
 
Uzi unaleta burudani umeshusha madini ya uhakika.nimejifunza kitu,baadhi ya nyuzi Kama hizi wengine ndo zilitushawishi kujiunga JF.mambo ni fire [emoji91][emoji91][emoji91].Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika[emoji1241]

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Follow me on Twitter for tourism and wildlife fact in Tanzania
Karibuni wadau hapa utapata taarifa zote za Utalii nchini Tanzania
 
>>Hili ni tangazo la biashara. Naamini limelipiwa inavyostahili.

>>TANAPA na mamlaka zingine za utalii punguzeni viingilio kuvuta wazawa zaidi kutembelea vivutio hivi. Mkumbuke kutalii sio sehemu ya utamaduni wetu.
 
Baada ya kchombo kikubwa cha habari duniani CNN kulitaja eneo la ngorongoro kuwa eneo namba moja ambalo kila mtalii duniani angetamani kuliona afrika kampuni ya fasaribookings.com ineitaja nchi yetu ya Tanzania kuwa ndio nchi yenye vivutio vingi duniani .

Tunaipongeza serkali ya awamu ya tano kwa kuzidi kupiga hatua katika kujitangaza kuvutia watalii


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa unamapenzi ya dhati kwili na hii awamu ya 5,? au kunamgao unapata maana kila baada ya nusu saa lazma uanzishe uzi hum jukwaani

Ni hayo tu:
 
Tanzania hua inaongoza kila kitu, mara uchumi, mara umasikini, utasikia Magufuli anaongoza. Hata sijui nini hatuongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…