Vodacom wanaingilia mpesa ya mteja na kutoa pesa zote kulipia nipige tafu bila hiari ya mtu

Vodacom wanaingilia mpesa ya mteja na kutoa pesa zote kulipia nipige tafu bila hiari ya mtu

Na ukiweka laki nne wanafanya hivyo hivyo?
 
Mkuu hujanielewa.
Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida
Wanakuwekea ilu utumie unavyotaka wewe, badala ya kununua kifirushi Cha elfu tano Sasa nunua Cha 4500. Wako sahihi maana utalipa utakapoongeza salio.
Zamani kabla hawajaboresha watu Kama wewe miikopa hamlipi mnaanza kujiunga juu kwa juu Sasa hamlipi madeni Hadi mmpende wenyewe.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Nilichoelewa wewe ndiyo umetoa hela kununua kifurushi, kwa kulipia kwa Mpesa, wao wamekata deni lao, na kiasi kilichobakia kinaendelea kuwa muda wa maongezi.
Hawajakwapua kutoka Mpesa.

Dawa ya deni kulipa, pole!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kuna mtandao mmoja mimi sijakopa hiyo nipige tafu sijui waliniwekea kwa njiagani.

Huwa najiunga kifurushi cha mwezi, naweka elfu kumi , natakakujiunga naambiwa eti saliohalitoshi kuwapigia wananiambia eti nilikopa, daaah, nilifoka sana kidogo niwatukane matusi ya nguoni nikajizuiya.

Yani sikuwahikukopa nilishangaa sana, mbaka leo sielewi.

Napanga niende oficinikwao waniambie tatizo nini mana nilikasirika sana kituambacho sijafanya alafu wananiambia nilikopa daah.

alafu pesa wakaielekeza kwenye muda wa maongezi pia.
Hovyo sana.
 
Unaambiwa ulijiunga na huduma ya ringtones
Niliwapigia niliwakaa.. kama moto. Wasnge kila nikiweka salio baada mda nakuta 0.00 nawapigia wananipa procedure, nikiweka tena salio baada ya mda nakuta 0.00.. kuna siku nikachachamaaa vibayaa kama mwehu, tokea siku hiyo hawajarusi huo useng wao hadi leo. Naweka salio linakaa tu,
 
Niliwapigia niliwakaa.. kama moto. Wasnge kila nikiweka salio baada mda nakuta 0.00 nawapigia wananipa procedure, nikiweka tena salio baada ya mda nakuta 0.00.. kuna siku nikachachamaaa vibayaa kama mwehu, tokea siku hiyo hawajarusi huo useng wao hadi leo. Naweka salio linakaa tu,
Hao mbwa wamenichosha na ule u-enge wao wa Tuzo point. Nikitaka kuziingiza Mpesa inakuwa shughuli. Inaonekana 300 wakati pointi ni 5000+
 
Hao mbwa wamenichosha na ule usenge wao wa Tuzo point. Nikitaka kuziingiza Mpesa inakuwa shughuli. Inaonekana 300 wakati pointi ni 5000+
Wana ka utapeki flani hivi ka Technolojia. Jana bimepiga menu ile ya DAR UNI nimekuta kifurushi GB 2, kwa siku 7. Buku tano nikaunga, ila narudi badae nakutana na menu ingine buku tano GB 1.22 😀😀😀😀... Nikasema hawa ni wezi sanaaa.. Tuzo Point kwangu huwa zinabadilika vizuri tu.. huenda wana kisa na wewe 😀😀
 
Lipa deni masharti yao yako wazi. Voda nawapenda na ndio mtandao ninaouamini wana huduma za uhakika sana
 
Ni sawa unaenda dukani kwa mangi. Kwa kuwa ulikopa sukar ya mia5 jana, leo unaenda kwake na elf5 kupata bidhaa ya elf 2 , anakata deni, bidhaa husika anakupa na chenji harudishi anakujazia bidhaa usiyoitaka.
Umeelezea vizuri Sana hata mtoto Mdogo atakuelewa
 
Lipa deni mzee, hii tabia ya kihuni mtaacha lini watanzania? Obligation yako huijui endapo unaingia mkataba wa kukopa? Mi naona hao jamaa hawana tatizo ila wewe ndio mwenye shida mahali flani!

Vodacom, hapo poooa!!!
Exactly, haiwezekani ukope wakati Mpesa ina noti za kutosha.
 
Wachangiaji wengi wa hii mada hawajaelewa kilichoandikwa. Tuwe tunasoma na kuelewa ndg zangu.
 
Mkuu hujanielewa.
Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida
mh! si wanaweza kutuibia hwa jamaa..
 
Voda wanaingilia mpesa ya mteja na kutoa pesa zote kulipia nipige tafu bila hiari ya mtu

Niwape indhari kuna mtindo voda wamekuja nao, kama unadaiwa nipige tafu mfano 500 ukitaka kununua kifurushi kupitia mpesa mfano kifurushi cha 5000 wanachokifanya ukilipia kwa mpesa wanachukua elfu 5 ulolipia kifurushi kwa mpesa hawakupi kifurushi bali wanaielekeza hiyo 5000 kuja kwenye salio la kawaida wanakata 500 yao halafu hiyo 4500 iliyobaki wanaibakisha kwenye salio la kawaida haya wanafanya bila hiari ya mteja huu ni wizi

Kwanini wasikate pesa wanayodai tu badala yake wanaingia kwenye mpesa na kukomba kiasi chote ulichotarajia kununua kwenye mpesa kisha wanaweka kwenye salio la kawaida bila khiari ya mteja? Huu utaratibu wa kibazazi voda mmeutowa wapi?hii ni too much kwa kweli


Tatizo sio kukata pesa yao, tatizo wanakata pesa yao halafu hizo nyengine wanazichukua wanakuwekea kwenye salio la kawaida hili ndo tatizo, dawa ya deni ni kulipa na ndivyo ilivyo wakate pesa yao lakini sio wakishakata wanachukua na pesa yote ilobaki kwenye mpesa na kuiweka katika salio la kawaida...
[emoji3][emoji3]
 
Tabia mbovu saaana hii wanafanya..!

Wanapaswa kukata deni lao halafu inayobaki waiache MPESA, kitendo cha kuileta kwenye muda wa maongezi sio sahihi
 
Kwani watu bado hawajanielewa
 
Back
Top Bottom