DOKEZO Vyombo vya ulinzi na Usalama taarifa hii naomba muichukulie kwa uzito mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kagame aliwahi kuahidi kumpiga Kikwete. Sina hakika kama aliwahi kufuta Kauli hii.

Anyway, Rwanda sio majirani kwa kujisahaulisha sana.
Nilikua Kigali wakati anatoa hiyo hotuba kwa vijana wa chama chake.
I was like""Damn what's wrong with you Uncle""
 
Hivi umeelewa alichoandika mleta mada? Na umepewa likes kabisa na Wasioelewa wenzio. JF ya sasa tuna upungufu mkubwa wa watu wa mijadala compared to 2010s.

Issue sio mtu atoke Rwanda avuke now kwa kujipenyeza penyeza na kujifanya ni Muha (Mha), Bali ni watu waliojikuta wako Tanzania baada ya mipaka kuwekwa na wakoloni Lakin originally ni Warwanda.

Sema hoja ya mleta mada inakosa mashiko sababu Rwanda-Burundi zilikua ni sehemu ya Tanganyika hivyo hata kama kuna Waha wa Rwanda nao walikua sehemu ya Tanganyika before, so wamerudi tu kwao. Sio kwa dhana ya upandikizi kama anavyotaka kutuaminisha.
upo sawa mkuu tunaweza kua na maoni tofauti katika hili my point ilikua hii

why waha..?na sio wengine.?
je nikuwafanya wajione ni sehemu ya wanyarwanda?

my views ilikua sehemu za mipaka Kuna muingiliano mkubwa wa nchi mbili lakn kwanini huyu mtu ambae kwa cv zake lazma ni mtu wa usalama pia katika nchi yake kwenda specific kwa waha?

answer was planting more sleeper Agents. why.?

ukijiuliza whats is happening in Congo eneo LA kivu unakuta Kuna watu wanaitwa BANYAMULENGE hawa watu ni raia official wa Congo lakn lugha na tamaduni zao ni za tutsi na mpaka Leo tunaona machafuko ya kila siku eneo la kivu lakn nn sababu?
ni hili kabila LA BANYAMULENGE ambao kiasili ni wanyarwanda lakn waliweza kujipenyeza na kua kabila kubwa pale Congo but now wanatumiwa kwenye vita kwa sababu ndani yao kulikua na sleeper agents wengi ambao walikua wanafanya ujasusi ndani ya nchi nyingine lakn wakitambulika kama Raia wa Congo

so my view was Lengo la hawa watu ni kufanya muingiliano mkubwa ambao utawafanya maybe waha kujiona waRwanda kwa msaada wa sleeper Agents waliowapandikiza kwa muda mrefu

lakn hayo ni maoni tu ndio maana kwenye comment yangu nikaeleza kua vyombo husika wataliona kwa ukubwa wake ila kwangu mimi sioni kama ni threat kwa usalama wetu

nimefika kigoma Mara moja kwanza ni sehemu yenye kamba nyingi za Jeshi kujumlisha zile za mafumzo (malezi)ambazo najua (MI)wanafanya kazi usiku na mchana pia tuna usalama wa nchi wanajua kazi zao lakn MA afisa uhamiaji wapo active sana hasa ukiwa unatoka kigoma Kuja mikoa mingine unaweza kuona mpaka kero ukaguzi uliopo

Ndio maana nikasema hili haliwezi kua threat kwetu
tuna vyombo imara Zaid ya watu wanavyo fikiri
 
Mkuu CCM tumetoka nayo mbali sana
I dont care mmetoka nayo wapi lakin kama taifa, ccm ni a very powerful machine, na ndio maana kuna time nasikitika napoona kama wanakosa plan hiv kwenye succession kwapika vijana wao angalu kuje kuwepo replica za akina Mahiga, akina Salim A Salim, akina kikwete akina mkapa. Na ukiacha hao frontliners, ccm ina behind the scene machinery ambazo hutakaa uwajue ila ndio waa push mambo yanakua yanaenda.

Upinzani tuna la kujifunza hapa.
 
Nimeishi kule ujanani, serikali nzima ni ya Watutsi na nawafaham mpaka wenye ID za Rwanda ila wanaajiriwa serikali ya Uganda. Hata main opposition ilikua Besigye ili hata Museveni akidondoka cheo kibaki western Uganda.
Lakin inafahamika hakuna nchi iliobeba wakimbiz wengi wa kinyarwanda kama Uganda, na wengi walipokelewa na uraia wakapewa ndio maana hata kagamae kiuhalisia ni Raia wa Uganda .. hajakulia Rwanda yule maishabyake yote.labda hii yaweza kuwa sababu kwamba hakkkua na namna lazima wawepo tu serikalin
 
Ninaandika haya kwa sababu nakupenda nchi yangu Tanzania kwa sababu na wewe unanipenda pia. Ninaandika haya kwa sababu sitamani hata siku moja kuona machafuko ndani ya nchi yetu nzuri ya kupendeza inayotamaniwa na kila nchi/kila mtu.

Japo nimeingilia kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi yetu naimani wenye kazi yenu mpo humu na kama yatakua na tija mnaweza kuyachukua na kama hayana tija mnaweza kuachana nayo japo naimani yatakua na tija kama sio kesho hata vizazi vijavyo.

Kazi ya ulinzi ya usalama wa nchi yetu ni jukumu la kila raia mwema mwenye mapenzi mema na nchi hii bahati nzuri sana mimi ni kati ya raia wema ninayeipenda nchi yangu Tanzania, binafsi kuna taarifa humu JF wakati mwingine ninazisoma kama story na zingine ninazichukulia kwa uzito mkubwa kati ya taarifa ambayo leo hii nimeichukulia kwa uzito mkubwa ni Ndugu "Vicent Karega Mnyarwanda kudai kuwa Waha ni wenyeji wa Rwanda".

Naanzia hapa hii taarifa ingekua imesemwa na mtu kama mimi pale Rwanda wala nisingejisumbua kuja na hili bandiko ila kwa sababu imesemwa na Vicent Karega basi imebidi nije na kuwapa vyombo vya ulinzi na usalama la kufikiri kidogo.

Who is Vicent Karega?

Baada ya kupitia vyanzo anuwai nimegundua huyu mtu ni mtu muhimu sana kwenye Serikali ya Rwanda chini ya Rais Kagame.

Vicent Karega alishawahi kuwa balozi wa Rwanda Nchini South Afrika, wote tunaelewa nini kilichowapata waliokua wanajeshi wa vyeo vya juu waliokua kinyume na Sera za Kagame na kuishia kwenda kuishi South Afrika wengi wao walikula vyuma waliuliwa kipindi wanakula vyuma huyu jamaa ndio alikua balozi kule.

isitoshe Vicent Karega alishawahi kuwa Balozi wa Rwanda nchi Democratic Republic of Congo wote tunaelewa kinachoendelea pale Drc chini ya M23 rais wa Congo amekua akitoa shutuma kila kukicha Rwanda ipo nyuma ya M23 sio ajabu hata Tp mazembe waliwekewa ngumu kuvaa yale maandishi.

Pia Vicent Karega Ubelgiji walimkataa kama Balozi wa Rwanda nchini mwao, tunafahamu kati ya nchi za Ulaya Ubelgiji ndio nchi yenye Intelijensia kali sasa kama wao walimkataa hatuwezi kujua sababu ila ajabu anaweza kuteuliwa kuwa Balozi Tanzania akapokelewa vizuri tu.

Baada ya kusoma ile taarifa humu Jf kuna maswali mawili matatu nimejiuliza

Vicent Karega anasema waha wapo karibia milioni 2 hebu tujiulize hizi takwimu kazitoa wapi na watu milioni 2 ni wengi sana jeshi zima la Urusi hata milioni 2 hawafiki je mpaka ametaka kufahamu idadi ana malengo gani ?

Akazidi kusema ni Kabila la tatu kwa ukubwa nchi Tanzania mimi binafsi sifahamu hizo takwimu ila Vicent Karega anazifahamu. Plse vyombo vya ulinzi na usalama najua mpo makini sana ndio maana tunalala usingizi mtamu ila naomba muongeze umakini zaidi hasa ujajusi.

Kwanini nimetoa angalizo nlishawahi kuja na uzi humu kuonyesha jinsi Urusi anavyopandikiza raia wake nchi za jirani na mwisho wake kudai raia wake wanaonewa na kuishia kuanzisha vita kafanya hayo Georgia, Ukraine, Finland, Chechnyia...nk sio ajabu leo nchi kama Finland inataka kujenga uzio kwenye mpaka wake na Urusi ili kuzuia warusi wasiingie Finland.

Je mpaka Vicent Karega ameamua kusema haya anataka kupima Tanzania itareact vipi binafsi ningependa sana nchi kama nchi itulie isijibu kitu, Je wameshamaliza kuipeleleza nchi yetu na kufahamu ubora wetu na udhaifu wetu sitaki kuamini katika hilo.

Ni kweli Watanzania tunapenda sana wageni ila kwa dunia ya sasa ni vyema tukaanza kuangalia maslahi ya nchi kwanza turudi kwenye lile Somo letu la Uraia Ulinzi na Usalama ni Jukumu la Kila Mtanzania.

Vvyanzo vya habari.

View attachment 2810918
View attachment 2810919
Afrika tuwaze kuungana
Woga na usinambe nyuma vyaturudisha.
 
Waha tuna comment wapi maana Naona mnaanza kutugombani
Hilo jina KOBO-G ni moja kati ya majina ambayo yamechafua Ukuta mkoani kigoma kama ilivyo chata ya WAPHIBA

Je wewe ndio huyo Kobo G (jamaa mmoja mweusi saana muhitimu wa Katubuka secondary)
 
Waha wenyewe wanasemajee?
Waha sasa wanagombewa kama mpira wa kona? ...mbona miaka yote wanaambiwa na maafisa uhamiaji kuwa ni warundi? ....
Kauli za kunyanyapaa raia hasa wa Kigoma, matokeo yake ndio haya ya wajanja kuitumia fursa!.

Waha ni moja kati ya makabila 120 ya Tanzania. wana eneo lao, utamaduni na mila zao. Hata kama lugha ya kiha inafanana na Kirundi au Kinyarwanda haiwezi kuwa sababu ya kuwabatiza waha urundi au unyarwanda.
 
Hilo jina KOBO-G ni moja kati ya majina ambayo yamechafua Ukuta mkoani kigoma kama ilivyo chata ya WAPHIBA

Je wewe ndio huyo Kobo G (jamaa mmoja mweusi saana muhitimu wa Katubuka secondary)
😃😃da we jamaa umesoma cuba
 
Wabongo tunapenda Sana kujifariji laiti tungejua,hao miamb wanawatu wao Hadi wa kufoji vyeti na kuingizwa jeshini rasmi

Siibez nchi yangu,ila hakuna muda wa kua makini hivi sasa na baadae
Na walishaingiaaaa

Acha wabongo waendelee kukatika

Miziki ehh selemani ehh na wakina zuchu

Ova
 
Ninaandika haya kwa sababu nakupenda nchi yangu Tanzania kwa sababu na wewe unanipenda pia. Ninaandika haya kwa sababu sitamani hata siku moja kuona machafuko ndani ya nchi yetu nzuri ya kupendeza inayotamaniwa na kila nchi/kila mtu.

Japo nimeingilia kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi yetu naimani wenye kazi yenu mpo humu na kama yatakua na tija mnaweza kuyachukua na kama hayana tija mnaweza kuachana nayo japo naimani yatakua na tija kama sio kesho hata vizazi vijavyo.

Kazi ya ulinzi ya usalama wa nchi yetu ni jukumu la kila raia mwema mwenye mapenzi mema na nchi hii bahati nzuri sana mimi ni kati ya raia wema ninayeipenda nchi yangu Tanzania, binafsi kuna taarifa humu JF wakati mwingine ninazisoma kama story na zingine ninazichukulia kwa uzito mkubwa kati ya taarifa ambayo leo hii nimeichukulia kwa uzito mkubwa ni Ndugu "Vicent Karega Mnyarwanda kudai kuwa Waha ni wenyeji wa Rwanda".

Naanzia hapa hii taarifa ingekua imesemwa na mtu kama mimi pale Rwanda wala nisingejisumbua kuja na hili bandiko ila kwa sababu imesemwa na Vicent Karega basi imebidi nije na kuwapa vyombo vya ulinzi na usalama la kufikiri kidogo.

Who is Vicent Karega?

Baada ya kupitia vyanzo anuwai nimegundua huyu mtu ni mtu muhimu sana kwenye Serikali ya Rwanda chini ya Rais Kagame.

Vicent Karega alishawahi kuwa balozi wa Rwanda Nchini South Afrika, wote tunaelewa nini kilichowapata waliokua wanajeshi wa vyeo vya juu waliokua kinyume na Sera za Kagame na kuishia kwenda kuishi South Afrika wengi wao walikula vyuma waliuliwa kipindi wanakula vyuma huyu jamaa ndio alikua balozi kule.

isitoshe Vicent Karega alishawahi kuwa Balozi wa Rwanda nchi Democratic Republic of Congo wote tunaelewa kinachoendelea pale Drc chini ya M23 rais wa Congo amekua akitoa shutuma kila kukicha Rwanda ipo nyuma ya M23 sio ajabu hata Tp mazembe waliwekewa ngumu kuvaa yale maandishi.

Pia Vicent Karega Ubelgiji walimkataa kama Balozi wa Rwanda nchini mwao, tunafahamu kati ya nchi za Ulaya Ubelgiji ndio nchi yenye Intelijensia kali sasa kama wao walimkataa hatuwezi kujua sababu ila ajabu anaweza kuteuliwa kuwa Balozi Tanzania akapokelewa vizuri tu.

Baada ya kusoma ile taarifa humu Jf kuna maswali mawili matatu nimejiuliza

Vicent Karega anasema waha wapo karibia milioni 2 hebu tujiulize hizi takwimu kazitoa wapi na watu milioni 2 ni wengi sana jeshi zima la Urusi hata milioni 2 hawafiki je mpaka ametaka kufahamu idadi ana malengo gani ?

Akazidi kusema ni Kabila la tatu kwa ukubwa nchi Tanzania mimi binafsi sifahamu hizo takwimu ila Vicent Karega anazifahamu. Plse vyombo vya ulinzi na usalama najua mpo makini sana ndio maana tunalala usingizi mtamu ila naomba muongeze umakini zaidi hasa ujajusi.

Kwanini nimetoa angalizo nlishawahi kuja na uzi humu kuonyesha jinsi Urusi anavyopandikiza raia wake nchi za jirani na mwisho wake kudai raia wake wanaonewa na kuishia kuanzisha vita kafanya hayo Georgia, Ukraine, Finland, Chechnyia...nk sio ajabu leo nchi kama Finland inataka kujenga uzio kwenye mpaka wake na Urusi ili kuzuia warusi wasiingie Finland.

Je mpaka Vicent Karega ameamua kusema haya anataka kupima Tanzania itareact vipi binafsi ningependa sana nchi kama nchi itulie isijibu kitu, Je wameshamaliza kuipeleleza nchi yetu na kufahamu ubora wetu na udhaifu wetu sitaki kuamini katika hilo.

Ni kweli Watanzania tunapenda sana wageni ila kwa dunia ya sasa ni vyema tukaanza kuangalia maslahi ya nchi kwanza turudi kwenye lile Somo letu la Uraia Ulinzi na Usalama ni Jukumu la Kila Mtanzania.

Vvyanzo vya habari.

View attachment 2810918
View attachment 2810919

Shughulika na changamoto zako za Uchumi, itakusaidia.
 
Back
Top Bottom