Vyama vinavyojinadi kuleta mabadiliko ya Katiba baada ya uchaguzi kupitia Ilani

Vyama vinavyojinadi kuleta mabadiliko ya Katiba baada ya uchaguzi kupitia Ilani

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
katiba-pc.jpg

Madai ya kuwa na katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano yamekuwa ya muda mrefu, tangu wakati wa kurejesha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, ambapo Tume ya Jaji Francis Nyalali ilipendekeza suala hilo ili katika iliyokuwepo iendane na mfumo huo.

Hata hivyo, mabadiliko ya Katiba hayakufanyika wakati huo, badala yake yalifanyika marekebisho ya baadhi ya vifungu kuonyesha kuwa Tanzania imepokea mfumo wa vyama vingi.

Madai ya Katiba mpya yameendelea kuwepo miaka kwa miaka, hadi mwaka 2011, Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete alipounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba.

Tume hiyo ilikusanya maoni na kuandika rasimu ya kwanza na ya pili ya Katiba. Baada ya hapo liliundwa Bunge Maalum ya Katiba ambalo lilijadili na kutoka na Katiba inayopendekezwa tayari kupigiwa kura za maoni.

Hata hivyo, mchakato wa kura ya maoni haukufanyika kutokana na muda kuwa finyu kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015. Baada ya Hayati Rais John Magufuli kuingia madarakani, alitangaza kutoendelea na mchakato huo, akisema anajikita kwenye maendeleo kwanza.

Hata baada ya kuingia kwa Samia Suluhu Hassan mwaka 2021, mchakato huo uliendelea kupigwa danadana. Lakini tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, CCM imeahidi kwenye ilani yake kushughulikia mchakato wa Katiba mpya.

Mbali na CCM, vyama vingine navyo vimeweka ahadi hiyo kwenye ilani zao, ikiwemo NCCR Mageuzi, CUF na CHAUMMA.

CCM
images.png


Katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2025-2030, ibara ya 47 (ii) CCM imeahidi; “Kuhuisha na kukamilisha mchakato wa katiba mpya.”

Pengine huu ni wakati ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wadau. Lakini swali linakuja, CCM italeta Katiba ittakayokata kiu ya Watanzania kwa Zaidi ya miaka 30?

Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba, CCM ni chama tawala na kina uwezekano mkubwa wa kuendelea kutawala katika uchaguzi huo. Kama Katiba ya matakwa ya wananchi isipopatikana kupitia ahadi hii, basi malalamiko yataendelea.

NCCR Mageuzi
download.jpg

Kwa upande wa chama cha NCCR Mageuzi nacho kimeendelea kuiweka ahadi hiyo kwenye ilani yake. Chama hicho kina historia ndefu ya kupigania mabadiliko nchini kama lilivyo jina lake.

Katika ilani yake ya mwaka 2025- 2030, chama hicho kimeandika kauli ya umma unaotaka ujiongoze kupitia katiba mpya.

“Sasa ni miaka 33 tangu tulipoanza kudai Katiba Mpya. Madai haya yanatokana na msukumo wa mabadiliko ulimwenguni. Hatuwezi kuzuia mabadiliko. Katiba Mpya ni lazima!

“NCCR-Mageuzi inaamini katika utawala wa kisheria, na uongozi shirikishi katika kujenga maendeleo endelevu katika jamii kwa kutumia itikadi ya UTU. Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama chetu lilikuwa ni kupata Katiba Mpya, kama kiini cha uwezo wa kujipangia utaratibu wenye kuleta maendeleo kwa wote. Maendeleo yenye kulinda UTU wa kila mtanzania na uhai wa mazingira yetu,” imesema ilani hiyo.

CHAUMMA
CHAUMMA WEB.jpg

Kwa upande wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), nacho kimeahidi kupigania madai hayo kama kitachaguliwa kuingia madarakani.

Ilani yao imesema, baada ya kupata ridhaa ya wananchi kuongoza dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanya masuala yafuatayo ya kipaumbele katika siku 100 za kwanza yakiwamo madai ya katiba mpya.

“Kuwasilisha Bungeni muswada wa Sheria kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya. Aidha muswada utapendekeza kuundwa kwa Tume kwa ajili ya kuratibu na kuandika Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kurejea taarifa mbalimbali za Tume ya Jaji Nyalali,Jaji Kisanga,Jaji Warrioba, Katiba Pendekezwa ya mwaka 2014 na taarifa Kikosi Kazi cha Rais kilichoundwa mwaka 2023/2024 na kurejea masuala mengine mtambuka kulingana na maendeleo ya Teknojia ya Habari na Mawasiliano.”

Ilani hiyo imesema tume hiyo itaundwa kwa kuvihusisha vyama vyote vya siasa, taasisi za dini, asasi za kiraia na makundi mengine ya kijamii ili kupata katiba bora na hatimaye kupigiwa kura ya maoni na wananchi.

Sambamba na hilo, CHAUMMA kimeahidi kuwa na mfumo wa Serikali Tatu yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

CUF
CUF_partylogo.png

Kwa upande wa Chama cha Wananchi (CUF), ahadi ya mabadiliko ya Katiba haijaachwa nyuma. Kimeeleza historia ya madai ya katiba mpya katila ilani yake kikiahidi kuyapigania mara baada ya kuingia madarakani.

“Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya CUF itahakikisha kuwa mchak ato wa uandaaji wa Katiba Mpya ya wananchi utafufuliwa katika ki pindi cha miezi mitatu baada ya Serikali kuapishwa.”

Ilani hiyo imesema Katiba ya wana nchi itaandaliwa kwa kushirikisha wadau wote katika mjadala wa kitaifa; ikiwa ni pamoja na wataalamu wa katiba, Vyama vya siasa, madhehebu mbalimbali ya dini, wakulima, wafanyakazi, taasisi zisizo kuwa za kiserikali, wanafunzi, na makundi mbalimbali ya jamii kama wenye ulemavu, wastaafu, vijana, wanawake, wazee, na kadhalika. Mjadala huu utajikita katika kuboresha Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Warioba.

“Maoni yatakayokusanywa katika mjadala huu ndiyo yatakayokuwa msingi mkuu wa maandalizi ya Rasimu ya Katiba mpya na kuzingatia matakwa ya misingi ya demokrasia ya kweli na u endeshaji wa nchi hapo baadaye kwa chama chochote kitakachopewa ridhaa ya kuongoza nchi. Katiba Mpya itapatikana katika kipindi cha Bunge la mwaka 2026/27 na uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2028 na Uchaguzi Mkuu ujao wa mwa ka 2030 utafanyika nchini tukiwa na Katiba Mpya.

“Katiba mpya itabainisha wazi kuwa Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 ndiyo sheria mama ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzanaia,” imesema.
 
Back
Top Bottom