Kila kitu kinatengenezwa. Mexico iko pua na mdomo na Marekani, India ni hasimu wa China kiulinzi na kidiplomasia. Ukiinua India ambayo ina workforce na mishahara midogo zaidi kuliko China unapunguza kuihitaji China.
Population ya India ni kubwa zaidi ya China, elimu ipo hukosi watu ukifungua hata viwanda vya aeronautics. Soko lipo. Unabaki na vitu kama kuongeza umeme wa kutosha, bandari, reli vitu ambavyo investors wanaweza ingia miaka michache tu vikawepo.
Wateja wakubwa wa China hawa hapa. Ukiachana na Urusi, nani rafiki wa China kidiplomasia hapa? ASEAN wenyewe ndio hao kuna Philippines na Vietnam wanagombea bahari na China. Wengine kina Singapore wana mikopo kibao na investments kubwa za EU na Marekani
View attachment 3088151
Marekani ndio mwekezaji mkubwa kwa China, na ndio mteja mkubwa, na ndio mtoaji mkubwa wa teknojia kwa China. Ni kitendo cha kuhamisha influence wakiona mlinganyo sio kwa maslahi yao. Yaani unacheza na Marekani aliyeipiga Ujerumani ikachakaa kisha akaisimamisha iko top 5 kiuchumi? Akaipiga Japan ikachakaa kisha akairudisha top 5 kiuchumi duniani? Akaikuta South Korea haina hata bajeti ya kulipa mishahara wafanyakazi, akaanza kutoa hela hata za kuendeshea serikali leo hii South Korea inashindana GDP na Urusi?
Hapo ni fair game anayeona hana maslahi anatoka ila wakiamua kufungiana vioo kuna mtu ataumia zaidi.