Vyombo vya habari vinaua CHADEMA kwa kuripoti wanaohama — asema Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA bara

Vyombo vya habari vinaua CHADEMA kwa kuripoti wanaohama — asema Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA bara

Yaani hapa ndio umejiona unajua kupindisha maana. Naona kila mwanaccm anatamani cdm ijione inakufa kwa kugomea uchaguzi wa kuhuni. Hilo mtasubiri sana.
Hata Roma wakati inasambaratika viongozi na chawa wa viongozi hawakukubali hadi iliposambaratika kabisa. Time will tell.
 
Vyombo vya habari havina wajibu wa kuipendelea CHADEMA.

Hata kanuni ya neutrality kwenye habari kimsingi ni mazingaombwe tu, waandishi wa habari wana ajenda zao na vyombo vya habari vina pande zao.

In fact CHADEMA wanatakiwa kuwa na vyombo vyao vya habari vya kueneza ajenda zao.
CCM wanamiliki TBC
 
VYOMBO VYA HABARI VINAUA CHADEMA KWA KURIPOTI WANAOHAMA — ASEMA HECHE, MAKAMU MWENYEKITI CHADEMA BARA

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mheshimiwa John Heche, ameibua hoja nzito inayolenga mahusiano ya vyombo vya habari na vyama vya siasa, akidai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinahujumu mustakabali wa CHADEMA kwa kuegemea kuripoti habari za wanachama wanaohama tu.

Kauli hii imeibua mjadala mpana kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kuchangia ustawi wa demokrasia. Kwa mtazamo wa kitaalamu wa propaganda, Heche amejaribu kuibua huruma ya umma kwa chama chake kwa kuonyesha kuwa vyombo vya habari vinachagua upande wa kupotosha hadhira badala ya kuangazia pia mafanikio na misimamo ya msingi ya chama.

Katika siasa za Tanzania leo, ambapo taarifa huenea kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii na televisheni, ujumbe wa Heche unaashiria kulinda taswira ya chama chake na kuhimiza uwiano wa kihabari.
Chadema tangazeni wanaohamia. Naona nanyi sasa mnatangaza wanaohama tuu.
 
Hata Roma wakati inasambaratika viongozi na chawa wa viongozi hawakukubali hadi iliposambaratika kabisa. Time will tell.
Hiyo cdm tuliambiwa inasambaratika hata wakati wa watu kwenda kuunga juhudi, na hadi leo ipo. Itakuwa hii ya hawa wachache walioshindwa na kuanza nongwa?
 
Chadema tangazeni wanaohamia. Naona nanyi sasa mnatangaza wanaohama tuu.
Cdm ina mvuto automatically haihitaji promo za wahamiaji. Ifahamike kuhamia kama una biashara zako ni kutafura kutekwa, ama kuhujumiwa biashara zako. Tunataka uchaguzi wa haki tu maana kura ni siri kisha uje utoe mrejesho.
 
Acha tuhamie kimyakimya tusubiri uchaguzi 2030.
 
% 90 ya vyombo vya habari nchini ni mali ya ma ccm kwa namna moja au ingine, hayawezi kuripoti habari njema za chadema ukizingatia ndio chama tishio dhidi yao...tofauti kabisa na vyama kibaraka kama chaumma.

Chadema wanapaswa kuanzisha online radio, tv nyingi tena kwa majina tofauti kwa ajili ya kuripoti habari zao.
 
2030 karibu, tutasubiri hata 2050, lakini hatushiriki chaguzi za kipuuzi.
Naona tuandike wosia kabisa, 2050 nikiwa hai nitakuwa kikongwe kabisa, sijui mwenzangu labda bado teen-ager.
 
Wanaangalia maslahi kwanza, kama habari kuwa Chadema inakufa inauza basi ndo itakayosambaa.
 
Huenda kweli hilo ni tatizo kwao..., Sasa what is the Solution ?!!! Na hili kuzuia hii sintofahamu nadhani hao wanaohama wasingehama wala kusingekuwa na hii habari, Au habari ni za kutunga na hazitokei ?

By the way; "When a dog bites a man, that is not news, but when a man bites a dog, that is news"
 
we mdada kwani upo kwenye siku zako hujamuelewa heche alichosema ni hivi waandishi wa habari wanachukua habari za upande mmoja bila ku balance story umeelewa mama
 
Kauli hii imeibua mjadala mpana kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika kuchangia ustawi wa demokrasia. Kwa mtazamo wa kitaalamu wa propaganda, Heche amejaribu kuibua huruma ya umma kwa chama chake kwa kuonyesha kuwa vyombo vya habari vinachagua upande wa kupotosha hadhira badala ya kuangazia pia mafanikio na misimamo ya msingi ya chama.
Inaonekana hilo neno 'propaganda', unapenda sana kulitumia; una uhakika unajuwa maana yake halisi?
Kwa hiyo tuseme wewe mwenyewe unasimamia wapi, ni mpiga 'propaganda' vilevile?
 
Kauli dhaifu sana. Kumbe CHADEMA inakufa? Si alisema iko strong? Ndiyo tujue uwezo wa kiongozi ni pamoja na kujua aongee nini katika mazingira magumu. Hapa amekiri CHADEMA iko ICU.🙏🙏🙏
Nimesikia nesi akipiga kelele,dokta..dokta wahi huyu mgonjwa anavuruga vichaa wenzake...
 
nadhani wana report wanaohamia chauma na sio wanaohama cdm, kwani si wote waliohama cdm wameenda chauma, pili chadema wareport wanao jaza nafasi za waliohama kuliko kuanza kulalamika kitoto
 
Hiyo cdm tuliambiwa inasambaratika hata wakati wa watu kwenda kuunga juhudi, na hadi leo ipo. Itakuwa hii ya hawa wachache walioshindwa na kuanza nongwa?
Ina wabunge wangapi kwenye Bunge linaloisha? Inashiriki Uchaguzi Mkuu ujao?
 
Kama kweli kasema hii kauli basi Heche nae ni shenzi kwelikweli. aache ujinga kabsa na kudeka sisi wanachi tupo pamoja na chama hayo mengine hayaache tu
 
Heche ni wa hivyo sana.Kila mtu kila taasi na kila chombo Cha habari ni adui kwa CHADEMA.
Nitajie ni TV station gani imerusha live au hata kuonesha kwenye taarifa ya habari mikutano ya NO REFORMS NO ELECTION kama wanavyo rusha mikutano ya makala na chimpanzee ili ujishindie dunia iwe yako yote. Fanya hivyo chap ushindi ni wako.
Msiwe wanafiki kwa mambo yaliyo wazi kabisa
 
Back
Top Bottom