Vuguvugu la kurudisha kadi za CCM watatumbuliwa ma-DC wangapi?

Huu mchezo unachezwa ndani. Rais wetu Dkt Samia kama kawaida yake ni mkurupukaji kama alivyokurupuka suala la DP World na bendera ya Kenya kwenye jengo la Burj Khalifa. Sasa sijui nani atamg’onga sikio kuwa hekima yake na uongozi wenye uadilifu ni muhimu zaidi ya kadi za CCM, yaani ajulishwe mizizi ya kuwa kiongozi bora siyo kujitengenezea mfumo nje ya mfumo yaani kujiaminisha Gabon waliyoyafanya basi nikae karibu na wajeda eti watanilinda hahahahaha. Kwa ufupi Mama hata sisi chawa wake huwa hatumuelewi ila kwa sababh ya uchawa lazima tumuunge mkono tu maana katiba inampa mamlaka ya kuua bila kushitakiwa etc
 
Nadhani ni wakati was kuwa na mabadiliko sahihi, hi nchi sio ya kifalme.
[emoji117]Kwamba utakula Kwasababu una juana na fulani au fulani.
[emoji117]Usalama wa taifa wajiangalie, Kuna viongozi Wana tumia magari ya mabilioni, wakati Kuna vijiji havina maji ya uhakika.
[emoji117]Na ikiwapendeza walipuane tu, huko ikulu[emoji855]

Walipuane tuuu
Tumechoka[emoji706]
 
Huu mchezo unachezwa ndani. Rais wetu Dkt Samia kama kawaida yake ni mkurupukaji kama alivyokurupuka suala la DP World na bendera ya Kenya kwenye jengo la Burj Khalifa. Sasa sijui nani atamg’onga sikio kuwa hekima yake na uongozi wenye uadilifu ni muhimu zaidi ya kadi za CCM, yaani ajulishwe mizizi ya kuwa kiongozi bora siyo kujitengenezea mfumo nje ya mfumo yaani kujiaminisha Gabon waliyoyafanya basi nikae karibu na wajeda eti watanilinda hahahahaha. Kwa ufupi Mama hata sisi chawa wake huwa hatumuelewi ila kwa sababh ya uchawa lazima tumuunge mkono tu maana katiba inampa mamlaka ya kuua bila kushitakiwa etc
Nakubaliana na Wewe kabisa maana kuna wakati Sisi kama chawa tunabanwa maswali mpaka unawaza sasa na hili nilijibuje maana kisheria Haliko sawa ila tu naogopa nisikosea adabu ma kuipinga itikadi yangu....
 
Hayati mwendazake aliifahamu vema nguvu ya uma, kuchokwa kwa chama chake na kutopendwa kwa viongozi wa chama chake ndio maana aliamua kibabe sana kukataza mikutano ya kisiasa na mijadala huru ya wananchi...

NGUVU ya uma ni kitu chenye nguvu sana maana ni muunganiko wa roho nyingi zenye nishati inayowaza jambo moja kwa pamoja, tofauti kabisa na nguvu ya kiongozi anayewaza jambo moja kwa msaada wa vyombo vya ulinzi vinavyopokea ujira na kumtumikia mtawala!

Chama tawala kimechokwa na hata wanachama wake! Hili si jambo la kushangaza hasa kutokana na ukongwe wake.. Wananchi wa Mtwara wanaojulikana kwa misimamo na utata wiki iliyopita baada ya kuchoshwa na ujinga wa viongozi wao wakaamua kwenye mkutano wa hadhara kurudisha kadi za CCM kufikisha ujumbe kunakohusika.

Watawala ama kwa kukurupuka ama kwa kutafuta huruma ya jamii ama kwa kutowaza kwa weledi wakaamua kwa haraka kuwatumbua viongozi wa kisiasa waliosababisha tatizo! Haikuwa hatua mbaya walifanya vema kusimama na wananchi. Lakini kwakuwa mambo ni mengi na muda ni mchache wakadhani hilo limeisha.

Jana kwenye mkutano wa hadhara huko wilayani Lushoto moja ya ngome kongwe za CCM wananchi wa kijiji cha View Point kwenye mkutano wa hadhara nao wakarudisha kadi za ccm kuonesha kutoridhishwa kwao na viongozi wao wa kisiasa
Mbegu iliyopandwa Mtwara imechipukia Milimani lushoto mamia ya kilometa. Moto uliowashwa Mtwara umeruka hadi Lushoto mwendo wa masaa si chini ya 20 kwa mwendo wa gari.

Tafsiri yake ninini hapa? Wananchi wamechoka na uoga hatimaye umewatoka! Hawaogopi tena! Ni ngumu kutabiri kituo kifuatacho kitakuwa wapi.. Kama kikiwa kanda ya ziwa hiyo ni habari ya kutisha sana...

Swali la kujiuliza je na DC wa Lushoto naye atatumbuliwa kwa kuzembea mpaka wananchi wakarudisha kadi za chama?

Je, asipotumbuliwa itakuwaje kwa aliyetumbuliwa? Maana makosa yanafanana.

Na je hili vuguvugu la kurudisha kadi za ccm tena kwenye mikutano isiyokuwa ya wapinzani likishika kasi. Watatumbuliwa wangapi!? Au wangapi hawatatumbuliwa?

View attachment 2736303
samia watu hawakutaki.Achia kiti urudi Paje ukalee wajukuu.
 
Watu wanakuambia ukiweka ccm na andazi watu watachagua andazi kwa mana hiyo watu ata chauma akishindana na ccm kwa uchaguzi huru saa nne mzee wa ubwabwa yupo ikulu
Ndo maana hakuna mbadala wa CCM kwasababu andazi haliwezi kuongoza kwa maana yake ukiitoa CCM yaliyobaki ni maandazi
 
Hayati mwendazake aliifahamu vema nguvu ya uma, kuchokwa kwa chama chake na kutopendwa kwa viongozi wa chama chake ndio maana aliamua kibabe sana kukataza mikutano ya kisiasa na mijadala huru ya wananchi...

NGUVU ya uma ni kitu chenye nguvu sana maana ni muunganiko wa roho nyingi zenye nishati inayowaza jambo moja kwa pamoja, tofauti kabisa na nguvu ya kiongozi anayewaza jambo moja kwa msaada wa vyombo vya ulinzi vinavyopokea ujira na kumtumikia mtawala!

Chama tawala kimechokwa na hata wanachama wake! Hili si jambo la kushangaza hasa kutokana na ukongwe wake.. Wananchi wa Mtwara wanaojulikana kwa misimamo na utata wiki iliyopita baada ya kuchoshwa na ujinga wa viongozi wao wakaamua kwenye mkutano wa hadhara kurudisha kadi za CCM kufikisha ujumbe kunakohusika.

Watawala ama kwa kukurupuka ama kwa kutafuta huruma ya jamii ama kwa kutowaza kwa weledi wakaamua kwa haraka kuwatumbua viongozi wa kisiasa waliosababisha tatizo! Haikuwa hatua mbaya walifanya vema kusimama na wananchi. Lakini kwakuwa mambo ni mengi na muda ni mchache wakadhani hilo limeisha.

Jana kwenye mkutano wa hadhara huko wilayani Lushoto moja ya ngome kongwe za CCM wananchi wa kijiji cha View Point kwenye mkutano wa hadhara nao wakarudisha kadi za ccm kuonesha kutoridhishwa kwao na viongozi wao wa kisiasa
Mbegu iliyopandwa Mtwara imechipukia Milimani lushoto mamia ya kilometa. Moto uliowashwa Mtwara umeruka hadi Lushoto mwendo wa masaa si chini ya 20 kwa mwendo wa gari.

Tafsiri yake ninini hapa? Wananchi wamechoka na uoga hatimaye umewatoka! Hawaogopi tena! Ni ngumu kutabiri kituo kifuatacho kitakuwa wapi.. Kama kikiwa kanda ya ziwa hiyo ni habari ya kutisha sana...

Swali la kujiuliza je na DC wa Lushoto naye atatumbuliwa kwa kuzembea mpaka wananchi wakarudisha kadi za chama?

Je, asipotumbuliwa itakuwaje kwa aliyetumbuliwa? Maana makosa yanafanana.

Na je hili vuguvugu la kurudisha kadi za ccm tena kwenye mikutano isiyokuwa ya wapinzani likishika kasi. Watatumbuliwa wangapi!? Au wangapi hawatatumbuliwa?

View attachment 2736303
Uzuri wake ujumbe unawekwa wazi wananchi wana kero na wanamhitaji Mkuu wa wilaya hataki kwenda kuwasikiliza tatizo la nani ni lake yeye abebe lawama
 
Sijui hali ya huyu mwana ccm aliyerudisha card maisha yake yatakuwaje baadae.

Mikutano ya cdm imezidi kuwa moto na mwiba mkali sana kwa mabwenyenye ccm.

Ebu tazameni hii clip ndiyo mtaelewa kilichoktokea kwenye mkutano wa cdm pale Lushoto.
1693657000967.jpg
 
Back
Top Bottom