Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
mi kuna saa spid inafika 80 nashtukia kabisa.. sijui ka ntawahi zidisha 80
Hao itakuwa walikuwa 'matingasi'
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mi kuna saa spid inafika 80 nashtukia kabisa.. sijui ka ntawahi zidisha 80
Arusha kila mtu billionea kule shenzi typeAyo TV ni vimbelembele
Wao utasikia kila mtu bilionea
Waandishi machawa tu
Ova
Sorry to say this. Arusha ulimbukeni ni mwingi sana, I think kama magu asingeingia madarakani pangekuwa ni miliki ya watu wachache. Moja ya achievement ya magu ni kuleta law and order kwenye hiyo sehemu, na kwenye Hilo alikiwa ana-negotiate na mtutu wa bunduki, walivyoona jamaa Hana masihara wakatulia kimya na mavurugu ya kijingajinga yakapungua. Dar licha ya changamoto zake Pako fair sana kwa mtu yeyote na matajiri wengi hawana mentality za kijima kutaka ku-control watu.Wanataka zile kiki za billionea wa Arusha
Kosa amealikwa au ?Habari haijasema Kama mwandishi alikuwa ameanza coverage Bali alikuwa ndio anafika msibani, au Mimi ndio nimewaka ?
Kama Ni hivo nilivoelewa Basi Ni kosa kumnyang'anya vifaa vyake
Hahahahaha Arusha ilitaka kuwa kamaSorry to say this. Arusha ulimbukeni ni mwingi sana, I think kama magu asingeingia madarakani pangekuwa ni miliki ya watu wachache. Moja ya achievement ya magu ni kuleta law and order kwenye hiyo sehemu, na kwenye Hilo alikiwa ana-negotiate na mtutu wa bunduki, walivyoona jamaa Hana masihara wakatulia kimya na mavurugu ya kijingajinga yakapungua. Dar licha ya changamoto zake Pako fair sana kwa mtu yeyote na matajiri wengi hawana mentality za kijima kutaka ku-control watu.
Mkubwa ivyo kupigwa.
Katika hali isiyo ya kawaida vurugu zimeibuka katika msiba wa watoto wawili wa matajiri jijini Arusha ambao walikuwa ni wachumba waliofariki ajalini jana ambapo zimepelekea mwandishi wa habari kutoka AyoTV kunyang’anywa camera.
Mbali na kunyang’anywa camera mwandishi huyo alinyang’anywa kadi (memory card)na kisha kuvunjwa na ndugu wa karibu akiwemo mdogo wa marehemu,Brighton Temu maarufu kama “Bonge “.
Vurugu hizo zimefuatia mara baada ya mwandishi huyo,Gedfrey Thomas kutinga msiba
ni kwa marehemu, eneo la KwaMrefu majira ya saa 10:30 leo jioni kufuatilia tukio la kifo cha mtoto wa Tajiri Denso.
Taarifa zimeeleza kwamba mara baada ya mwandishi huyo kutinga msibani hapo akiwa ameshikilia camera yake mkononi ndipo kundi la vijana waliojitambulisha ndugu wa karibu akiwemo mtoto wa mfanyabiashara anayemiliki mgahawa wa Uzunguni City Park ,Kevin Masuwa alimvamia na kutishia kumpiga mwandishi huyo.
Taarifa kutoka msibani zimeeleza kuwa kundi hilo la vijana wanaodaiwa kuwa katika hali ya ulevi ndipo lilimuamuru mwandishi huyo akabidhi camera na baada ya kuwakabidhi walichomoa kadi na kisha kuivunja na kisha wakamrejeshea camera yake.
Hatahivyo,taarifa zimedai kuwa mara baada ya vurugu hizo ndipo baba wa marehemu tajiri....maaarufu kama “Denso “ndipo alipomfuata mwandishi huyo na kumuuliza gharama za kadi hiyo ili amlipe lakini mwandishi huyo alikataa na kudai anahitaji kadi pekee.
Akihojiwa na waandishi wa habari Mwandishi huyo kwanza alilaani tukio hilo na kudai anawatambua vijana waliomfanyia fujo na kumyang’anya vifaa vyake vya kazi.
Mwandishi huyo alisema kwamba yeye alifika msibani hapo kufuatilia tukio la ajali lililopekea mauti ya kijana huyo kama Mwandishi na ghafla alipoingia ndani ya eneo la tukio alishangaa kuvamiwa na kundi la vijana mbalimbali.
“Mimi baada ya kufika msibani niliingia moja kwa moja eneo la tukio nikiwa nasogea ndani ghafla walitokea vijana ninaowatambua kwa sura wakaniamuru niwakabidhi camera nilipotaka kukataa walitishia kunipiga ndipo nikawakabidhi wakachomoa kadi na kisha kuivunja “alisema Mwandishi huyo
Hatahivyo,alisisitiza kuwa kitendo kilichofanyika sio cha uungwana na anajiandaa kutoa taarifa mbele ya jeshi la polisi mkoani Arusha.
WATOTO wawili wa Matajiri wakubwa katika jiji la Arusha,wanaodaiwa kuwa ni wachumba , Estomi Temu na mpenzi wake Nice Mawala(24)Mkazi wa Njiro walifariki dunia jana kwa ajali mbaya eneo la kwa Mrefu katika jiji la Arusha .
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ,ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 7 usiku katika eneo hilo wakati gari la kifahari walilokuwa wakitumia lilikuwa kwenye mwendo kasi.
Katika tukio hilo linalodaiwa walitoka Klabu ,Nice alipasuka kifua na kuvunjika mkono wa kulia huku Estomi akiumia kwa ndani na kuvuja damu masikioni puani na mdomoni.
Watu mbalimbali wameendelea kufurika katika msiba huo ambao umeibua gumzo ambapo idadi kubwa ya magari ya kifahari imeibua gumzo kufuatia kupangana kuanzia nyumbani mpaka barabarani katika kituo cha KwaMrefu baada ya kukosekana eneo la maegesho.
Mwisho.
Kapuku akifia guest house au kichakani anakula demu lazima watafika nyumbani mkuuMisiba ya kitajiri media huwa zina fanya mtaji wa kuuza habari...mbona leo mtaani kwetu kafa jamaa kapuku sjawaona
Naona hao waandishi sio uchawa ni mazoea tu. Nimeishi Moshi wale watu mtu akiwa na gari kali moja na nyumba ambayo haifiki thamani ya hata 400M tiyari anaitwa billionaire bila kuzingatia assets zake na liabilities. Unaweza shangaa mtu mwenye mali za thamani ya 700M naye anaitwa billionaire. Mtu kwao wana kagari kamoja tiyari ashaitwa wa kishua mtaani.Arusha huko kila familia bilionea
Alafu hao ayo TV huko kila msiba ukitokea utasikia watoto wa mabilionea,sjui gari la kifahari [emoji1]
Ila siyo kila shughuli za watu wanataka makamera kamera pichapicha....
Ova
Mallard ayo utasikia familia ya bilionea fulani,aise jamaa machawa sanaArusha kila mtu billionea kule shenzi type
Hahahahhahah anatuona sie wa Mwakaleli kinoma yani 😂😂😂Mallard ayo utasikia familia ya bilionea fulani,aise jamaa machawa sana
Kuna habari yao moja eti walisema,mtoto wa bilionea kaingiza gari mtaroni ....wtf .....
Ova
Kiuhalisis denso Ni tajiri Sana tu Hilo la ubilionea sijui.mnatumiaga vigezo gani kumuita mtu tajiri?au sijui bilionea?hii tabia iko sana kanda ya kaskazi haswa arusha.Kwani mkisema familia ya mfanyabiashara haitaeleweka?
Alitakiwa ahifadhi kwanza chombo chake cha kazi mahali salama. Sasa we kuingia tu na camera nje nje unategemea nini?Habari haijasema Kama mwandishi alikuwa ameanza coverage Bali alikuwa ndio anafika msibani, au Mimi ndio nimewaka ?
Kama Ni hivo nilivoelewa Basi Ni kosa kumnyang'anya vifaa vyake
mnatumiaga vigezo gani kumuita mtu tajiri?au sijui bilionea?hii tabia iko sana kanda ya kaskazi haswa arusha.Kwani mkisema familia ya mfanyabiashara haitaeleweka?
Ingekuwa vema hizi story zenu za romance msimuliane mahome kwenu huko. Watu tunaomboleza kwa kuondokewa na Hawa madogo nyie na malavidavi tu jamvinNjoo tulale my V..😅😅
love you so more💞