PostGE2025 Vusi Thembekwayo: Haiingii akilini ushinde uchaguzi kwa 97.6% halafu uogope maandamano ya watu!

PostGE2025 Vusi Thembekwayo: Haiingii akilini ushinde uchaguzi kwa 97.6% halafu uogope maandamano ya watu!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hata Mwambengele mwenyewe akikaa anajishangaa aliwezaje kudanganya kuwa kura milioni 32 zilipigwa ilhali nchi ilikua katikati ya mauaji ya halaiki.
 
Swali ni kwamba yale maandamano ya Wakatoliki Feki ni halali? Walipata wapi kibali? Kwanini hawakuchwapwa risasa za vichwani, migongoni na Tumboni?

Kwamba CHADEMA ndio wamewatuma Wakatoliki! please hawa CDM wamepanga bure kwenye vichwa vyenu.
Ingalikuwa ni Wanachama wao leo tungeongelea marehemu! Mahakamani tu wanachapwa seuse maandamano
Maandamano yasiyo na ukomo mpaka SSH atoke ikulu, hayo maneno peke yake yanatosha kuonyesha hao waandamanaji ni watu wa namna gani na kipi kilichomo vichwani mwao.

Maandamano ambayo hakuna anayekwenda kuomba kibali kwa mkuu wa Polisi wa Mkoa ili wapewe ulinzi wa kipolisi unaona kabisa hao wanataka vurugu na serikali.

Waliandamana sana CHADEMA kabla ya hizi vurugu zao za October 29, walieleza sera zao kwa mapana kadri walivyoweza. Tundu Lissu akaona haitoshi ngoja aje na kauli mbiu ya kukinukisha ili dola itoke madarakani kwa nguvu!. Hapo akalikoroga mazima.
 
Siwezi kukimbia uzi mkuu nipo hapa. Hizi ni siasa nyepesi zenye nia ya kuchafuana lakini zimeshashindwa tayari.

Tume inaendelea na kazi muda huu, tusubiri nini watakachokiweka hadharani, tatizo wapo wanasiasa wanahusika na huo uhalifu sasa wanatumia nguvu nyingi kuipaka matope tume ili isifikie lengo lililotarajiwa.

Walianza kwa kufungua kesi mahakama kuu kupinga uwepo wake. Hawajui kwamba Rais anao wajibu wa kuunda tume pale anapoona ipo haja kwa mamlaka aliyonayo.
Onyesha credibility na integrity ya Tume kutokana na mazingira ya taharuki iliyotokea
Wanolalamikiwa ndio wameunda Tume, impartiality ipo wapi?

Waziri wa Ulinzi wakati wa tukio ni kamishna wa Tume.Majaji wa Tume wametumikia pamoja na walioteua Tume
Aliyeunda Tume ana uwezo wa kukataa au kukubali mapendekezo! si Tume ya kisheria ni ushauri

Juzi kiongozi mmoja katuhumu CHADEMA hadharani kwamba walitaka mwaka uishe walete vurugu.
Huko nyuma tulisikia viongozi wakitoa hoja tofauti. Katika mazingira ambayo viongozi wa juu wanatoa matamko, uhuru wa Tume upo wapi?

Kwanini unasema watu wasubiri Tume lakini viongozi hawana subira, wanaendelea na matamko

Hii si tume ya kimahakama, haina uwezo wa kumwita shahidi au mtuhumiwa kisheria.
Maandamano ambayo hakuna anayekwenda kuomba kibali kwa mkuu wa Polisi wa Mkoa ili wapewe ulinzi wa kipolisi unaona kabisa hao wanataka vurugu na serikali.
Wakatoliki Feki walipewa kibali wapi? mbona hawajachwapa risasi za ''kuulia Wanyama'' kwa mujibu wako
Waliandamana sana CHADEMA kabla ya hizi vurugu zao za October 29, walieleza sera zao kwa mapana kadri walivyoweza. Tundu Lissu akaona haitoshi ngoja aje na kauli mbiu ya kukinukisha ili dola itoke madarakani kwa nguvu!. Hapo akalikoroga mazima.
Jambo jema, OCT29 viongozi wote wa CHADEMA walikuwa mahubusu, I mean hata wajumbe wa kamati kuu

Haya hayakuwa maandamano ya CHADEMA ni ya Wananchi, wasikilizeni mpate majibu.

JokaKuu
 
Onyesha credibility na integrity ya Tume kutokana na mazingira ya taharuki iliyotokea
Wanolalamikiwa ndio wameunda Tume, impartiality ipo wapi?

Waziri wa Ulinzi wakati wa tukio ni kamishna wa Tume.
Majaji wa Tume wametumikia pamoja na uongozi walioteua Tume
Aliyeunda Tume ana uwezo wa kuktaa au kukubali mappndekezo! si Tume ya kisheria ni ushauri

Juzi kiongozi mmoja katuhumu CHADEMA hadharani kwamba walitaka mwaka uishe walete vurugu.
Huko nyuma tulisikia viongozi wakitoa hoja tofauti
Katika mazingira ambayo viongozi wa juu wanatoa matamko, uhuru wa Tume upo wapi?

Kwanini unasema watu wasubiri Tume lakini viongozi hawana subira hiyo, wanaendelea na matamko

Hii si tume ya kimahakama, haina uwezo wa kumwita shahidi au mtuhumiwa kisheria.

Wakatoliki Feki walipewa kibali wapi? mbona hawajachwapa risasi za ''kuulia Wanyama'' kwa mujibu wako

Jambo jema, OCT29 viongozi wote wa CHADEMA walikuwa mahubusu, I mean hata wajumbe wa kamati kuu

Haya hayakuwa maandamano ya CHADEMA ni ya Wananchi, wasikilizeni mpate majibu.

JokaKuu
Walioleta taharuki walitaka nchi isitawalike ili mabwana zao warudi tena kwa mgongo wa wale jamaa wa no reform.

Maisha yakaendelea kama kawaida kwa nia ya kuitetea Tanzania katika vita mbaya dhidi ya wasaliti tulionao humu humu kati yetu.

CCM ina miaka 48 usitegemee ukawepo usawa wa kisiasa kwa kulinganisha na vyama vya mwaka 1992 na kuendelea. Vigumu sana kuongelea siasa za nchi hii bila ya mhusika kuwa na uhusiano wa namna moja au nyingine na CCM.

Uhuru wa tume upo katika kuhakikisha anayeshinda anaongoza nchi, kumbuka alichosema Mwigulu kilikuwa na mantiki sahihi, lazima dola ilindwe. Ikifa dola unakuwa mwanzo wa maisha ya Somalia na Sudan, umaskini wa kutisha unaanzia hapo.

Umemuona huyo mkatoliki akichoma moto kituo cha mafuta au kuvunja ATM za benki?. Umemuona huyo mkatoliki akichoma moto kituo cha mwendokasi? Wangefanya ule ujinga waliofanya wale wahuni wa Oct29 wangeshakwenda kuwasilimia wahenga waliokwisha kutangulia mbele ya haki.

Yale hayakuwa maandamano ulikuwa uhuni uliotaka kuiingiza Tanzania katika machafuko, muunganiko wa yote yaliyofanyika kuanzia kwa tume kuja kwa serikali nzima lengo lake kuu ni kulinda dola ya JMT.
 
CCM ina miaka 48 usitegemee ukawepo usawa wa kisiasa kwa kulinganisha na vyama vya mwaka 1992 na kuendelea.
Ikiwa hakuna usawa! kwanini tufanye uchaguzi? Hayo maridhiano ni ya CCM na nani aliye sawa naye?
Vigumu sana kuongelea siasa za nchi hii bila ya mhusika kuwa na uhusiano wa namna moja au nyingine na CCM.
Kama kuna mwanaCCM mwenye akili, huu ni wakati wa kutafakari hatma yake kisiasa. Kwa chuki iliyofuruta ndani ya jamii, CCM haina future! OCT29 inaeleza hali ya baadaye ya CCM
Uhuru wa tume upo katika kuhakikisha anayeshinda anaongoza nchi, kumbuka alichosema Mwigulu kilikuwa na mantiki sahihi, lazima dola ilindwe. Ikifa dola unakuwa mwanzo wa maisha ya Somalia na Sudan, umaskini wa kutisha unaanzia hapo.
Tunazungumzia Tume ya kuchunguza OCT29! Hiyo ya uchaguzi hatuna sababu ya kuijadili
Umemuona huyo mkatoliki akichoma moto kituo cha mafuta au kuvunja ATM za benki?. Umemuona huyo mkatoliki akichoma moto kituo cha mwendokasi?
Je, hayo ndiyo kibali cha Polisi? Swali ni hili ikiwa wale wa OCT29 hawakuwa na kibali, Wakatoliki Feki walikuwa na kibali kipi cha Polisi?
Wangefanya ule ujinga waliofanya wale wahuni wa Oct29 wangeshakwenda kuwasilimia wahenga waliokwisha kutangulia mbele ya haki.
Vifo vya watu si jambo la kusherehekea! nimekuasa mara nyingi. Kilichotokea ni damu kumwagika
Laana ya Damu ni nzito. Unamjua mtu anaitwa Abdallah Zombe (ACP). Unaijua hali yake baada ya Damu za watu 4. Endeleeni kupiga mvinyo, Damu haifanyiwi masihara
 
Ikiwa hakuna usawa! kwanini tufanye uchaguzi? Hayo maridhiano ni ya CCM na nani aliye sawa naye?

Kama kuna mwanaCCM mwenye akili, huu ni wakati wa kutafakari hatma yake kisiasa. Kwa chuki iliyofuruta ndani ya jamii, CCM haina future! OCT29 inaeleza hali ya baadaye ya CCM

Tunazungumzia Tume ya kuchunguza OCT29! Hiyo ya uchaguzi hatuna sababu ya kuijadili

Je, hayo ndiyo kibali cha Polisi? Swali ni hili ikiwa wale wa OCT29 hawakuwa na kibali, Wakatoliki Feki walikuwa na kibali kipi cha Polisi?

Vifo vya watu si jambo la kusherehekea! nimekuasa mara nyingi. Kilichotokea ni damu kumwagika
Laana ya Damu ni nzito. Unamjua mtu anaitwa Abdallah Zombe (ACP). Unaijua hali yake baada ya Damu za watu 4. Endeleeni kupiga mvinyo, Damu haifanyiwi masihara
Maridhiano kati ya CCM ni wengine waliopiga kura, nyinyi mlioususia uchaguzi mkiweka mbele chuki na uhasama kwenye hayo maridhiano sidhani kama mtahitajika.

Chuki ya kutengenezwa na wanasiasa, ukimvuta kando kijana akuelezee kwa kina kwanini ana chuki hawezi kujenga hoja ya maana. Mwenye akili timamu anayaona mengi sana yanayofanywa na serikali nchi nzima.

Tume ya kuchunguza october 29 wengi wetu hatujui kwanini imeundwa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa inatakiwa iwepo tume iwapo katika nchi panatokea mauaji dhidi ya ubinadamu (crime against humanity), inapokuwepo tume inabidi taasisi za kimataifa zije nchini na tume itakayoundwa huko nje ili tume mbili ziweze kufanya kazi pamoja.

Mkuu mimi ni muumini mzuri wa dini, haya ni maongezi tu ya humu mtandaoni, nauelewa uzito wa damu inayomwagika.

Inawezekana walikuwa na kibali cha polisi, hawakuchoma moto mali ya mtu yoyote wala ya serikali.

Hata SSH na wasaidizi wake kila siku wanamlilia Mungu, haki anayoitoa ni Mungu sio sisi binadamu.

Heshima kwa mamlaka lazima iwepo, huko USA Trump anapambana na waandamanaji kwa kutumia nguvu kubwa, huo ni utaratibu wa dunia nzima.
 
Eti?!
Msaafara wake umezidishwa kwa kuongezewa ulinzi kama tuko vitani, mahelkopta, bullet proof cars, na ni ni na nini!
Kina Maduro wako wapi?!
Anaruka ruka tu kama maharage yanayochemshwa!
Mwisho wake unakaribia kwa kasi!
 
Maridhiano kati ya CCM ni wengine waliopiga kura,
''Maridhiano na waliopiga kura?'' yaani watu wa mitaani tu! kwahiyo mtakusanya watu mfanye maridhiano! good
Chuki ya kutengenezwa na wanasiasa, ukimvuta kando kijana akuelezee kwa kina kwanini ana chuki hawezi kujenga hoja ya maana. Mwenye akili timamu anayaona mengi sana yanayofanywa na serikali nchi nzima.
Hivi hoja za utekaji, kupotezwa watu si za maana! Hoja za Tume huru ya uchaguzi si ya maana.
Hoja ya kuchagua Chama na Viongozi wanaotaka wao si ya maan! Hoja za rasilimali si za maana!
Tume ya kuchunguza october 29 wengi wetu hatujui kwanini imeundwa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa inatakiwa iwepo tume iwapo katika nchi panatokea mauaji dhidi ya ubinadamu (crime against humanity), inapokuwepo tume inabidi taasisi za kimataifa zije nchini na tume itakayoundwa huko nje ili tume mbili ziweze kufanya kazi pamoja.
Hoja ni credibility and integrity ya Tume. Pili, je Tume ina nguvu za kisheria? Je Tume ni inclusive ili kuleta impartiality katika taarifa yake? Je taarifa ya Tume ni ''legally binding?''
Pili, ni sheria gani ya Nchi au ya Kimataifa inayoelekeza kwamba lazima kuwe na local investigation kabla ya Tume za nje hazijaja kufanya kazi.
 
Eti?!
Msaafara wake umezidishwa kwa kuongezewa ulinzi kama tuko vitani, mahelkopta, bullet proof cars, na ni ni na nini!
Kina Maduro wako wapi?!
Anaruka ruka tu kama maharage yanayochemshwa!
Mwisho wake unakaribia kwa kasi!
Jana kawadhihaki watu aliowaua, na kawadhihaki Watanzania wote kwamba hatuna cha kumfanya.
 
''Maridhiano na waliopiga kura?'' yaani watu wa mitaani tu! kwahiyo mtakusanya watu mfanye maridhiano! good

Hivi hoja za utekaji, kupotezwa watu si za maana! Hoja za Tume huru ya uchaguzi si ya maana.
Hoja ya kuchagua Chama na Viongozi wanaotaka wao si ya maan! Hoja za rasilimali si za maana!

Hoja ni credibility and integrity ya Tume. Pili, je Tume ina nguvu za kisheria? Je Tume ni inclusive ili kuleta impartiality katika taarifa yake? Je taarifa ya Tume ni ''legally binding?''
Pili, ni sheria gani ya Nchi au ya Kimataifa inayoelekeza kwamba lazima kuwe na local investigation kabla ya Tume za nje hazijaja kufanya kazi.
Zipo taasisi za dini vipo vyama mbalimbali vya kijamii. Hao wataridhiana, huwezi kuridhiana na watu waliotaka uchaguzi usifanyike nchi iingie kwenye vurugu.

Utekaji upo dunia nzima na sio kweli kwamba kila anayetekwa mhusika mkuu ni serikali, Padre kule Tabora alipotea kwa wiki nzima watu wakasema katekwa kumbe kafichwa na kimada mmoja. Wengine wanatekana baada ya kwanza kuwa wamedhulumiana kwenye biashara au wamekwazana.

Mkuu hiyo tume imeundwa kwa msingi wa kisheria kwa sababu maalum, huwezi kumuweka Heche humo eti kwa kigezo cha kuweka usawa. Hapo cha muhimu ni kuweka msingi wa kisheria kwamba kuna kitu kinafanyika humu nchini. Hiyo tume itafanya kazi na tume ambayo inaweza kuja kuchunguza suala hili ikitokea AU au EU.

Huwezi kumkamata SSH wakati tayari ipo tume inafanya kazi, Kenya walifanya kosa la kutounda tume mwaka 2007 matokeo yake Kenyatta na Ruto wakapelekwa The Hague, imeundwa kwa ushauri wa AG Hamza Johari ambaye ni mtaalam wa sheria za kimataifa.

Hiyo tume ni tofauti na nyingi tulizoziea miaka ya nyuma.
 
Hata Mwambengele mwenyewe akikaa anajishangaa aliwezaje kudanganya kuwa kura milioni 32 zilipigwa ilhali nchi ilikua katikati ya mauaji ya halaiki.
Tatizo ni kukulia background ya kimaskini, kwa mtu ambaya hana tamaa ya pesa hawezi kujitoa fahamu kiasi kile kwa kujidharirisha yeye na taaluma yake kwa kuidanganya dunia.

Na shetani samiya ameweza kuitawala tanganyika atakavyo kwa sababu ameshaona majitu ya huku hayana uchungu na aridhi hii ukiyapa rushwa ya mabilion tu yatafanya chochote unachoyaagiza.
 
Jana kawadhihaki watu aliowaua, na kawadhihaki Watanzania wote kwamba hatuna cha kumfanya.
Kuna muda naona inapaswa atudharau zaidi ya hapa, ikiwezekana awe anawachapa watanganyika makofi adharani..

...pengine labda na nawa wapumbav wote wanaompa kiburi watashtuka na kugundua huyu mtu hafai kuendelea kututawala.
 
💯%.
 
Tatizo ni kukulia background ya kimaskini, kwa mtu ambaya hana tamaa ya pesa hawezi kujitoa fahamu kiasi kile kwa kujidharirisha yeye na taaluma yake kwa kuidanganya dunia.

Na shetani samiya ameweza kuitawala tanganyika atakavyo kwa sababu ameshaona majitu ya huku hayana uchungu na aridhi hii ukiyapa rushwa ya mabilion tu yatafanya chochote unachoyaagiza.
Kuhusu muungano RIP Sitta aliongelea kwanini upo kama ulivyo. Hivyo kuvumiliana ni wajibu wa kibinadamu tunao siku zote.

Huo unaodhani ujinga wa watu wa huku bara ni hekima na busara zenye kuhitajika ili maisha yaweze kusonga mbele.
 
Jana kawadhihaki watu aliowaua, na kawadhihaki Watanzania wote kwamba hatuna cha kumfanya.
Inasikitisha! sijui kwanini hawasomi hali ya Nchi. Kwani ni lazima waongee? Na kama inabidi wanashindwaje kuchagua maneno. Jana imetonesha vidonda
 
Jamaa anashangaa imewezekanaje 88% ya wapiga kura wote wajitokeze na kati ya hao 98% wakupigie kura ila cha ajabu unaogopa 2% tu ya watu kwamba watakupindua kwa maandamano!!!
Million 70 - Million 30 = ? Million 40 au sio?

Ni mfano tu lakini tuchukulie labda sasa Million 40 inakarisha Million 30 na hio Million 40 ndio 2%
 
Back
Top Bottom