VoA: Lissu aomba Rais Magufuli kufanya maridhiano na wapinzani wake

Hayo masanduku yako wap wakuu, mliowakamata wapo wapi wenye hayo masanduku ili twende mahakamani , hata kama sio kisutu pelekeni huo ushahidi huko ICC..... Sometyme naona kama nyie ni wataabishaji wa Taifa , JPM ana mapungufu shazi ila somtyme ni far better kuliko hlo genge la wahuni , mnaloose focus mapema Sana , ....
Genge la wahuni mpaka mnapiga [push up kuomba kura, mnaiba kijinga mpaka chekechea wanacheka!
 
Anaona aibu alivyoisambaratisha CHADEMA kwa kipindi kifupi. Hata hajui nini kimetokea.
Ndio kibaraka wa mhutu , Lengai Ole Sabaya Pimbi mkubwa Jiwe akitoka kibarua hamna tena , kwahiyo Ni kuunga mkono umwagaji damu ili mkono uende kinywani mataga .
 
Alafu nikwambie mkuu Lissu anakijua kinachokuja mbele ndo mana ameshauri ivo, kwani anajua jiwe hawez kukubali, kifupi Lissu amejiondoa kwenye lawama kubwa zijazo kutokana na anayoyaona mbele
 
Hayo masanduku yako wap wakuu, mliowakamata wapo wapi wenye hayo masanduku ili twende mahakamani , hata kama sio kisutu pelekeni huo ushahidi huko ICC..... Sometyme naona kama nyie ni wataabishaji wa Taifa , JPM ana mapungufu shazi ila somtyme ni far better kuliko hlo genge la wahuni , mnaloose focus mapema Sana , ....
Kura hizo wanajua ni kura feki walizotengeneza na kutoa photocopy. Karatasi zote zina serial number moja. Hakuna popote wanakubali kuzionesha
 
Alafu nikwambie mkuu Lissu anakijua kinachokuja mbele ndo mana ameshauri ivo, kwani anajua jiwe hawez kukubali, kifupi Lissu amejiondoa kwenye lawama kubwa zijazo kutokana na anayoyaona mbele

Unajitahidi kweli kumtetea huyo takataka hata kwa mambo ambayo yako wazi kwa kila mtu kuona, unazidi kudhihirisha jinsi gani IQ yako isivyotosha kutatua matatizo, ...
 
Swaga za Lumumba!

Acha kupotosha! Kaulizwa nini angemshauri Magufuli na ndio akajibu angemshauri yafanyike maridhiano na hili la maridhiano haliajaanza kuzungumziwa leo. Au wewe mtu kutoa ushauri kama alivyotakiwa ndio kulegea?

Alafu mbona hujaongelea aliposema utawala huu kuwa ni wa kikatili na akaonya miaka mitano ijayo itakuwa migumu zaidi?

Mbona hujaongelea aliposema kakimbia kuokoa maisha yake ili aendeleeze mapambano?

Kasema wazi ni bora aendelee kuwa hai ili aendeleze mapambano kwani akifa hatoweza kuendeleza mapambano na ndio maana aliona ni bora kwanza awoke maisha yake ili apate nafasi ya kuendelea mapambano.
Wewe unasimaje mkuu. Yoote kayaandika wewe unasema hakuandika!!
 
Hayo masanduku yako wap wakuu, mliowakamata wapo wapi wenye hayo masanduku ili twende mahakamani , hata kama sio kisutu pelekeni huo ushahidi huko ICC..... Sometyme naona kama nyie ni wataabishaji wa Taifa , JPM ana mapungufu shazi ila somtyme ni far better kuliko hlo genge la wahuni , mnaloose focus mapema Sana , ....

Katika mahojiano aliyofanya leo na VOA, Lissu amekiri kuwa Watanzania wamempuuza kwa kutokuandamana pamoja na yeye kutoa wito huo kwa nguvu zote.

Amesema hata kabla ya uchaguzi aliwahimiza watanzania kuwa tayari kuingia barabarani lakini bado haikusaidia, Watanzania walimgomea. Ametulaumu watanzania kuwa hatujawa tayari kwa mabadiliko.

Alipouulizwa akikutana na Rais Magufuli kwa sasa atamwambia ujumbe gani. Kwa unyenyekevu huku akimwita 'Mheshimiwa Rais Magufuli' na siyo tu kumwita casually Magufuli alivyozoea kumwita, Lissu amemwomba akubali kusamehe akitumia neno 'arudi nyuma' na akubali maridhiano na kusema hapendi kutumbukia kwenye shimo. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kupitia VOA ya tarehe ya leo.

My take:
Lissu ameshaelewa kuwa Watanzania wamemshtukia na wanampuuza.

Amesalimu amri na ameanza kulegea na sasa anaanza kulialia na kuomba maridhiano. Kwa mara ya kwanza anaanza kuimba wimbo wa maridhiano.

Tuombe uzima, tutaona upande mwingine wa shilingi kwa huyu Tundu Lissu. Wana CHADEMA bakini na maneo ya akiba, muda si mrefu mtabadilisha majina yenu ya JF na kukimbia jukwaa.

===========

MTANGAZAJI: Safari yako ya kwenda hapo ubelgiji imeibua hisia mseto, hebu tueleze umefikaje na kwanini?

LISSU: Nimefika Ubelgiji jana asubuhi nikitokea Tanzania ambako niliondoka juzi mchana na nimeondoka kwa sababu usalama wangu ulikuwa mashakani. Tangu baada ya uchaguzi nilianza kupata vitisho kwenye simu kwamba kuna amri imetolewa ya kunimaliza na kwa mtu ambae nimepitia niliyoyapitia mie ya kushambuliwa kwa risasi na karibu kuuliwa miaka mitatu iliyopita, hivi vitisho nilivipa uzito mkubwa sana na kwahiyo nilifanya jitihada ya kwanza kujificha na baadae nilikimbia ubalozi wa Ujerumani ambako nilikamatiwa nje na polisi lakini baadae maafisa wa kibalozi waliingilia kati na nikaachiliwa a baadae nikakaa kwa balozi wa Ujerumani nchini Tanzania kwa siku nane mpaka nlipoondoka kuja huku.

MTANGAZAJI: Kuna swali limeulizwa kwenye mitandao ya kijamii hivi leo kwamba mheshimiwa Lissu atahutubia Bunge la Jumuiya ya umoja wa Ulaya, zungumzia hilo, ni kweli si kweli!

LISSU: Mimi napenda sana kukaribishwa kuhutubia vikao kama hivyo lakini hili linalozungumzwa mitandaoni ni porojo tu za mitandaoni, mimi sijaomba wala kuombwa kuhutubia kikao chochote cha Bunge la Ulaya kwa hiyo hayo ni mambo ya kutunga ya mitandaoni tu na wanayoyatunga wana sababu zao.

MTANGAZAJI: Kwa wale wanaosema Tundu Lissu amteroka Tanzania, ameachiwa wengine kufanya kazi, labda arejee tena kuwania Urais, ungewaambia nini? Wanaona kama ni kusaliti labda ungekaa nao mpambane pamoja. Msukumo uliokuwa umetangaza wewe na viongozi wengine wa kisiasa kwamba watanzania watokee kwa wingi kwenye barabara za Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi, msukumo huo bado upo? Kama upo i nini hasa kwa mawazo yako iwe hatma yake.

LISSU: Sijatoroka kama nilivyosema nimeondoka Tanzania mchana kweupe, nimepitia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, nimepita kwa passport ya Tanzania niliyopewa na serikali siku ya Jumatatu, kwa hiyo sijatoroka lakini nilichofanya nimeondoka ili kuokoa maisha yangu. Sasakwa watanzania wenzangu sharti wafahamu kwamba ni muhimu kuendelea kuishi ili niweze kupambana kesho na keshokutwa, nikikaa nikauawa basi safari ya mapambano yakwangu angalau itakuwa imeishia hapo na mimi nataka niendelee na mapambano ya kudai demokrasia, ya kudai nchi ambayo tunastahili na inabidi ili niendeleze mapambano inabidi niwe hai, inabidi kukimbia kujiokoa ili kuishi na kupigana siku nyingine, ndicho nilichofanya.

Hatma ya siasa za Tanzania, ni wazi wito wa kupinga matokeo ya uchafuzi uliofanyika tarehe 28 Oktoba haukuitikiwa na watanzania, nilisema wakati wote wa kampeni endapo uchaguzi na watawala wa sasa, wananchi wachukue hatua ya kulinda demokrasia yao wao wenyewe na ndichi nilichofanya niliitisha watu wajitokeze kuchukua hatma ya nchi yao kwenye mikono yao, hawakufanya hivyo sio kwa sababu mimi sikutoa wito, inaelekea kwasababu wananchi hawako tayari kupambania haki zao kwa hiyo tuendelee siku zijazo. Kwa tafsiri yangu tu, kwa hii miaka mitano iliyopita, miaka mitano ijayo itakuwa migumi sana kwa nchi yetu kwa kuzingatia aina ya mtawala ambae tunae, Rais Magufuli amedhihirisha wazi jinsi ambavyo ni mtawala katili, asiyejali demokrasia, haki za binadamu, uchumi wa nchi yetu na kwahiyo miaka mitano inayokuja itakuwa miguma sana kwa watanzania wa kila aina.

MTANGAZAJI: Kuna wito mliotoa kwa jumuiya ya kimataifa iafanye juu chini mnapata haki na uchaguzi haukufanyika ambavyo mlitarajia ungefanyika, swali langi ni hasa katika jumuiya ya Afrika Mashariki katika ujirani huo wa Tanzania, unaweza kusema wamefanya vya kutosha kushinikiza ama kuwasaidia kwamba mnapata haki kama ambavyo mliuliza.

LISSU: Jumuiya ya Afrika Mashariki haijafanya kile ambacho ilitakiwa ikifanye kwa maana ya kwamba mimi nafahamu na nafahamu kwa sababu nilizungumza na waangalizi wa umoja wa Afrika ulioongozwa na Goodluck Jonathana na waliniambia wao pamoja na waangalizi wa EAC walishuhudia matukio mengi ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kwa namna ambayo wasingeweza kusema uchaguzi huu ulikuwa huru wala wa haki kwa yale ambayo wao wenyewe waliyashuhudia a kuyapiga picha masanduku ambayo yalikuwa yameshajazwa kura na kuwekwa kwenye vituo vya kupigia kura kabla zoezi la kupiga kura halijaanza. Sasa ripoti waliyotoa EAC inasema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki ni ripoti ya uongo, hatukutegemea kwamba waangalizi hawa wangeweza kuzungumza hivyo baada ya kushuhudia hayo ambayo tunaambiwa waliyashuhudia lakini tusistaajabu sana, Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi gani na zinaongozwa na watawala wa aina gani ukiachia Kenya ambayo demokrasia yake iko mbele zaidi katika hiyo Jumuiya, nchi nyingine zote zilizobaki ndio hizo za kina Museveni, Rais wa maisha, Generali Kagame, Rais wa maisha, Burundi ndio hivyo tena na Magufuli anaelekea kuwa Rais wa maisha. Wengine tunasubiri ripoti ya AU.

MTANGAZAJI: Mwisho, kama ungepata nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli hivi leo, ungemwambia nini?

LISSU: Ningemwambia mheshimiwa Rais itisha mkutano wa kitaifa wa maridhiano tutengeneze nchi ambayo makundi mbalimbali ya kisiasa yataridhiana, tuwe na nchi ambayo itakuwa na umoja wa kitaifa, huko unakoelekea unaenda kututumbika sisi wote katika shimo kubwa na na nchi yetu inaweza kuangamia, rudi nyuma, fanya maridhiano tujenge nchi kwa pamoja, tujenge nchi ya kidemokrasia na nchi ambayo itakuwa sehemu ya Jumuiya ya kimataifa, sisi tunahitaji dunia zaidi kuliko dunia inavyotuhitaji, usifikiri kwamba unaweza kuishi peke yako katika dunia hii ambayo kila mtu anahusiana na mwingine.

MTANGAZAJI: Nikushukuru sana Tundu Lissu kwa kuzungumza na sauti ya Amerika

LUSSU: Asante sana kaka BMJ kwa kunipa nafasi hii

----MWISHO----​

View attachment 1626195

My take:
Lissu ameshaelewa kuwa Watanzania wamemshtukia na wanampuuza.

Amesalimu amri na ameanza kulegea na sasa anaanza kulialia na kuomba maridhiano. Kwa mara ya kwanza anaanza kuimba wimbo wa maridhiano.

Tuombe uzima, tutaona upande mwingine wa shilingi kwa huyu Tundu Lissu. Wana CHADEMA bakini na maneo ya akiba, muda si mrefu mtabadilisha majina yenu ya JF na kukimbia jukwaa.
Nonsense kabisa. Maridhiano na msaliti.???
 
Kura feki zimetengenezwa na CHADEMA kuhadaa wananchi ndiyo maana wanazichoma badala ya kuzitumia kama ushahidi. Wanajua wangezipeleka police wangeumbuka. Umeona wapi mtu anakamata ushahidi kisha anauharibu/anachoma ushahidi huo?
Ndivyo Polepole alivyokufundisha ujibu?
umequote video moja tu, hiyo video nyingine kura zimepekuliwa mbele ya Mapolisi unajifanya hujaiona eh, au unataka kusema na Mapolisi nao wamo kwenye mchongo wa Chadema?
 
Mikura feki ilitapakaa kila mahali
Inaelekea waliotoka kifungoni baada ya mitandao kufungwa, hawajui kuwa hizi videos za wizi wa kura wa waziwazi zilitrend sana kwenye social media kwa wale waliokuwa wana access ya mtandao
 
Ndivyo Polepole alivyokufundisha ujibu?
umequote video moja tu, hiyo video nyingine kura zimepekuliwa mbele ya Mapolisi unajifanya hujaiona eh, au unataka kusema na Mapolisi nao wamo kwenye mchongo wa Chadema?
Lakini wewe uliona wapi kielelezo kinaharibiwa na mlalamikaji? Kama mlalamikaji kaharibu kielelezo ataithibitishia vipi mahakama kosa pasipo kuacha shaka yoyote?
 
Mbona kama hata mwezi haujaisha tangu kufanyika kwa uchaguzi ambapo tuliambiwa huko chako kuna mtu kajijengea airport yake na mama yake, ameua watu wa kwao na kuwatumbukiza majini, ni dikiteta, ni mshamba, hajui kuandika hata sentensi moja ya kiingereza iliyo sahihi, elimu yake ina mashaka, amejitajirisha kwa makumi ya maelfu ya eka ya aridhi, ameiba kura, anamtafuta Lisu amuue, ni muuaji wa genocide, and blah blah blah. Then eti leo anatwambia eti yuko tayari kukaa naye mezani kuzungumzia maridhiano! So, nadhani huyu mtu aanze kukaa kwanza mezani na Amsterdam wamwandikie JPM barua ndefu ya kumwomba msamaha kwa kumharibia jina lake mwenyewe na Tanzania kama taifa.

Tundu buana
 
Lakini wewe uliona wapi kielelezo kinaharibiwa na mlalamikaji? Kama mlalamikaji kaharibu kielelezo ataithibitishia vipi mahakama kosa pasipo kuacha shaka yoyote?
Tatizo mlikuwa mmefungiwa mitandao ndiyo maana hamjui kuwa Viongozi wa Chadema waliitisha press conference na kuzionyesha baadhi ya kura zilizokamatwa!

Kuna hiyo video ya ACT Wazalendo wanakuonyesha mikura waliyoikamata!

Kuna video huko Juu Mapolisi nao wamekamata kura, sasa unataka kuwauliza polisi kidhibiti kiko wapi?

Uchaguzi wa Raisi hauhojiwi mahakamani na ni dhahiri hiyo ni gemu iliyosukwa na mamlaka husika, hata ukienda mahakamani, kwa mahakama hizi za CCM ni kupoteza muda. Kwenye awamu hii mahakama imegeuka kuwa ni Kigoda cha Jiwe kukanyagia pindi anapopora haki za wananchi!
 
Katika mahojiano aliyofanya leo na VOA, Lissu amekiri kuwa Watanzania wamempuuza kwa kutokuandamana pamoja na yeye kutoa wito huo kwa nguvu zote.

Amesema hata kabla ya uchaguzi aliwahimiza watanzania kuwa tayari kuingia barabarani lakini bado haikusaidia, Watanzania walimgomea. Ametulaumu watanzania kuwa hatujawa tayari kwa mabadiliko.

Alipouulizwa akikutana na Rais Magufuli kwa sasa atamwambia ujumbe gani. Kwa unyenyekevu huku akimwita 'Mheshimiwa Rais Magufuli' na siyo tu kumwita casually Magufuli alivyozoea kumwita, Lissu amemwomba akubali kusamehe akitumia neno 'arudi nyuma' na akubali maridhiano na kusema hapendi kutumbukia kwenye shimo. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kupitia VOA ya tarehe ya leo.

===========

MTANGAZAJI: Safari yako ya kwenda hapo ubelgiji imeibua hisia mseto, hebu tueleze umefikaje na kwanini?

LISSU: Nimefika Ubelgiji jana asubuhi nikitokea Tanzania ambako niliondoka juzi mchana na nimeondoka kwa sababu usalama wangu ulikuwa mashakani. Tangu baada ya uchaguzi nilianza kupata vitisho kwenye simu kwamba kuna amri imetolewa ya kunimaliza na kwa mtu ambae nimepitia niliyoyapitia mie ya kushambuliwa kwa risasi na karibu kuuliwa miaka mitatu iliyopita, hivi vitisho nilivipa uzito mkubwa sana na kwahiyo nilifanya jitihada ya kwanza kujificha na baadae nilikimbia ubalozi wa Ujerumani ambako nilikamatiwa nje na polisi lakini baadae maafisa wa kibalozi waliingilia kati na nikaachiliwa a baadae nikakaa kwa balozi wa Ujerumani nchini Tanzania kwa siku nane mpaka nlipoondoka kuja huku.

MTANGAZAJI: Kuna swali limeulizwa kwenye mitandao ya kijamii hivi leo kwamba mheshimiwa Lissu atahutubia Bunge la Jumuiya ya umoja wa Ulaya, zungumzia hilo, ni kweli si kweli!

LISSU: Mimi napenda sana kukaribishwa kuhutubia vikao kama hivyo lakini hili linalozungumzwa mitandaoni ni porojo tu za mitandaoni, mimi sijaomba wala kuombwa kuhutubia kikao chochote cha Bunge la Ulaya kwa hiyo hayo ni mambo ya kutunga ya mitandaoni tu na wanayoyatunga wana sababu zao.

MTANGAZAJI: Kwa wale wanaosema Tundu Lissu amteroka Tanzania, ameachiwa wengine kufanya kazi, labda arejee tena kuwania Urais, ungewaambia nini? Wanaona kama ni kusaliti labda ungekaa nao mpambane pamoja. Msukumo uliokuwa umetangaza wewe na viongozi wengine wa kisiasa kwamba watanzania watokee kwa wingi kwenye barabara za Tanzania kupinga matokeo ya uchaguzi, msukumo huo bado upo? Kama upo i nini hasa kwa mawazo yako iwe hatma yake.

LISSU: Sijatoroka kama nilivyosema nimeondoka Tanzania mchana kweupe, nimepitia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, nimepita kwa passport ya Tanzania niliyopewa na serikali siku ya Jumatatu, kwa hiyo sijatoroka lakini nilichofanya nimeondoka ili kuokoa maisha yangu. Sasakwa watanzania wenzangu sharti wafahamu kwamba ni muhimu kuendelea kuishi ili niweze kupambana kesho na keshokutwa, nikikaa nikauawa basi safari ya mapambano yakwangu angalau itakuwa imeishia hapo na mimi nataka niendelee na mapambano ya kudai demokrasia, ya kudai nchi ambayo tunastahili na inabidi ili niendeleze mapambano inabidi niwe hai, inabidi kukimbia kujiokoa ili kuishi na kupigana siku nyingine, ndicho nilichofanya.

Hatma ya siasa za Tanzania, ni wazi wito wa kupinga matokeo ya uchafuzi uliofanyika tarehe 28 Oktoba haukuitikiwa na watanzania, nilisema wakati wote wa kampeni endapo uchaguzi na watawala wa sasa, wananchi wachukue hatua ya kulinda demokrasia yao wao wenyewe na ndichi nilichofanya niliitisha watu wajitokeze kuchukua hatma ya nchi yao kwenye mikono yao, hawakufanya hivyo sio kwa sababu mimi sikutoa wito, inaelekea kwasababu wananchi hawako tayari kupambania haki zao kwa hiyo tuendelee siku zijazo. Kwa tafsiri yangu tu, kwa hii miaka mitano iliyopita, miaka mitano ijayo itakuwa migumi sana kwa nchi yetu kwa kuzingatia aina ya mtawala ambae tunae, Rais Magufuli amedhihirisha wazi jinsi ambavyo ni mtawala katili, asiyejali demokrasia, haki za binadamu, uchumi wa nchi yetu na kwahiyo miaka mitano inayokuja itakuwa miguma sana kwa watanzania wa kila aina.

MTANGAZAJI: Kuna wito mliotoa kwa jumuiya ya kimataifa iafanye juu chini mnapata haki na uchaguzi haukufanyika ambavyo mlitarajia ungefanyika, swali langi ni hasa katika jumuiya ya Afrika Mashariki katika ujirani huo wa Tanzania, unaweza kusema wamefanya vya kutosha kushinikiza ama kuwasaidia kwamba mnapata haki kama ambavyo mliuliza.

LISSU: Jumuiya ya Afrika Mashariki haijafanya kile ambacho ilitakiwa ikifanye kwa maana ya kwamba mimi nafahamu na nafahamu kwa sababu nilizungumza na waangalizi wa umoja wa Afrika ulioongozwa na Goodluck Jonathana na waliniambia wao pamoja na waangalizi wa EAC walishuhudia matukio mengi ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi kwa namna ambayo wasingeweza kusema uchaguzi huu ulikuwa huru wala wa haki kwa yale ambayo wao wenyewe waliyashuhudia a kuyapiga picha masanduku ambayo yalikuwa yameshajazwa kura na kuwekwa kwenye vituo vya kupigia kura kabla zoezi la kupiga kura halijaanza. Sasa ripoti waliyotoa EAC inasema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki ni ripoti ya uongo, hatukutegemea kwamba waangalizi hawa wangeweza kuzungumza hivyo baada ya kushuhudia hayo ambayo tunaambiwa waliyashuhudia lakini tusistaajabu sana, Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi gani na zinaongozwa na watawala wa aina gani ukiachia Kenya ambayo demokrasia yake iko mbele zaidi katika hiyo Jumuiya, nchi nyingine zote zilizobaki ndio hizo za kina Museveni, Rais wa maisha, Generali Kagame, Rais wa maisha, Burundi ndio hivyo tena na Magufuli anaelekea kuwa Rais wa maisha. Wengine tunasubiri ripoti ya AU.

MTANGAZAJI: Mwisho, kama ungepata nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli hivi leo, ungemwambia nini?

LISSU: Ningemwambia mheshimiwa Rais itisha mkutano wa kitaifa wa maridhiano tutengeneze nchi ambayo makundi mbalimbali ya kisiasa yataridhiana, tuwe na nchi ambayo itakuwa na umoja wa kitaifa, huko unakoelekea unaenda kututumbika sisi wote katika shimo kubwa na na nchi yetu inaweza kuangamia, rudi nyuma, fanya maridhiano tujenge nchi kwa pamoja, tujenge nchi ya kidemokrasia na nchi ambayo itakuwa sehemu ya Jumuiya ya kimataifa, sisi tunahitaji dunia zaidi kuliko dunia inavyotuhitaji, usifikiri kwamba unaweza kuishi peke yako katika dunia hii ambayo kila mtu anahusiana na mwingine.

MTANGAZAJI:
Nikushukuru sana Tundu Lissu kwa kuzungumza na sauti ya Amerika

LUSSU: Asante sana kaka BMJ kwa kunipa nafasi hii

----MWISHO----​

View attachment 1626195

My take:
Lissu ameshaelewa kuwa Watanzania wamemshtukia na wanampuuza.

Amesalimu amri na ameanza kulegea na sasa anaanza kulialia na kuomba maridhiano. Kwa mara ya kwanza anaanza kuimba wimbo wa maridhiano.

Tuombe uzima, tutaona upande mwingine wa shilingi kwa huyu Tundu Lissu. Wana CHADEMA bakini na maneo ya akiba, muda si mrefu mtabadilisha majina yenu ya JF na kukimbia jukwaa.
Weka link acha porojo
 
Hivi maridhiano si yanahitaji pande zote mbili ziwe zimekwazana au kununa?

Au mtu akizira akanuna inabidi aliyenuniwa ndo akambembeleze ili asinune? Malezi ya sampuli hii mie nilifikiri mwisho ilikuwa 2015?
 
Back
Top Bottom