Viwango vya mishahara kwa walimu: Ualimu ni mateso

Sasa kutaja alfabeti bila kuweka kiwango cha pesa wanacholipwa ni kutuumiza tu macho kusoma sisi tusioelewa hizo kanuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko Afya nasikia kamshahara ni kanono kidogo tofauti na Kilimo,pia visemina vipo vingi.
Ni kawaida ila wanazidi walimu kidogo.

Mfano: Nurse ngazi ya cheti anapata Tsh 432,000 lakini anafanya kazi ngumu, anafanya kazi mpaka usiku na Weekends.

Likizo ni siku 28 mara moja kwa mwaka.

Lakini Mwalimu wa ngazi hiyo hiyo anapata Tsh 419,000. Hapa mwalimu kila wanafunzi wakifunga shule, na yeye anafunga.

Mwisho kazini ni saa 9:30 anarudi nyumabni.

Sasa hapo ndio utaona wapi kuna afadhali.
 
Unashangaa laki tatu hiyo ni kubwa sana,kuna watu wana 120000/100000/80000 na maisha yanaendelea asilimia za mkopo zilipoongezwa jamaa walikuwa wanakomba kila kitu pasipo kujari sheria ya kubakiza one third.
[emoji38][emoji38][emoji38]! Huo mpango niliwahi ufanya! Nilitamani kununua nyumba, hela toka mkopo wa bank A ikawa haitoshi!

Nilichofanya ni kuongea na kijana wangu wa hazina anisimamishie makato kwa mwezi mmoja ikaja pay slip "safi", nikachukua tena fomu na kwenda bank B kukopa na nikafanikiwa.

Sasa bank zote zikawa zinanyang'anyana mshahara wangu kama mafisi wagombeavyo mzoga, mi nawachora tu nikiwa ndani ya mjengo.

Zoezi hilo hadi kumalizika inabidi uwe umejizatiti kisaikolijia hasa na uwe na miradi ya kukuongezea kipato iliyosimama sawasawa, vinginevyo utakuwa kama umefukuzwa kazi kwa aibu.

Maana na ile furaha ya mwisho wa nwezi ya: "leo mshahara umetoka",inakuwa haikuhusu na hautakiwi kulalamika popote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka gani huo ?
 
Huko Afya nasikia kamshahara ni kanono kidogo tofauti na Kilimo,pia visemina vipo vingi.
Afya
Certificates wote TGHS A-432,000/= Take home 387,700/=
Diploma wote-680,000/= Take home 584k na tuchenji kadhaa
Degree ndipo kuna tofautiana maana scale kwa Nursing, pharmacy na md tofauti mfano Pharmacy degree Tghs d-1.2 M, Md-Tghs E- 1.48M na hizo ni Ajira mpya
 
Kwa hiyo unaturingishia mkuu?
 
Kumbe wapo juu ya Walimu na Kilimo.
 
Dah!!!, Bora ualimu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚eti hutakiwi kulalamika popote. Ila nadhani kwa sasa hivi haiwezekani hii
 
Unakuta wenzako wanasubiri mishahara wewe wala hauwazi kabisa!!kwa siku unaingiza faida ya 80000/= hadi 100000/= tena unawashangaa wanavohaha!!!
Hiyo faida hata mwalimu akitaka kyingiza anaingiza tu.

Ni suala ka akili tu. Kuwa mtumishi haiana maana kwamba umefunhwa mikono usifanye mishe ya pembeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…