Vyakula vipi umekula pindi umepigika vilivyo?

Ulikuwa unajua ni maji ya mchele au ulifikiri ni aina fulani ya chakula?
Maji ya mchele huwa yananukia,na nyumba wakiyopika mchele harufu huwepo,angeshindwaje kujua kua haya ni maji ya mchele,mkuu...?
 
Maji ya mchele huwa yananukia,na nyumba wakiyopika mchele harufu huwepo,angeshindwaje kujua kua haya ni maji ya mchele,mkuu...?
Mkuu, njaa isikie tu. Ikikukolea, hata chakula ambacho ulikuwa ukiisikia harufu yake unahisi kutapika, ukikutana nacho, unaweza usiisikie ile harufu iliyokuwa ikikukera, badala yake ikawa inanukia harufu ya chakula ukipendacho.
 
𝐔𝐠𝐚𝐥𝐢 𝐦𝐤𝐮𝐛𝐰𝐚,𝐧𝐚 𝐮𝐠𝐚𝐥𝐢 𝐦𝐝𝐨𝐠𝐨 𝐧𝐝𝐢𝐨 𝐦𝐛𝐨𝐠𝐚
 
Nishakula ugali na sukari dadeki, kuna kipindi miaka hiyo andazi mmoja tunagwana wawili halafu kimyaaa hakuna kulalamika like nothing happened ....Mungu ashukuriwe Kwa kweli wanaJF
 
Kuna Siku tumeenda kufanya kazi Fulani ya Site

Hakukuwa na maduka jirani Wala mama ntilie

Hivyo alipita Mama mmoja anatoka shambani, alikuwa amebeba mizizi Fulani hivi(Inaitwa Ming'oko) kule mikoa ya Kusini.

Ndiyo mara ya kwanza nikala hiyo Ming'oko kuepusha njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…