Vodacom wamefungia line yangu ikiwa na milioni 10 kwenye M-PESA

Wakuu kwema?

Line yangu ya Vodacom inasoma mtandao vizuri lakini haifai kupiga namba yoyote, iwe ya kawaida au Mpesa au kununua vifurushi

Nilipoenda kwenye Vodashop nikidhani kuwa nilifungiwa sababu sikuhakiki namba vizuri

Lakini Vodashop walipoicheki wakasema niliihakiki vizuri na imetokea error tu yaani imefungwa kwa bahati mbaya na nisubiri kwa saa 24 itakuwa imefunguliwa, hiyo ilikuwa ni wiki iliyopita

Saa 24 zilipopita bado ikawa imefungiwa, nikaenda Vodacom makao makuu kuwaelezea

Makao makuu wakaniambia mbona line yako inaonekana imeshafunguliwa? Nikawaonyesha kwa kupiga simu pale kuwa haifai kupiga

Ndipo wakaniambia watashughulikia ndani ya saa 24 itakuwa tayari

Nikasubiri saa 24 zikapita bado ikawa haifai, nikawapigia huduma kwa wateja kupitia namba nyingine, huduma kwa wateja wakasema namba inaonyesha imeshafunguliwa nikate simu niijaribu tena, tukabishana pale maana nilijua haitaweza kupiga

Nikarudi tena makao makuu, wakaniambia wameishughulikia na ndani ya masaa 3 itakuwa tayari, masaa 3 yakipita ikawa haifai kupiga vilevile

Kesho yake nikarudi tena makao makuu nikawaeleza kuwa line haikufaa kupiga na sasa ninachotaka ni kupata hela zangu kwenye M Pesa hata kwa njia nyingine maana sina imani na mifumo yao tena (kumbuka siwezi kuingia M Pesa wala kufanya chochote)

Makao Makuu wakasema haiwezekani kupata hizo hela kwa njia nyingine, ni kupitia menu ya M Pesa tu,
Ila wakaniambia waliofunga line sio wao ni TCRA ila wanaipigania sana na kesho yake (leo) itakuwa tayari, jamaa akanipa na namba yake binafsi nimpigie kama haiatakuwa tayari

Sasa leo line haijawa tayari, na jamaa hapokei Simu

Wakuu hapa nafanyaje, maana hela zimekwama na sina uhakika kama nitazipata lini au ndio zitapotea moja kwa moja

CC Vodacom Tanzania
Mbona dili hilo washtaki hao wapuuzi
 
Haya mambo kumbe bado yapo lakini mimi kwa ufahamu wangu ukiangalia ile chati ya makato mwisho wa kuweka pesa ni mil 5
Lakini hata hivyo maelezo ya mtoa mada yamenitia hofu Sana kuweka pesa mpesa naona sio salama kabisa ni jambo la kushangaza kampuni kubwa kama voda wanaoingiza faida za mabilioni wakubali kampuni yako ipate sifa mbaya kwa kesi ya kuiba mil 10 ya mteja
 
Wakuu kwema?

Line yangu ya Vodacom inasoma mtandao vizuri lakini haifai kupiga namba yoyote, iwe ya kawaida au Mpesa au kununua vifurushi

Nilipoenda kwenye Vodashop nikidhani kuwa nilifungiwa sababu sikuhakiki namba vizuri

Lakini Vodashop walipoicheki wakasema niliihakiki vizuri na imetokea error tu yaani imefungwa kwa bahati mbaya na nisubiri kwa saa 24 itakuwa imefunguliwa, hiyo ilikuwa ni wiki iliyopita

Saa 24 zilipopita bado ikawa imefungiwa, nikaenda Vodacom makao makuu kuwaelezea

Makao makuu wakaniambia mbona line yako inaonekana imeshafunguliwa? Nikawaonyesha kwa kupiga simu pale kuwa haifai kupiga

Ndipo wakaniambia watashughulikia ndani ya saa 24 itakuwa tayari

Nikasubiri saa 24 zikapita bado ikawa haifai, nikawapigia huduma kwa wateja kupitia namba nyingine, huduma kwa wateja wakasema namba inaonyesha imeshafunguliwa nikate simu niijaribu tena, tukabishana pale maana nilijua haitaweza kupiga

Nikarudi tena makao makuu, wakaniambia wameishughulikia na ndani ya masaa 3 itakuwa tayari, masaa 3 yakipita ikawa haifai kupiga vilevile

Kesho yake nikarudi tena makao makuu nikawaeleza kuwa line haikufaa kupiga na sasa ninachotaka ni kupata hela zangu kwenye M Pesa hata kwa njia nyingine maana sina imani na mifumo yao tena (kumbuka siwezi kuingia M Pesa wala kufanya chochote)

Makao Makuu wakasema haiwezekani kupata hizo hela kwa njia nyingine, ni kupitia menu ya M Pesa tu,
Ila wakaniambia waliofunga line sio wao ni TCRA ila wanaipigania sana na kesho yake (leo) itakuwa tayari, jamaa akanipa na namba yake binafsi nimpigie kama haiatakuwa tayari

Sasa leo line haijawa tayari, na jamaa hapokei Simu

Wakuu hapa nafanyaje, maana hela zimekwama na sina uhakika kama nitazipata lini au ndio zitapotea moja kwa moja

CC Vodacom Tanzania
Hizo danadana bila kufungua kesi utapata tabu saana
 
Mzee mnachezea hela jombaa c ukae na mwanasheria uwanyookeee.
 
Mimi juzi waliifungia yangu siku 3 wakaifungua wenyewe bill kuhangaika😅😅ilikuwa na laki 6 halafu sikusajili kwa kitambulisho changu.roho iliniuma kichizi😅wakaifungua wenyewe.sijui wanashida gani Hawa jamaa
 
Washanipigaga elfu ,60 yangu kipindi hicho nipo first year ndo najifunza funza kutunza ela nikasahau namba ya Siri fatilia adi voda shop lakini wapi mpaka kesho sithubutu kuacha laki Mpesa,
 
Sasa kama ipo wanashindwa vipi kuitoa au kuihamisha kwenda namba nyingine wakati wao ndio wenye hiyo system.....huu uhuni huu unafanyiwa
Mkuu hiyo huwa inawezekana lakini inahitaji escalation kubwa sana, ingekua rahisi hivyo watu wangekua wanalia kila siku
 
Sheria za Benki Kuu ya Tanzania haziruhusu mtu kuwa na million 10 kwa wakati mmoja kwa siku kwenye line ya simu; maximum amount ni million 5 kwa siku. Wewe uliwezaje kuweka million 10 kwa wakati mmoja kwenye line ya simu, na wakati huo huo ukashindwa tena kuwa mwangalifu na laini yako hadi ikafungiwa ikiwa na kiasi kikubwa hicho cha fedha?
Ndiyo maana mimi kati ya kazi ambazo nilitamani sana kufanya nchi hii, ni u-Polisi, ila basi tu sikubahatika
Kaka, hiyo ya mil5 ilifutwa baada ya kuibuka COVID sasahivi ni 10m
 
Kuweka hela nyingi kwenye cmu ni risk sana,mm nishapoteza 600k kwenye Airtel money kipindi kile wanaofa ya hakatwi mtu.nilienda Sana makao makuu yao ila ckupata msaada wowote kila cku ilikuwa sound tu nikaona napoteza muda
 
Mimi juzi waliifungia yangu siku 3 wakaifungua wenyewe bill kuhangaika😅😅ilikuwa na laki 6 halafu sikusajili kwa kitambulisho changu.roho iliniuma kichizi😅wakaifungua wenyewe.sijui wanashida gani Hawa jamaa
Na hujatoa hela hadi leo??? watanzania bhana
 
Back
Top Bottom