Vyombo vya habari vinaua CHADEMA kwa kuripoti wanaohama — asema Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA bara

Vyombo vya habari vinaua CHADEMA kwa kuripoti wanaohama — asema Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA bara

mbona tunajua ndio maan kila vipress wanakimbilia
 
Kw akuanzia na heading ya thread ni kama hataki vyombo vya habari kuripoti habari za watu wanaohama CHADEMA.

"VYOMBO VYA HABARI VINAUA CHADEMA KWA KURIPOTI WANAOHAMA — ASEMA HECHE, MAKAMU MWENYEKITI CHADEMA BARA".
Huyu aliyeleta hii habari ni sehemu ya hivyo vyombo vya habari vinavyopotosha. Alichoongea Heche kiko humu humu. Hakuna popote aliposema hivyo, bali ameonyesha udhaifu wa vyombo vya habari, na ni kwa jinsi gani wanaripoti kiupotoshaji. Tena wala hakutaja vyombo vya habari kama hoja kuu. Bali alikuwa anaweka record sawa kuwa namna vyombo vya habari vinaripoti si kweli kuwa kuna mpasuko mkubwa, na akaweka ni asilimia ngapi ya walioondoka. Walioondoka hawafiki hata asilimia 6% ya wahusika. Na hiyo ni kwa data, si kwa porojo.
 
Vyombo vya habari havina wajibu wa kuipendelea CHADEMA.

Hata kanuni ya neutrality kwenye habari kimsingi ni mazingaombwe tu, waandishi wa habari wana ajenda zao na vyombo vya habari vina pande zao.

In fact CHADEMA wanatakiwa kuwa na vyombo vyao vya habari vya kueneza ajenda zao.
Hapa nakuunga mkono 😊
 
VYOMBO VYA HABARI VINAUA CHADEMA KWA KURIPOTI WANAOHAMA — ASEMA HECHE, MAKAMU MWENYEKITI CHADEMA BARA

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mheshimiwa John Heche, ameibua hoja nzito inayolenga mahusiano ya vyombo vya habari na vyama vya siasa, akidai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinahujumu mustakabali wa CHADEMA kwa kuegemea kuripoti habari za wanachama wanaohama tu.



Kauli hii imeibua mjadala mpana kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kuchangia ustawi wa demokrasia. Kwa mtazamo wa kitaalamu wa propaganda, Heche amejaribu kuibua huruma ya umma kwa chama chake kwa kuonyesha kuwa vyombo vya habari vinachagua upande wa kupotosha hadhira badala ya kuangazia pia mafanikio na misimamo ya msingi ya chama.

Katika siasa za Tanzania leo, ambapo taarifa huenea kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii na televisheni, ujumbe wa Heche unaashiria kulinda taswira ya chama chake na kuhimiza uwiano wa kihabari.
Walipokua wakiungwa mkono na kusaidiwa kueneza zile fitina zao na Lissu walisikia raha sana sio? Leo inawauma nini? Lissu na Lema walitumika mno kuchafua wenzao kwa fitina za kishenzi na hivi Vyombo viliwapaisha sana Leo wanalia Lia!! Kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa shwaini!!
 
Cha ajabu hayo pia kayasema mbele ya vyombo vya habari, so wasiwe wanaandika?

Tatizo la chadema ni kuwa, hawakosei.
 
Yeye kaonyesha kwa ushahidi uhovyo wa vyombo vya habari tena kwa data. Kupitia taarifa yenye ukweli ndio tumeona upuuzi wa vyombo vya habari.
Hiyo ni PROJECT ya CCM mnategemea nini. Vita ya siku hizi ni ya kutumia HABARI NA MAWASILIANO. ICT. mtumie na nyinyi ubunifu wa teknolojia na habari kukuza propoganda msiwe wa kweli mno. dr Slaa atawasaidia kwa hilo. Vinginevyo mtapelekwa puta na vijana wa chaumma.
 
Hakuna popote aliposema vyombo vya habari vinaua cdm, bali amesema vyombo vya habari vinaripoti kama cdm inakufa, na akaonyesha ni jinsi gani cdm haifi kwa data, kinyume na namna vyombo vya habari vinavyotaka kupotosha. Ww mleta mada usitake kupotosha kama hatujaelewa alichosema Heche.
Na mods wanauacha uzi wenye maneno hayo.
 
Walioondoka hawafiki hata asilimia 6% ya wahusika. Na hiyo ni kwa data, si kwa porojo.
Heche akili hana hata kama waneondoka asilimia sita ni kubwa sababu walioondoka ndio matajiri wenye pesa na ma helikopta na waliokuwa wakigharimia kampeni za CHADEMA kwa pesa zao

Hajui kupiga hesabu za Takwimu na kuzitafsiri.Swala si tu wameondoka asilikia sita je hao asilimia sita ni nani hasa kiuzito ndani ya CHADEMA ?
 
Hiyo ni PROJECT ya CCM mnategemea nini. Vita ya siku hizi ni ya kutumia HABARI NA MAWASILIANO. ICT. mtumie na nyinyi ubunifu wa teknolojia na habari kukuza propoganda msiwe wa kweli mno. dr Slaa atawasaidia kwa hilo. Vinginevyo mtapelekwa puta na vijana wa chaumma.
Cdm ilisharuka hatua hizo za kupotezwa maboya na propaganda mfu. Alichofanya Heche ni kuviharibia biashara vyombo vya habari.
 
Heche akili hana hata kama waneondoka asilimia sita ni kubwa sababu walioondoka ndio matajiri wenye pesa na ma helikopta na waliokuwa wakigharimia kampeni za CHADEMA kwa pesa zao

Hajui kupiga hesabu za Takwimu na kuzitafsiri.Swala si tu wameondoka asilikia sita je hao asilimia sita ni nani hasa kiuzito ndani ya CHADEMA ?
Cdm ndio ilikuwa haitaki hao matajiri uchwara kwani waligeuza cdm kuwa chama cha madalali. Na kwa kudhibitisha wakaanza na mkuu wa hao wanaojiita wafanyabiashara sijui matajiri. Cdm ni chama cha wananchi wa kawaida, si cha wauza unga, wakwepa kodi na majizi kama ilivyo ccm. Waende huko chauma ndio chenye uhaba wa wafuasi.
 
Kama wanatoa takwimu za kweli za wanachama wanaohama,hapo hakuna kosa🤔🤔
 
Wala hajataka vyombo vya habari viipendelee cdm. Bali ameviumbua vyombo vya habari kuripoti jambo kishabiki na akaweka ukweli ni upi kwa data. Ni kama kaviumbua vyombo vya habari, na wala hakuwa anataka huruma yao.
Kwahiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema anakiri chama kinakufa ndio maana analalamika. Yupo kinyume na ninyi mlio JF mnosema, "waondoke tu"! Ahahahahaha!!!
 
Kwahiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema anakiri chama kinakufa ndio maana analalamika. Yupo kinyume na ninyi mlio JF mnosema, "waondoke tu"! Ahahahahaha!!!
Yaani hapa ndio umejiona unajua kupindisha maana. Naona kila mwanaccm anatamani cdm ijione inakufa kwa kugomea uchaguzi wa kuhuni. Hilo mtasubiri sana.
 
Vyombo vya habari ni wafanya biashara sio mambo ya taaluma tu!!.Kama vile siasa nayo ni biashara ofisi yake ni mdomo,kama ni hivyo na yeye aitakie mema CCM au CHAUMA aone watakavyimkimbia wale kindakindaki
 
Back
Top Bottom