Uchaguzi 2020 Vyama vya Upinzani Tanzania ni dhaifu sana! Havina mikakati na watu makini wanaojua siasa!

Ukiona mnawajadili sana wapinzani ujue wapo na inaonekana wanawapa tabu sanaaa.Wasingekuwepo msinge wajadili kamwe.
 
Hili ni zao sahihi la chama tawala. Mwenyekiti wa kwanza alinukuliwa akisema kwamba upinzani imara utatokana na CCM. Viongozi wa sasa wa upinzani, kwa asimia kubwa, wanatoka CCM. Ukipanda mahindi usitarajie kuvuna mtama.
 
Mkuu kwa hili CCM pia imo.
 
Kama vyama ni dhaifu uharamia huu ktk uchaguzi ni wa nini?? Tuanzie hapo.
 

Wasukuma mna matatizo kweli kweli kwakuwa mkuu ni kabila yenu ni kusifia sifia tuu. CCM ndiyo ina udhaifu mkubwa ni chama kinachoongozwa na watu waoga na ndiyo maana hakuna maendeleo. Utaibaje na kudhulumu haki kipumbavu namna hiyo huku una chama makini.

Una jeshi la polisi una tume ya uchaguzi tena umenunua madege unajenga madaraja unaunganisha mabarabara nchi nzima ni mpumbavu tu atakaye sema chadema haina watendaji makini.

Ushamba wenu sasa unaenda mbali zaidi mpk kwenye siasa. Ushamba wa madaraka sasa tunauona mnaogopa nini
 
Kweli. Lakini CCM ina miradi. Inaweza ikajiendesha kwa kutumia mapato kutoka huko. Vipi Chadema. Hata duka hawana. Wafuasi wao, wamebaki kusifia mali binafsi za Mwenyekiti Mbowe!
 
Mnavizuia vyama hivi kufanya siasa then mnageuka kuvilaani kwamba ni dhaifu- angalieni msije ukajilaani ninyi wenyewe!! hivi vyama vipo kwenye KATIBA na SHERIA za nchi - mnavyofanya nyie CCM si sawa kabisa...mnajilaani bila kujua.
 
Kwa mazingira ya sasa ulitaka waingie msituni? Mkishavimbiwa viporo vyenu na kulewa mataputapu mnajitungia tu tungo zenu za kipumbavu.
 
Mazwazwa mnapongezana kwa mashuduu haya
 
Binafsi kwa mtazamo wangu hoja zako zina uwalakini kwa sababu zifuatazo;

1. Kama wapinzani wangelikuwa hawana uzito wowote linganifu na ccm kiushindani basi wasingelikuwa na kulazimisha wabebwe na mamlaka za chaguzi

2. Miaka mingi sasa ccm wamekuwa wakishinda katika chaguzi zilizojaa bias nyingi zinazowapendelea.

Mf. Angalia uchaguzi nyingi hasa miji ambayo upinzani umekuwa ukishinda matokeo hayajawahi kutangazwa kwa amani mpaka damu imwagwe na mamlaka za serikali dhalimu ya ccm
Rejea Arusha
Mwanza
Sehemu za Dar na
Mbeya
 
Toa ushauri sasa vifanye nini ili vifanye siasa zenye mlengo unaoupenda? , la sivyo inaonyesha hata wewe unalalamika tu.
 
Hata wewe ni mmoja wapo
 
Mbali na hoja yako ya msingi lakini Usisahau kuwa mtaji wa vyama ni watu.

Na watu wa vyama vya upinzani ni wale waliochoshwa na siasa kale za chama tawala.

Sasa unapowaza hiyo hoja yako pia jiulize ni watu wangapi wanaochoshwa na siasa kale za chama tawala kila siku maana hata viongozi wenu wastaafu baadhi yao wako wapi?

Washachoka, wanaobaki kwa sasa ni ccm maslahi, wakiguswa wanahama.
 


!
!
Subiri Kwanza Mkuu Na Samahani, Umesema je Kuhusu Mimba? Kwamba Jamaa Alipatikana Katika Mkesha Wa Mwenge! 🙌 😂 😂 😂 😂 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…