Vodacom: Tutawafidia wateja wetu waliopata changamoto ya Mtandao wakiwa wamenunua huduma

Ukipigwa ban useme moderator madikteta
Haaa haaa haaa sasa wanipige ban kwani niko nao ninapotumia internet bure?

Hapa nilipo wamenitumia sms wameniambia watanifidia bando langu mtandao ukikaa sawa ila kwa sasa natumia bure tu sina kifurushi wala nini.

Screeshot hiyo kama unabisha bisha.
Screenshot_20240515-181716_Messages.jpg
 
Dar es Salaam, 15 Mei 2024: Vodacom Tanzania inafuraha kutangaza kuwa huduma ya intaneti imerejea kikamilifu baada ya upungufu wa ubora wa huduma za intaneti nchi nzima. Tulipata changamoto ya kukatika kwa nyaya chini ya bahari hivi majuzi.

Tunaelewa kuwa tukio hili limeleta usumbufu na tunaomba radhi kwa hilo. Kwa sababu hii, wateja wote walioshindwa kutumia huduma ya intaneti watarejeshewa vifurushi vyao.

Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha unapata huduma bora na kasi ya juu kabisa.

Tunakushukuru kwa uelewa na uvumilivu wako.
Imetolewa na:
Uongozi
Vodacom Tanzania PLC
Nasubiri shuhuda kwa ambaye amesharejeshewa mb zake
 
KUNA PESA YANGU ILIGANDA HEWANI TOKA MAJUZI

SASA SIJAJUA KAMA INAHUSIANA NA HITILAFU YA MKONGA
 
Voda wameniwekea 3GB asubuh hii..:naangalia Tigo wameweka 5G zitumike ndani ya week
 
Dar es Salaam, 15 Mei 2024: Vodacom Tanzania inafuraha kutangaza kuwa huduma ya intaneti imerejea kikamilifu baada ya upungufu wa ubora wa huduma za intaneti nchi nzima. Tulipata changamoto ya kukatika kwa nyaya chini ya bahari hivi majuzi.

Tunaelewa kuwa tukio hili limeleta usumbufu na tunaomba radhi kwa hilo. Kwa sababu hii, wateja wote walioshindwa kutumia huduma ya intaneti watarejeshewa vifurushi vyao.

Tunaendelea kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha unapata huduma bora na kasi ya juu kabisa.

Tunakushukuru kwa uelewa na uvumilivu wako.
Imetolewa na:
Uongozi
Vodacom Tanzania PLC
Huduma za mpesa kwa walio nje ya nchi bado hazifanyi kazi. Mnarejesha lini?
 
Back
Top Bottom