Vyama vya Upinzani vitakavyoshiriki huu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni wasaliti wa watanzania

Vyama vya Upinzani vitakavyoshiriki huu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni wasaliti wa watanzania

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
7,564
Reaction score
9,043
Chama chochote cha upinzani kitakachoshiriki huu uhuni unaoitwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni wasaliti wa watanzania.

Kwanini nasema hivyo, matukio yote yaliyoripotiwa nchi nzima yameonyesha ukiukaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za uchaguzi ambazo hazijawahi tokea toka uhuru, hivyo demokrasia na haki za binadamu zinavunjwa hadharani mchana kweupe. Kama haya yametokea mwanzo tu je kwenye kutangazwa matokeo si kasheshe?

Unapofanya kitu lazima upime faida na hasara. Ukipima faida za vyama vya upinzani kushiriki huu uchaguzi utaona kabisa ni ziro kabisa kwa upande wao. Ila kwa upande wa CCM na Magufuri wao itakuwa ni faida maana vyama vya upinzani vitamsaidia Magufuli na CCM yake kuubariki uchaguzi haramu uonekane halali mbele ya jumuiya za kimataifa.

Nini kifanyike?
yama vya upinzani visishiriki huu uchaguzi, hii itaifanya serikali, CCM na Magufuli wakose uhalali wa uchaguzi wao.

Wapinzani watakaoshiriki huu uchaguzi watakuwa ni wasaliti na ndio wale mapandikizi ya idara nyeti kwenye upinzani, huu ndio muda wa kuwatambua.
 
Haitatokea vyama vya upinzani kususia uchaguzi maana hata wao wanapiga hela za ruzuku kupitia chaguzi mnaopata taabu ni ninyi wananchi mnaowekwa front kupigwa Na jua. Viongozi ni wakati wao wa kupiga hela ndo maana kamwe hawatasusia
 
Wakae wakijua wakishiriki tu kwa sababu zozote watazotaja tutawajua ni wasaliti wachumia tumbo na wajasilia siasa.
 
Kuachia nguruwe shamba lamihogo inahtaji busara yahali yajuu sana..
 
Tanzania hakuna upinzani.

Na huu unaodhaniwa kuwa ni upinzani haujui umuhimu wa uchaguzi .

Na kama wanajua faida ya uchaguzi hawajui umuhimu na faida ya kushinda uchaguzi.

Wajiulize ni kwa nini binadamu wenzao toka CCM wapo tayari hata kuua watu kwa halaiki alimradi wapate madaraka.
Jibu ni moja CCM wanajua umuhimu wa kupata kula kupitia mgongo wa uchaguzi.

Wapinzani wale wanaorafuta ajira kupitia uongozi wa kisiasa wanapaswa kitambua kuwa kwa sasa hakuna ajira na sehemu yenye ajira yenye ulaji ni siasa.

Ni wajibu wao kutetea chakula chao.

Kama wao wananyanganywa nafasi zao za ajira hiyo mchana kweupe halafu wanaufyata na kukimbilia kwenye mitandao bila shaka wameridhika kuona wenzao wakila bata kupitia madaraka.

Mtu unaporwa begi la pesa halafu badala ya kukimbiza mwizi na kumkamata kwa msaada wa wanaochukia wezi ,unabaki kusimulia jinsi ulivyoporwa Huku mwizi akizidi kuchanja mbuga kwa maringo na majivuno.

Uswahilini zamani vibaka walikua wanachomwa na tairi shingoni.

Kwenye sio hasa wezi wananawiri na kujisifu na hata kutegemea kupata madaraka baada ya kufanikisha wizi.
 
Bado nashindwa kuzielewa akili, mitazamo, mikakati, mbinu na nia ya wanasiasa wa upinzani Tanzania, ila wakishiriki huu uchaguzi tujue kuwa hatuna upinzani Tanzania, hivyo tutafute, au tujitolee baadhi kushika jalamba la upinzani tuachane na wapinzani uchwara.
 
kushiriki huu uchaguzi fake kwa vyama vya upinzani ni kujizika kisiasa.
Wananchi tu wa kawaida na elimu zao ndogo wameelewa hali ya ukiukwaji wa sheria, katiba, demokrasia na haki za binadamu wakaamua kutojiandikisha, vipi wanasiasa wasomi kabisa wasilielewe hili?
 
Ni kweli hivi unakubali kushiriki kwenye uchaguzi wa namna hii,kiongozi huyo wa chama cha upinzani anatoa wapi ujasiri wa kuwaambia wanachama wake washiriki uchaguzi? Viongozi wa namna hii ni wa kupigwa makofi mchana kweupeeeeee!
Nalog off
 
Kisheria: Neno CHADEMA, na Chama cha Demokrasia na Maendeleo ni vitu viwili tofauti. Nitakupa mfano: Wakati nasajili kampuni yangu Brela ambayo inaishia na neno Limited.

Badala ya kumalizia kwa kuandika neno limited nikawa naandika kwa ufupi ltd kwenye Memorandum and Article of Association ikanibidi niifumue na kuandika upya kufanya marekebisho tu penye neno ltd niandike limited. Sheria inazingatia sana neno kwa neno nukta kwa Nukta. Umeelewa mkuu?

Vyama vya siasa vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria hivyo kisheria hakuna chama kinaitwa CCM, CHADEMA, CUF, n.k. Ni mazoea ya kufupisha!
 
Back
Top Bottom