Vyama vya siasa ya Upinzani kushambulia vyama vya wafanyakazi ni mkakati au Heche na Nondo wanatumika?

Umeandika vizuri ila kama ni CWT basi Heche yuko sahihi. Hiyo CWT haina msaada wowote kwa mwalimu. Kugawa Tshirt kwa hela ulizomkata mwalimu ni upuuzi mtupu. Kutotetea waalimu wanapokatwa hela za mwenge ni upuuzi mwingine wa CWT. Ingekuwa sio CWT ningeunga mkono hoja yako.
 
Elimu juu ya vyama vya wafanyakazi ninayo kwakuwa mie pia ni mwanachama.Lakini natambua pia kuwa chama cha wafanyakazi chaweza kuwepo na kisitekeleze malengo ya kuanzishwa kwake.Hii ndiyo hoja yangu ya msingi.CWT kwa sasa haiwezi kutekeleza malengo ya kuanzishwa kwake kwa asilimia miamoja kwasababu ya kutekwa na ccm.Inapofika kwenye kufanya au kutekeleza maazimio magumu kama kuitisha mgomo(silaha kuu ya trade unions)CWT hawawezi tena.
Ni watu wachache wanauona huu muunganiko wa CWT na CCM na jinsi ambavyo unaathiri utekelezaji wa malengo ya kuanzishwa kwa CWT.Inawezekana wewe pia hauoni,na sikulaumu.
 
CWT nilichama la hovyo kuliko lichana lolote nililowahi kulishuhudi. Viongozi pandikizi toka sisiem kwa maslai yao na binafsi.
Walimu wangekuwa wanaskili wangeandamana kukipinga hikichama nyonyaji!!
Wanadanganya kurudisha hela lkn kimsingi hiyo ni fitna na unafiki hata matishet wanayogawa ni uzuzu wa danganya toto!
 
Wewe tafuna michango ya wafanyakazi mnayoshirikiana na serikali KUIBA mishahara yao kwa Makato ya LAZIMA.


Usifikiri wafanyakazi ni wajinga.

Hizi stori mchoko kadanganye madhumati wenzio siku ipite.
 
Umeandika ujinga sana humu baada ya kuleta hoja za maana unakuja kusema issue za T-shirt kweli walimu wanahitaji sana izo t-shirt ...stupid
Watu wakisema chama cha walimu hakina msaada kwa walimu wanamaanisha
1.walimu ndo kundi la watumishi wanaofanya kazi mpaka muda wa ziada remedial class bila kulipwa "overtime "
2.walimu ndo kundi la watumishi ambao hawana allowance yoyote salary to salary
3.walimu ndo kundi la watumishi ambao wanaishi kwenye mazingira magumu vijijini huko walimu wamegawana vyumba kwenye nyumba moja na wanaishi na familia zao.
4.walimu ndo mtumishi ambae ananyaswa na kusumbuliwa hata sehemu ambayo alitakiwa kupewa stahiki zake mf. Uhamisho n.k lkn CWT Ipo kimya.
5.walimu wanapitia nyakati ngumu sana ndo maana wanaingia kwenye mikopo isiyokua na tija wajinasue na hali ya maisha kwaio walikua wanahitaji msaada wa CWT hatua kwa hatua kwenye utetezi wa maslahi yao.
Matokeo yake viongozi CWT wamekua wabinafsi wameacha kabisa kujadili agenda za walimu na wamejikita kwenye ugomvi,kubambikiana kesi ,kuondoana kwenye chama,kuhamishana kwa kukomoana .
Kukosana baadhi ya viongozi na kutokuwepo kwa umoja ndani ya chama cha walimu hatutegemei kama kero za walimu zitakuja kufanyiwa kazi kwaio ni bora hiki chama kifutwe walimu wajue hawana mtetezi kuliko waendelee kukatwa michango yao iendelee kuliwa na wajanja wachache.
 
Mwl analazimishwa kuchangia mwenge wakati mwenge una bageti yake CWT wako kimya
 
100%
 
Kukosana baadhi ya viongozi na kutokuwepo kwa umoja ndani ya chama cha walimu
Migogoro ipo kila sehemu ,hakuna sehemu isio kuwa na Migogoro hata mawaziri wana Migogoro na mandibu wao au makatibu wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…