PostGE2025 Vusi Thembekwayo: Haiingii akilini ushinde uchaguzi kwa 97.6% halafu uogope maandamano ya watu!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
We chawa vip kuhusu wale wakatoliki wa uvccm je walipataje kibali?
 
Nilitegemea utajibu hoja za Vusi Thembekwayo!


JokaKuu
 
Bora yangekuwa maandamano ule ulikuwa uasi, unaweza kuita machafuko walitaka tuwe na anarchy, tusitawalike.

Mwanzoni waliachiwa waandamane na wanajeshi kule Kimara muda ulivyokwenda wakagundua hakuna maandamano bali vijana wamegeukia uhuni.

Hawakujua wale vijana kule polisi tunao wahuni wa zamani wanaojua njia na ujanja wote wa kihuni.
 
Kama huwezi kumjibu Vusi hakuna shida
Nashangaa umeibukia huku baada ya kukimbia hoja ya Wakatoliki feki . Tuliuza yale maandamano ya Wakatoliki yalikuwa halali?
 

..Polisi wameuwa watu wengi ambao hawakuwa kwenye maandamano. Hilo sijui unalizungumziaje.

Cc Nguruvi3
 
Yaani kwa “ushindi” alioupata, angekuwa anajiachia sana na wananchi kila kona ya nchi!

Lakini tokea hiyo Oktoba 29, sidhani kama keshaonekana hadharani zaidi ya mara 10.
Mara 10😂!!!! Tangu aapishwe ame engage na wananchi mara 1 tu kwenye kikao na wazee wa CCM Dar. Mara 2 zingine ni jeshini Arusha na hotuba ya mwaka mpya juzi.

Raisi wetu mpendwa inabidi awe anakutana na wananchi kwa kufanya mikutano nao. Watanzania walimpa ushindi wa kihistoria kwenye uchaguzi uliopita.
 
Imejengwa wapi?
 
Ukifanya jinai ya aina yoyote ile tukuue?
 
Samia amepoteza nafasi ya pekee sana ya kustaafu kwa heshima, PolePole alimsisitizia sana kuwa utaondoka kwa heshima Mama, acha na hizi mbio, akashupaza shingo.

Matokeo yake sasa hawezi kuondoka madarakani kwa heshima iwe kwa kujiudhuru au kwa kumaliza awamu yake kutokana na mauaji aliyofanya, heshima hiyo hana, muda wote ana hofu ya kuuliwa, uku anawasisi wa kupelekwa ICC, mara anaogopa mtoto wake Abdul atakuwa kwenye hali gani akitoka kwenye madaraka.
Nafasi ya pekee aliyomshauri Polepole ishapita, na muda haurudi nyuma.
 
..Polisi wameuwa watu wengi ambao hawakuwa kwenye maandamano. Hilo sijui unalizungumziaje.
Akirudi uni tag. Hawa watu wamepewa 'script' wafanye 'parroting''. Hawajui contents au context za script

Waliaambiwa wazungumzie uharibifu wa mali kwa nguvu. Walipouliza Watu wangapi walikufa, hoja ikafa
Wakasema kuna Wanajeshi kutoka Kenya wamekamatwa Tarime. Walipouliza wameshtakiwa wapi, hoja ikafa
Wakasema kulikuwa na coup d'etat ambayo ni Treason. Wakaulizwa nani kashtakiwa, hawana hoja
Wakasema kuna Vijana wa Kenya wameingia nchini. wakaulizwa kule mahubusu wamejaa Watanzania. Hoja ikafa

Huyo Steven Joel Ntamusano alishika bango ''ukitaka kufanya maandamano lazima kibali cha Polisi'' . Juzi tumemuuliza Wakatoliki Feki wamepewa kibali kituo gani. Bw Ntamusano kakimbia uzi, kaibukia huku

Haiwezekani ku solve tatizo kwa hila. Lazima Watanzania tukabaliane na ''Facts'' hata kama ni chungu kiasi gani.
 
Kama huwezi kumjibu Vusi hakuna shida
Nashangaa umeibukia huku baada ya kukimbia hoja ya Wakatoliki feki . Tuliuza yale maandamano ya Wakatoliki yalikuwa halali?
Hoja ya Vusi haina tofauti na ile ya Rais wa Botswana, wana haki na kila kinachotoka midomoni mwao.

Wakatoliki feki ni siasa za kupakana matope ili ionekane SSH anaa chuki na wakatoliki, CHADEMA wanapokosa hoja nzito wanakimbilia kwenye siasa za kianaharakati zinazodumu vichwani mwa watu kwa siku mbili au tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…