Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Kupanga ni kuchagua mkuu, kuweka mil 10 mpesa haimaanishi jamaa hayuko serious na uchumi wake. Yamkini ana akaunti nyingine mbalimbali na hiyo 10M kwake ni 'petty amount of money' kwa ajili ya matumizi madogomadogo ya dharura.

Sasa aende TCRA kwa minajili ipi? Yeye anatakiwa apambane na Vodacom Tanzania. Ukimwambia aende TCRA hiyo ni sawa na kupata changamoto kwenye akaunti yako ya NMB halafu uende ukalalamike BOT! Ni kweli kwamba BOT ni 'guarantor' wa NMB, kama ilivyo TCRA kwa Vodacom, lakini 'guarantor' ana mipaka yake kimamlaka, hawezi kufanya kila kitu. Yeye asumbuane na Vodacom, kama Vodacom wanasema TCRA ndiyo wenye shida basi haohao Vodacom ndiyo wawasiliane na TCRA and not the other way round.

Ushauri wangu; njoo kwetu Wanasheria tukuandikie NOTISI/BARUA YA MADAI NA KUSUDIO LA KUSHTAKI (DEMAND NOTICE AND AN INTENTION TO SUE), tuwape siku 3 wawe wamekulipa fedha zako za kwenye mpesa sambamba na kukulipa fidia ya usumbufu, vinginevyo tutawapeleka Mahakamani.

Yani hapo kuna hela mkuu, tena wakishaipata tu hiyo barua kutoka kwa Mwanasheria (Wakili) utambembelezwa wewe mpake ushangae! Naziona dalili za kuipoteza hiyo fedha ukiishia kulialia tu huku mitandaoni for what is rightful yours. Nchi ngumu sana hii [emoji1]..

Pambana mkuu. Ohooo!
Ndio voda ni kampuni kubwa inapaswa huduma zake ziwe za uhakika na hao vodacom wanajua kabisa watz wengi hawajui haki zao na hawajui sheria ndo maana wanafanya ayo mambo ya ajabu kila kukicha wanajua they can get away with it hawawez fanya ayo mambo kwa majiran kenya maana kenya wapo vizuri kwenye kujua haki zao siku nyingi iyo kampuni ingeshakuwa mahakamani na fidia wangelipa watu wanatafuta izo opportunity wapige mkwanja wangelipa zaidi ya iyo mil 10
 
Hao ni wezi hakuna sababu ya msingi hapo ila unawezaje kuweka kiasi hicho cha fedha kwenye line ya simu? Bank zipo na gharama zake nafuu na hutaifata pesa yako kama hivyo unavyofanya kwa hao wahuni..wangekua wanajali ilibidi wao ndio wawe wanakutafuta sio wewe ndio uwatafute kwa kosa lao..
 
Tunasema mengi ila mhusika hajakili au kukataa kujihusisha na zile issue za tuma kwa namba hii.

Nakumbuka TCRA waliweka namba ulipoti kwao issue za aina hiyo,

Sasa kama mhusika amepata hela ha tuma kwa namba hii au kasema anauza kitu fulani online kafamyiwa malipo kamblock mhusika na mhusika akareport TCRA Lazima kiumane.

Tuwaze na upande huo pia.

Ila kama anajua ni clean hela zake basi achukje hatua za kisheria
 
Mleta mada kuwa muwazi upate usaidizi. Vodacom au TCRA hawawezi kuamka asubuhi wakakufungia line bila sababu ya msingi. Ni either kuna hela imeingia toka number ambayo inafanya utapeli kuja kwako(Na sio mara moja) au namba yako imeripotiwa kufanya utapeli.
Njia mojawapo ya kumkamata tapeli ambaye ulikuwa unawasiliana naye kwa simu hata kama ameizima ni kwenda polisi, au TCRA ambako wataangalia number hiyo inawasiliana na nani mara nyingi, na mtu huyo anadakwa aseme mwenye namba hii ni nani.
Kwa kesi yako, wanajua wakiifungia line yako(assumption) kwa vile ina hela ni lazima utajipeleka tu, na nikuhakikishie tu kama unahusika na zile issue za tuma kwenye number hii, utaenda kudakwa mchana kweupe.
 
Ni kweli! Yeye aende TCRA akajur sababu hawawezi kumuibia hela zake.

Na alete mrejesho hapa akitoka TCRA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
kama laini inakuwa na balance ya buku mbili halafu ghafla ipate balance ya 10m lazima washtuke...subiri wakisha jihakikishia ni ya kwako na sio wakala amekosea kuweka hela yake, wataweza kuiachia
 
Utawekaje pesa nyingi kiasi hiko M-Pesa?? Binafsi mm siamini sana kuweka pesa zaidi ya M1 ktk line hizi za simu. Binafsi nana Bank tu ndio sehemu salama za kuweka pesa nyingi, huku kwengine ni kujitafutia matatizo tu!! Katka hii mitandao tunaweka pesa za kufanya miamala midogo midogo kama kununua vocha, kununua bidhaa mtandaoni n.k. Anza kuweka pesa Bank
Tatzo bank makato mengi sana. Ukiweka milion moja leo,, baada ya miezi sita unaweza kuta imebaki laki7.
 
Hao ni wezi hakuna sababu ya msingi hapo ila unawezaje kuweka kiasi hicho cha fedha kwenye line ya simu? Bank zipo na gharama zake nafuu na hutaifata pesa yako kama hivyo unavyofanya kwa hao wahuni..wangekua wanajali ilibidi wao ndio wawe wanakutafuta sio wewe ndio uwatafute kwa kosa lao..
Sio kila mtu anaishi maeneo yenye bank/ mawakala wa bank. Kwa hyo mtu analazimika kuweka hela kwny simu kwa sababu mawakala wa simu ni wengi. Mfano mtu analima mpunga huko mwanza kijiji cha nsumbugu ,,anataka kuwalipa vibarua je achome mafuta mpaka misungwi kufata hela bank??

Utamwambia atumie simbanking,,,, hv unayajua makato ya simbanking 🙃????
 
Nipo kwenye pilika za porini na mjini kutunza hela Bank ni salama sana kuliko sehemu ingine gharama ya sim banking imepungua sasa hivi Mkuu...
 
Back
Top Bottom