Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

Mambo ya Imani bana

Yaani unawezakuta Jiwe yuko Peponi halafu Ben Saanane yuko Motoni

Ila Kwa ushetani alioufanya Jiwe, Chances za kuwa Motoni Kwa Sasa ni Kubwa sana
 
Watu wenye roho za kishetani tu ndio hawajui maana ya msamaha.

Halafu wenyewe wanafikiri kusamehe ni faida ya yule unayemsamehe, kumbe wewe unayesamehe ndiyo unanufaika. Maana inasemwa ukiishi na chuki na kinyongo moyoni, unakuwa huna tofauti na mtu ambaye anaishi na magonjwa ya kudumu yasiyo ambukiza kama magonjwa ya moyo, kisukari, nk. Ugonjwa wa kinyongo una tabia kama za magonjwa hayo. Maana kuna kipindi unapanda na kuwa na uchungu mkali, hasa ukimuona au kukumbuka.
 
Mkuu

Naona Unaamini kabisa ule Upuuzi kuwa Jiwe Kwa Sasa kaukwaa Ukiranja wa Malaika
Unaanza Kujipendekeza kwake Ili ukienda.huko akuteue
 
Mkuu Mshana Jr humu jf kuna baadhi ya members ni authority, wewe ni mmoja wao, hivyo mimi siwezi kubishana na authority yako ila na mimi ni mtu enlightened hivyo nimeona mwanga na ninawajibu wa kuwaangazia na wengine.

Mtu akifa kabla hajazikwa ndio roho yake inatangatanga, akiisha ziko ni roho inakwenda straight hukumuni, na tunahukumiwa kwa mzani wa mema na mabaya, mema yakizidi mabaya unaingia peponi hata kama duniani ulikuwa muuaji!.

Unaanza kutumikia adhabu pale pale na sio kusubiria siku ya hukumu ya mwisho. Siku ya mwisho ya kiama na ufufuko wa miili, miili inayofufuliwa ni ile mili ya roho, na sio miili ya nyama, ukiisha kufa ule mwili wa nyama ukiisharudi mavumbini, ni mavumbi na shughuli yake imeishia hapo!.

Hivyo usidhani mtu akifa leo anasubiri hukumu ya mwisho!. No!. Ukifa leo unaingia kwa pilato leo Leo.
You are not right on this, ukifa unahukumiwa na adhabu unaanza kuitumikia pale pale, hakuna kusubiria.
Kwa upande wa karma.. Hii sote tunajua haikopeshi.. Tendo kwa tendo ..ubaya kwa ubaya na wema kwa wema.. Hivyo inategemea nani anaamini kwenye nini ndio atamuweka mhusika huko..
Hapa niko na wewe.
Kuna hili la mizania ya haki.. Hili hupimwa kwa matendo ya mtu mabaya na mazuri..Asili ndio huhukumu., hapa si dini bali ni asili, asili itakuchagulia njia yako kutokana na maisha uliyoishi kabla ya kifo
Naounga mkono hoja na hukumu hii ndio hukumu ya karma, kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake. Ukitenda ubaya, ukajuta, ukatubu, ukaomba msamaha, ukatenda mema, unakwenda mbinguni.
Sauti ile niliyosikia, inamaanisha mzani wa JPM, ametenda mema mengi kuliko mabaya, hivyo ameingia mbinguni straight!.
P
 
Kaa kimya pengine wewe sio Mtanzania kwamba yaliyotokea hujui, Vyeti feki na huo ujinga unasema usifiki kila mtu anategemea vyeti tuu maisha yaende..
 
Mkuu waliofanyiwa hivyo nawajua kama wanne hivi na walikuwa smart tuu, mmoja alipata stroke jumla mpaka leo alafu hii misukule yake iliyobaki inatetea sijui ujinga gani..
 
 
Yaani hatamimi alichoma nyavu zangu bila kosa tatizo watu wake niliwanyima pesa nahata Hutu mama atuangalie wavuvi kata yakalya tulionewa sana hadi Leo wanashikilia Mali zetu eti dhuluma nayo nichanzo cha mapato bora hivyo alivyo kufa
 
Mkuu, kuna mambo unachanganya , tuyaweke sawa

1. Kumshambulia JPM kama mwanadamu mwingine akiwa amefariki na hawezi kujitetea si sawa.

2. JPM alikuwa Kiongozi wa nchi, alitunga sera, kutoa maamuzi yaliyoathiri maisha yetu kwa kupenda au kutopenda

Mfano, aligomea chanjo kwa imani zake na kuwanyima fursa wengine, wakipoteza maisha kwa manung'uniko.

Kwa kuwa kiongozi, JPM aliishi kwa KODI zetu , alipewa kila fursa kuliko Mtanzania mwingine.

Kuna msemo 'with great power comes great responsibility ', hapo huwezi kutenganisha maisha yake na ya uongozi.

Ni kwa mantiki hiyo, wakosoaji wanazikosoa sera, mitazamo, madhaifu na maamuzi yake kama kiongozi wa nchi.
Hilo si kumkosoa binafsi ni kumkosoa kama kiongozi aliyebeba fursa na dhamana.

Ni kumkosoa kama kule kwa Nyerere tunaoufanya kwa miaka 23 au ule wa Mkapa. Wote ni Hayati.

Tofauti na Watangulizi wake rekodi ya JPM imegubikwa na mengi yanayokihiri na jitihada za kuyafunika ni hizi za marehemu hasemwi! mbona huko nyuma tumewaseama akina Nyerere, Mkapa n.k.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…