1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,307
Adui mkubwa wa Taifa hili na hatima yake ni Chama cha Majambazi.Kisheria: Neno CHADEMA, na Chama cha Demokrasia na Maendeleo ni vitu viwili tofauti. Nitakupa mfano: Wakati nasajili kampuni yangu Brela ambayo inaishia na neno Limited.
Badala ya kumalizia kwa kuandika neno limited nikawa naandika kwa ufupi ltd kwenye Memorandum and Article of Association ikanibidi niifumue na kuandika upya kufanya marekebisho tu penye neno ltd niandike limited. Sheria inazingatia sana neno kwa neno nukta kwa Nukta. Umeelewa mkuu?
Vyama vya siasa vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria hivyo kisheria hakuna chama kinaitwa CCM, CHADEMA, CUF, n.k. Ni mazoea ya kufupisha!
Tangu Uhuru na kabala ya Uhuru Chaguzi zote vifupisho vya Chama ndivyo vilivyotumika .
Kutojua Historia ya nchi yetu na sababu za Uhuru ndiko kunakowasababisha majambazi haya ambayo sasa yanaiba na kupora mchana kweupe yananawiri na kushamiri kila kona ya nchi.
Hivi ni mwana kijiji gani angeweza kuandika Kirefu cha TANU.
Hivi watanzania tumelogwa na nani zaidi ya Chama cha majambazi?
Tunachagua Majina ya Vyama au Viongozi wetu wenyewe?
Kama Tume na Serikali ingesema kuwa Chadema,CUF au ACT Wazalendo ni Vyama vipya visivyosajiliwa inakuaje hata hao majambazi wakiwa majukwaani wanatamka neno Chadema au CUF au TLP ?
Kwa nini muda wote wa harakati za uandikishwaji na Teuzi waliacha zikafanywa na Hivyo Vyama vipya ambavyo havikusajiliwa?
Leo Hii kila kona ya nchi Hii ukichukua hata Form za Kujaza vitambulisho vya Mkazi ukakagua zilivyojazwa utaona sehemu kwenye Dini mtu amejaza kwa kifupi RC.
Acheni Unafiki ,dhulma ,dhambi na nia ovu za kutamani kuona vifo ,majeraha,huzuni, vilio ,vifungo, shida na dhiki za Watanzania wenzenu kwa sababu tu mnataka kukaa milele madarakani.
Tumepuuza sana misingi ya umoja wetu na undugu wetu awamu hii ya Tano.
Tunafikiri amani ya Taifa letu italetwa na dhulma na chuki dhidi ya wapinzani?
CCM wanaangalia amani ya mioyo yao kupata maslahi tuuu na sio amani ya nchi na wananchi wake wote bila kujali Vyama.
Tumefikia mahali hata pa kujigamba kimakabila na kidini alimradi tu tufurahishe wanasiasa uchwara wenye hofu na woga wa kushindwa kwenye uchaguzi.
Hamajui kuwa Vyama vya upinzani vikifa ,Watanzania wataonyesha hisia zao wazi bila kujificha wakijifanya ni wanachama wa Kile Chama Gandamizi?
Hivi hamuoni kuwa hata wafanyakazi ,wanafunzi,Wafanyabiashara wakulima wa Korosho,wanaovunjiwa nyumba zao kibaguzi na watu wa kila kada wanahofia kudai haki zao na kuandamana kwa sababu ya kushughulikiwa kwa kupigwa risasi kwa kuitwa wapinzani na wasaliti?
Ukiondoa Vyama hivyo ujue wakiandamana watajiita Chama cha mapinduzi. Na itabidi waitwe wapiga kura wetu na tutakua tumerudi nyuma sana.
Leo hii ukiifuta Timu ya Simba kwa mfano ; usitegemee wanachama wa Simba watahamia Yanga kwa moto wa kuisaidia Yanga zaidi ya kwenda kuihujumu ili nayo ifutike kwenye ulimwengu wa Soka.
Ni wajibu wa Serikali kupitia wale tuliowalipa kwa kazi ya kusimamia uandikishwaji na ujazwaji wa Form hizo kuelekeza namna ya Ujazaji wa Forma hizo mana wao ndio wanaojua vigezo walivyoviweka bila kutoa Elimu kabla na kuondoa kile walicho kiita mazoea ambayo nayo waliyazoesha wao hasa Tume ya Uchaguzi.
Walikataa tangu Mwanzo kuwa Ofisi ya Mkurugenzi haina sifa na nia njema ya kusimamia uchaguzi kwa haki na kwa usawa .
Nchi hii ina baadhi ya viongozi na watawala amabo hawajui shida ya kupotea kwa umoja wetu kwa sababu tu watu wameweka mbele matumbo yao na hawajawahi kuguswa na kisasi kinachotokana na dhulma zao zaidi ya raha wanazopata wakipewa mavyeo baada ya kutenda uovu na uhuni wao.
Matokeo ya Chama Kiovu kushika hatamu ni kama haya ambayo kinaweza kuweka mawakili nchi nzima wa kutoa elimu kwa siri ya namba ya kujaza form lakini serikali yake na vyombo vyake haviwezi kutoa Elimu hiyo kwa wazi kwa watanzania wote ili kila mmoja ajue.
Tulisema mtaji mkubwa wa CCM ni kupitia ujinga wa watanzania ndio maana mpaka Karne ya 21 kuna watu wengi hata Form hawajui kuzijaza na imetangazia ulimwengu mzima kuwa wao peke yao ndio wanajua namba ya kujaza form.
Libya waliua Upinzani kwa Kisingizio cha kuleta maendeleo .
Na kweli walifanikiwa kuleta maendelo waliyoyaona ni umuhimu kuliko Uhuru wa watu.
Cha ajabu kabisa baada ya watawala kutimiza azma yao ya kutawala na kujiweka juu ya kila kitu kama Kerubi ndipo Wananchi walipokuja kuwatoa kwa marungu na mapanga na kuvurumisha majengo yao ambayo hayakuwa na tija katika mioyo yao na Uhuru wao binafsi.
Bila shaka Libya walisahau kuwa Bila kujenga Umoja wa Walibya wote maendeleo yatakua ni kwa wachache tu waliopo madarakani na familia zao.
Kuna mtu kwake maendeleo ni kuongea tu na kuonekana mbele za watu.
Kuna wengine maendeleo ni kukosoa na kukemea uovu unaofanywa na watawala na viongozi!
Sio kila binadamu ameletwa humu duniani kustarehe kwenye hayo mavitu yaliyofanywa na mikono ya watu.