Volkswagen yafikiria kufunga viwanda vyake nchini Ujerumani, moja ya sababu ni ushindani kutoka China

Ninachopendea Mchina hakufukuzi

Wewe mwenyewe ukiona moto umekuwa mkali unafunga unasepa.

Umenikumbusha Samsung nao walifunga plant China baada ya kuona ushindani mkali kutoka Xiaomi, Vivo, Huawei, Oppo
Sijajua sana kuhusu future ya iPhone nchini China ripoti ya karibuni inaonyesha imepigwa gap na kampuni za ndani

Kutoka kuwa ya kwanza kwenye soko la China mwaka jana mpaka kufikia kuwa ya 4 mwaka huu

Vivo, Huawei, Honor, iPhone, Xiaomi, Oppo
 
Maneno soko huria siku hizi kwa Marekani na Ulaya siyo ya kweli hawaishi kwenye hayo maneno
Walilazimisha nchi zetu zinazoendelea kuingia katika soko huria wakijua kwamba hakuna wa wakuwazidi katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Nakumbuka kwenye hotuba yake moja nyerere alifananisha na boxing kwa mtu ambaye hana utaalam akapambane na Mike iron
 
Urusi wanatengeneza magari gani
 
Walikuwa na nguvu ya kuhubiri kuhusu soko huria wakati hawana ushindani

Imagine Marekani chini ya utawala wa Biden imeiwekea China tariffs kwenye EVs kufikia 100%

Hii ni kuonyesha wameshindwa ku-compete na China
 
Nilijua hili lingetokea tu muda si mrefu. Biashara ya viwanda vya Ujerumani iliweza kushindana sokoni kutokana na kupata nishati ya bei ya kishkaji kutoka Urusi, sasa leo kaingia kiboya kwenye vikwazo dhidi ya Urusi na Mchina anazalisha magari bora kwa gharama nafuu lazima Ujerumani alambe sakafu.
 
Point haikuwa kulenga viwanda vya magari tu bali uchumi kwa ujumla. Ilitakiwa kwa sasa tuone -ve impacts za vikwazo ilivyowekewa Russia

Ila cha kusahangaza licha ya vikwazo ni kwamba uchumi wa Russia unakua kuliko mataifa yote ya Ulaya
Russia inauza gas na wateja wake ni nchi za Ulaya.
Halafu vikwazo huwa haviathiri uchumi labda nchi iwekewe vikwazo na dunia nzima
Angalia nchi kama Iran, Noth Korea
 
Umesema vyema, na hili limeumiza sekta ya viwanda vya Ujerumani kwa ujumla
 
Kila chenye Mwanzo 😁😁
 
Sijajua sana kuhusu future ya iPhone nchini China ripoti ya karibuni inaonyesha imepigwa gap na kampuni za ndani

Kutoka kuwa ya kwanza kwenye soko la China mwaka jana mpaka kufikia kuwa ya 4 mwaka huu

Vivo, Huawei, Honor, iPhone, Xiaomi, Oppo
Nadhani hata ile issue ya kuzuia watumishi kutumia iphone katika ofisi za umma inaweza kuwa mojawapo ya sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…