Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Mi pesa zangu sikuiz natunza kupitia lipa namba ya TIGO.

Kuweka pesa Bank ni risky mno.. nimewah zinguana sana na CRDB kipindi flani ilikua kila nikideposit hela baada ya muda nikicheki balance nakuta over 200k imekuwa deducted. Sitaki tena kuskia habari za Bank
Vitasa kila mahali
 
Wakuu kwema?

Line yangu ya Vodacom inasoma mtandao vizuri lakini haifai kupiga namba yoyote, iwe ya kawaida au Mpesa au kununua vifurushi

Nilipoenda kwenye Vodashop nikidhani kuwa nilifungiwa sababu sikuhakiki namba vizuri

Lakini Vodashop walipoicheki wakasema niliihakiki vizuri na imetokea error tu yaani imefungwa kwa bahati mbaya na nisubiri kwa saa 24 itakuwa imefunguliwa, hiyo ilikuwa ni wiki iliyopita

Saa 24 zilipopita bado ikawa imefungiwa, nikaenda Vodacom makao makuu kuwaelezea

Makao makuu wakaniambia mbona line yako inaonekana imeshafunguliwa? Nikawaonyesha kwa kupiga simu pale kuwa haifai kupiga

Ndipo wakaniambia watashughulikia ndani ya saa 24 itakuwa tayari

Nikasubiri saa 24 zikapita bado ikawa haifai, nikawapigia huduma kwa wateja kupitia namba nyingine, huduma kwa wateja wakasema namba inaonyesha imeshafunguliwa nikate simu niijaribu tena, tukabishana pale maana nilijua haitaweza kupiga

Nikarudi tena makao makuu, wakaniambia wameishughulikia na ndani ya masaa 3 itakuwa tayari, masaa 3 yakipita ikawa haifai kupiga vilevile

Kesho yake nikarudi tena makao makuu nikawaeleza kuwa line haikufaa kupiga na sasa ninachotaka ni kupata hela zangu kwenye M Pesa hata kwa njia nyingine maana sina imani na mifumo yao tena (kumbuka siwezi kuingia M Pesa wala kufanya chochote)

Makao Makuu wakasema haiwezekani kupata hizo hela kwa njia nyingine, ni kupitia menu ya M Pesa tu,
Ila wakaniambia waliofunga line sio wao ni TCRA ila wanaipigania sana na kesho yake (leo) itakuwa tayari, jamaa akanipa na namba yake binafsi nimpigie kama haiatakuwa tayari

Sasa leo line haijawa tayari, na jamaa hapokei Simu

Wakuu hapa nafanyaje, maana hela zimekwama na sina uhakika kama nitazipata lini au ndio zitapotea moja kwa moja

CC Vodacom Tanzania
Voda wameishapita na hiyo 10m..tafuta pesa nyingine
 
Sheria za Benki Kuu ya Tanzania haziruhusu mtu kuwa na million 10 kwa wakati mmoja kwa siku kwenye line ya simu; maximum amount ni million 5 kwa siku. Wewe uliwezaje kuweka million 10 kwa wakati mmoja kwenye line ya simu, na wakati huo huo ukashindwa tena kuwa mwangalifu na laini yako hadi ikafungiwa ikiwa na kiasi kikubwa hicho cha fedha?
Ndiyo maana mimi kati ya kazi ambazo nilitamani sana kufanya nchi hii, ni u-Polisi, ila basi tu sikubahatika
Kufanya miamala kwa line ya kawaida ndio 5 million, ila ukiiongezea uwezo unaweka hadi 100 million kutoa hadi 50 million kwa siku
 
Bora ufanye kwenda huko TCRA ili upate ushahidi na vigezo vya kuwaburuza mahakamani wote Voda na TCRA, tafuta wakili mzuri umfahamishe hiyo kadhia yako.

Huoni wamekupa shida juu ya pesa yako mwenyewe??.
Una uhakika kama hizo ni pesa zake mwenyewe?

Yeye aende TCRA halafu atakuja kutupa mrejesho

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nilisha liwa laki6 zamani na mimi nikaviziaaawee nikapita na laki2.3 nikaing'atang'ata nikapita hivi[emoji124][emoji124][emoji125][emoji125] pesa kwenye simu zinapita tu sio kutunza
 
Benki bado inabaki kuwa sehemu salama na rahisi kuweka na kutoa fedha
Endelea kuwasisitiza bila kuchoka
Haha umesahau kwenye makabati
download.jpg
 
Utawekaje pesa nyingi kiasi hiko M-Pesa?? Binafsi mm siamini sana kuweka pesa zaidi ya M1 ktk line hizi za simu. Binafsi nana Bank tu ndio sehemu salama za kuweka pesa nyingi, huku kwengine ni kujitafutia matatizo tu!! Katka hii mitandao tunaweka pesa za kufanya miamala midogo midogo kama kununua vocha, kununua bidhaa mtandaoni n.k. Anza kuweka pesa Bank
 
Vodacom ni wajinga kweli ni haki yako Wairekebishe iyo laini na pesa zako pia ziwepo vodacom ni kampuni kubwa inatkiwa ni sehemu safe kama mteja kuweka fedha zako ingekuwa upo huku nje faster tu una wa sue sa hii tz imejaa ujinga mwingi, ww wasikilize wanachokuambia fatilia wakiwa wanakuzingua nenda mbele ya sheria, nilisahau tu ktoa hela na nimesahua password ni laki moja kwenye Mpesa now ni 4years sijarudi bongo nikirudi tu wakinizingua watanitambua 😂😂 sheria na taratibu lazima zifatwe, nilivyo ningewaanika uko mitandaoni hao voda mbona wangeitapika iyo hela 😂
 
Duh! 10ml unahifadhi m-pesa! Haupo serious na uchumi wako. Anyway nenda TCRA.
Ikishindikana nenda kwa waziri wa habari na mawasiliano.
Kupanga ni kuchagua mkuu, kuweka mil 10 mpesa haimaanishi jamaa hayuko serious na uchumi wake. Yamkini ana akaunti nyingine mbalimbali na hiyo 10M kwake ni 'petty amount of money' kwa ajili ya matumizi madogomadogo ya dharura.

Sasa aende TCRA kwa minajili ipi? Yeye anatakiwa apambane na Vodacom Tanzania. Ukimwambia aende TCRA hiyo ni sawa na kupata changamoto kwenye akaunti yako ya NMB halafu uende ukalalamike BOT! Ni kweli kwamba BOT ni 'guarantor' wa NMB, kama ilivyo TCRA kwa Vodacom, lakini 'guarantor' ana mipaka yake kimamlaka, hawezi kufanya kila kitu. Yeye asumbuane na Vodacom, kama Vodacom wanasema TCRA ndiyo wenye shida basi haohao Vodacom ndiyo wawasiliane na TCRA and not the other way round.

Ushauri wangu; njoo kwetu Wanasheria tukuandikie NOTISI/BARUA YA MADAI NA KUSUDIO LA KUSHTAKI (DEMAND NOTICE AND AN INTENTION TO SUE), tuwape siku 3 wawe wamekulipa fedha zako za kwenye mpesa sambamba na kukulipa fidia ya usumbufu, vinginevyo tutawapeleka Mahakamani.

Yani hapo kuna hela mkuu, tena wakishaipata tu hiyo barua kutoka kwa Mwanasheria (Wakili) utambembelezwa wewe mpake ushangae! Naziona dalili za kuipoteza hiyo fedha ukiishia kulialia tu huku mitandaoni for what is rightful yours. Nchi ngumu sana hii [emoji1]..

Pambana mkuu. Ohooo!
 
Ulitamani kazi ya laana Sana Bora hujapata tu
Duniani kote, haipo kazi yenye sifa ulizozitaja wewe hapa. Kazi ambazo zinaongoza kwa kuonekana kuwa zina baraka, ni za watumishi wa Mungu pamoja na zile za dharula, zinazohusiana na uhai wa mwanadamu moja kwa moja, mojawapo zikiwa ni za udaktari na za usalama, uPolisi ikiwa ni mojawapo ya kazi hizo.

Ni kwa sababu watu wote wanaofanya kazi hizi wanaonekana kuwa ni immediate surbodinates wa Mungu moja kwa moja kwa sababu Mungu ndiyo chanzo cha uhai!
 
Mimi nilishaacha mambo ya kutumia simu kuweka hela. Hela iliyopo kwenye mpesa ni kwa ajili ya vocha tu. In the order of 10000's tu
 
Duniani kote, haipo kazi yenye sifa ulizozitaja wewe hapa. Kazi ambazo zinaongoza kwa kuonekana kuwa zina baraka, ni za watumishi wa Mungu pamoja na zile za dharula, zinazohusiana na uhai wa mwanadamu moja kwa moja, mojawapo zikiwa ni za udaktari na za usalama, uPolisi ikiwa ni mojawapo ya kazi hizo.

Ni kwa sababu watu wote wanaofanya kazi hizi wanaonekana kuwa ni immediate surbodinates wa Mungu moja kwa moja kwa sababu Mungu ndiyo chanzo cha uhai!
Kutamani kuwa polisi Ni kukosa hekima...
 
Back
Top Bottom