Bramo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 13,176
- 10,068
Mambo ya Imani banaWanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huwaletea makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Mada ya leo ni a bit abstract, ambapo Nimesikia sauti ya Voices From Within ikiniambia JPM yuko Mbinguni kwa Baba, hivyo nauliza swali, jee wajua kuwa JPM yuko peponi, Mbinguni, Kwa BABA YAKE?. Why watu wengine waendelee kumshutumu, kumsakama na kumsimanga?. Kwa nini asiachwe ajipumzikie zake kwa amani!. Mtu ameisha tangulia mbele ya haki, kwanini watu waendelee kumsema sema kwa ubaya.
Mimi mwana jf mwenzenu ni Mzee wa Sauti za Ndani "the inner voice", unafanya kitu fulani na mara unasikia sauti from within ikikuambia jambo fulani.
Angalizo kuhusu Abstract Topics.
Issues na mtu akiisha kufa, we all knows what happens to the body, but roho huwa inakwenda wapi, no one knows for sure, hivyo tunategemea mafundisho ya dini zetu.
Kuna sisi dini za wana wa Nabii Ibrahim, Wakristo na Waislamu tumefunzwa kuhusu mbinguni, peponi, ahera, jehanam ya moto wa milele, na kuna siku ya mwisho siku ya hukumu ya mwisho ya kiama atakapo rudi Mwana wa Adamu, ambapo kutakuwa na ufufuko wa miili na uzima wa milele.
Kuna wenzetu wa Buddhism na Hindu ambao ni waumini wa karma, wao wanaamini kwenye after life na incarnation.
Hakuna yeyote awaye yote aliwahi kufa akayashudia hayo na kurejea duniani kututhibitishia mbingu ipo, peponi kupo na motoni kupo, wala waumini wa reincarnation no one can say for sure alikuwa nani before, zaidi ya ushahidi wa deja vu, hakuna uthibitisho wowote wa reincarnation Ila kwa vile na mimi niliishi India, I know for sure karma ipo and it's for real!.
Hivyo hii mada ni mada ya imani, kama wewe huamini, please keep your faith nakuomba usibeze imani za wengine, ukijiona huamini, nakuomba jipitie zako kimya kimya, tuache sisi waumini.
Leo asubuhi nilikuwa nasoma michango ya wachangiaji wa bandiko langu hili,
Kuna mtu akachangia kitu, katika kumjibu nikatumia link hii
Sasa ni wakati nasoma bandiko lenyewe, na naomba nililete hapa bandiko lenyewe lote kwa faida ya wavivu to follow links.
Ndipo nikaisikia sauti, voices from within kuwa JPM yuko peponi, ahera, mbinguni kwa Baba!.
Kwa kawaida ya sauti, huwa inakuambia tuu kitu na haikupi sababu, hivyo naomba msiniulize sababu, hapa kazi yangu ni moja tuu kuwaeleza kile nilichosikia Leo ni JPM yuko peponi!.
Hivyo baada ya kuisikia hiyo sauti nikamsikiliza tena JPM kwa makini sana katika video hii
Nimejirisha bila chembe ya shaka, huyu mtu yuko mbinguni kwa Baba yake!.
Hapa simaanishi kuwa JPM yuko peponi kwasababu he is perfect kama malaika, no!. JPM was a human being hivyo he is not perfect and no one is perfect, kilichofanya hiyo sauti ni despite his human mistakes JPM alitubu kabla ya umauti na kusamehewa makosa yake yote, na ndio maana nimeambiwa, sasa he is in heaven now!.
Kwa bandiko hili, sasa ningewaomba watu humu, kutoendelea kumsakama, kumshutumu, kumsimanga na kuendelea kumsema vibaya, na badala yake tumwache apumzike kwa amani. Kama Mungu mwenyewe amemsamehe na kumuita kwake, who are you kuendelea kumsema sema vibaya?.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali.
Yaani unawezakuta Jiwe yuko Peponi halafu Ben Saanane yuko Motoni
Ila Kwa ushetani alioufanya Jiwe, Chances za kuwa Motoni Kwa Sasa ni Kubwa sana