[emoji38][emoji38][emoji38]! Huo mpango niliwahi ufanya! Nilitamani kununua nyumba, hela toka mkopo wa bank A ikawa haitoshi!
Nilichofanya ni kuongea na kijana wangu wa hazina anisimamishie makato kwa mwezi mmoja ikaja pay slip "safi", nikachukua tena fomu na kwenda bank B kukopa na nikafanikiwa.
Sasa bank zote zikawa zinanyang'anyana mshahara wangu kama mafisi wagombeavyo mzoga, mi nawachora tu nikiwa ndani ya mjengo.
Zoezi hilo hadi kumalizika inabidi uwe umejizatiti kisaikolijia hasa na uwe na miradi ya kukuongezea kipato iliyosimama sawasawa, vinginevyo utakuwa kama umefukuzwa kazi kwa aibu.
Maana na ile furaha ya mwisho wa nwezi ya: "leo mshahara umetoka",inakuwa haikuhusu na hautakiwi kulalamika popote!
Sent using
Jamii Forums mobile app