Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Katika muongo mmoja uliopita, Marekani imekandamiza kadiri iwezavyo Mpango wa Maendeleo ya Sekta za Utengenezaji za China wa mwaka 2025, ikitumia mbinu mbalimbali kuanzia “kutonunua” hadi “kutouza”, kuweka vikwazo visivyo na kimsingi dhidi ya makampuni ya teknolojia ya juu ya China, hadi kutuza ushuru mkubwa dhidi ya bidhaa za China. Kama aliyekuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang alivyosema, Mpango wa Maendeleo ya Sekta za Utengenezaji za China wa mwaka 2025 unalenga kuongeza uwezo wa utengenezaji wa China, na malengo yote ni wazi. Marekani inapaswa kuwa na imani zaidi na kushindana na China kwa haki na usawa.
Waziri wa zamani wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo hivi karibuni amekiri wazi kwamba “kujaribu kuzuia maendeleo ya China ni jambo lisilowezekana”. Matamshi hayo ni tofauti kabisa na msimamo wake mgumu dhidi ya China wakati alipokuwa madarakani. Mabadiliko haya makubwa yameonesha ugonjwa sugu wa kisiasa wa Marekani dhidi ya China.
Raimondo aliwahi kuwa “nyundo” ya kukandamiza China. Wakati alipokuwa Waziri wa Biashara wa Marekani, zaidi ya makampuni 200 ya China yaliwekwa kwenye “orodha nyeusi” ya wizara yake. Radio ya Kitaifa ya Marekani NBC ilitangaza mahojiano yaliyofanywa kwa njia ya video na Raimondo. Wakati huo, alisema, “Fikiria ikiwa kuna mamilioni ya magari ya China yanayoendeshwa kwenye barabara za Marekani, Wachina wataweza kukusanya data za Wamarekani kila dakika, na Beijing itaweza kuyazima magari hayo yote kwa wakati mmoja.” Matamshi yake hayo yalimfanya hata mwanahabari wa NBC awe na shaka, lakini alisisitiza kuwa ni matamshi kwa ajili ya “usalama wa taifa” wa Marekani.
Hata hivyo, baada ya kuondoka madarakani, Raimondo anaonekana kubadili mtazamo wake. Tarehe 11 mwezi huu, katika Kongamano la Teknolojia na Ubunifu la KPMG, Raimondo alipotoa maoni yake kuhusu ushindani wa China na Marekani katika akili bandia (AI), alisema, anaelewa kwamba China ni mshindani wa kimkakati wa Marekani, lakini Marekani inapaswa kudumisha mawasiliano na China, ama sivyo inaweza kusababisha maamuzi yasiyo sahihi, na kuongeza kuwa, ushirikiano kati ya China na Marekani katika sekta ya AI ni kwa maslahi ya pamoja ya nchi zote mbili. Zaidi ya hayo, Raimondo alipinga wazi sera za Marekani za kukandamiza China akisema, kujaribu kuizuia China ni hatua isiyo na mantiki, na ni sawa na mashindano ya mbio, kwani unaweza kuvuta shati la mpinzani wako, lakini kitendo hicho hakiweza kuleta ushindi. Ili kudumisha ushindi, inapaswa kukimbia kwa kasi zaidi, na huo ndio ufunguo wa mafanikio.
“Kuamka” kwa Raimondo kumeonesha Marekani imekuwa na ugonjwa sugu wa kisiasa dhidi ya China. Misimamo mikali dhidi ya China imekuwa kichocheo cha bei rahisi cha kisiasa, na kushangiliwa mara moja kwa kupigiwa makofi na pande mbalimbali. Kama matokeo, fikra za kimantiki zimefutiliwa mbali, uamuzi wa kimantiki umezuiwa, na maafisa wanatembea kwa tahadhari, wakihofia kuwa wanaweza kulaumiwa kuwa “laini kwa China” na kuwa na hatari ya kupoteza nyadhifa zao. Lakini ugonjwa huo wa kisiasa sio kama tu unatia sumu kwa mahusiano ya China na Marekani, bali pia unadhoofisha msingi wa maslahi ya muda mrefu ya Marekani