Vyuo vya private na migpa mikubwa kwa nini?


Mkuu umenena
 
 
Wengi wa graduates kutoka Private universities hawana lolote. GPA ya 4.6 ya LLB hata kiingereza ni taabu. Kwenye Law school ndiyo utakuta wengi wana referral kibao.
 
WE JAMAA BOYA KWELI, TUMAINI MAKUKIRA NANI KAKWAMBIA KUNA MWANACHUO ANAPATA GPA 4.7 LLB? KUPATA 3.5 NI SHIDAA, FANYA UTAFITI KAKA USIKuRUPUKE

Hahahah mitihani yenu ninayo ni rahisi kupita maelezo
 
Wengi wa graduates kutoka Private universities hawana lolote. GPA ya 4.6 ya LLB hata kiingereza ni taabu. Kwenye Law school ndiyo utakuta wengi wana referral kibao.

Umema mkuu
 
acha majungu we kiumbe mbona elimu yako haikusaidii....! Kama machaguo yangu nimechagua 2 private utasema nimepata division three mbaya kwa kuwa nipo private! Think b4 u done that's why unapata GPA ndogo unakurupuka mpigamsul!
 

Pameanza kuwepo utamaduni wa vijana wa kileo kusema vitu kwa seeping statements na generalizations bila utafiti. Yaani mtu anakurupuka na ki-assumption chake na kuhitimisha ndio ukweli.

Vyuo vyote vinadhibitiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. Na moja wapo ya conditions muhimu kwa kila chuo ni kuhakikisha members of faculty wanakuwa na sifa zinazotakiwa. Moja ya sifa hizo ni GPA isiyopungua 3.5 kwa Wakufunzi wanafunzi (TA)wenye Shahada ya kwanza na 4 kwa Wahadhiri Wasaidizi/Shahada za Uzamili. Haitokaa itokee mtu mwenye GPA chini ya 3.5 Undergraduate afanye kazi katika taasisi za elimu ya juu, iwe za umma au binafsi.

Najua kuna cases chache zilikuwepo wakati vyuo hivi vinaanza hasa hasa miaka ya 2000, lakini si kwa hivi sasa. Na kama wapo vihiyo ni wa kujificha sana. Ukiripoti TCU wanawajibishwa mara moja.

Tuache kueneza propaganda zisizo na mashiko wala ushahidi.
 


1. Naungana nawe kushangaa tabia ya ajabu ya watu wanaojiita wamesoma kujisifia vyuo walivyosoma badala ya uwezo binafsi. Mwisho wa siku (generally speaking) hutaheshimika kwa jina la chuo chako isipokuwa quality ya unachokifanya/sema. Vinginevyo, labda utembee na label itakayokutambulisha ulikotoka (which is nonesense).

2. Je, ni kweli mfumo wa elimu unapendelea shule za serikali? Swali hili lina pande nyingi za shilingi. Hivi tunaposema serikali inapendelea shule zake tunaaminisha nini? Selection? Au mazingira ya ufundishaji na hamasa ya walimu kufanya kazi?
Kuhusu selection, mambo yamebadilika siku hizi. Zamani, ukienda shule za binafsi ilionekana huna uwezo kwa sababu mazingira ya shule za umma yalikuwa bora na hivyo watu walikimbilia mazingira bora. Siku hizi, kwa sababu ya ubovu wa shule za umma (sijui kama ndio kupendelewa?) mambo yamebadilika. Wazazi wengi wenye uwezo wa fedha wanawapeleka watoto wao shule binafsi. Ushahidi wa hili ni kwamba shule nyingi nzuri za binafsi hufanya selection kabla ya shule za serikali. The best brains (wengi) wenye uwezo kifedha wanaenda shule za binafsi, waliobaki (wasio na uwezo au kwa sababu za kiuchumi) wanaenda shule zetu za kata kusubiri kufeli.
Hivyo utaona kuwa upendeleo unaosemekana kufanywa na serikali kwa shule zake kwa maana ya selection ni nadharia tu. Wengi "wanaopendelewa" kwenda kwenye shule za umma, na wenywe nafasi kiuchumi, hawaendi labda wakipangwa shule zenye nafuu kama zile za serikali (za zamani) kwa imani kwamba kule kuna walimu na wnaafundisha.

3. Kwa nini shule za binafsi zinafanya vizuri?
Well, sababu ni nyingi. Moja, nyingi (hasa zile zenye majina) zinawalipa walimu wake vizuri na zina mifumo inayowabana wafundishe kwa ufanisi. Kwa mfano wakati mwalimu mpya mwenye Shahada anaweza kulipwa 400K serikalini, mwenzake anaweza kulipwa mpaka 1,500K kwenye shule binafsi. Wakati mwalimu wa serikalini hana morali ya kufundisha na hajawekewa mfumo wa kumdhibiti kufundisha, mwenzake wa shule binafsi ana morali na anadhibitiwa afundishe.

4. Hali ikoje vyuo vikuu (private v/s public)?.

Ili tuone kama yanayoendelea sekondari ndiyo yanayoendelea Vyuo Vikuu, ni vyema kujiuliza ubora wa elimu unategemea nini? Ubora wa elimu ya juu unategemea mambo mengi. Lakini kwa uchache kuna mambo manne makubwa.

Moja, ni mitaala/curriculum bora inayotafsiriwa kwa ufanisi kazini. Mtaala bora ni ule unaomnoa mwanafunzi wa elimu ya juu kumwelezesha kuboresha maisha ya jamii katika eneo alilosomea kwa ufanisi.

Pili, ubora wa members of the Faculty/wanataaluma waliobobea kwenye maeneo yao. Kuanzia ngazi ya chini kabisa ya TA mpaka juu, ni lazima Chuo Kikuu kihakikishe kina watu wenye uwezo kitaaluma kwa maana ya ufundishaji makini na kufanya tafiti zenye kuchangia katika body of knowledge kwa maeneo yao. Ndio maana kigezo cha kupanda madaraja kwa Walimu/Academicians wa vyuo vikuu si muda kazini bali idadi na kiwango cha tafiti walizofanya.

Tatu, ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Hapa tuna maana ya vifaa, vitabu, machapisho, maabara zenye viwango, mfumo mzuri wa kuwezesha wanafunzi kujenga tabia ya kutafiti na kadhalika.

Nne, ni ubora wa wanafunzi wanaochaguliwa. Hatuzungumzii matokeo/grades (ambazo nyingi zinaleta maswali mengi kuliko majibu) bali uwezo halisi wa wanafunzi (thinking, reasoning, originality, imagination, talents na kadhalika). Mtu anaweza kuwa na Division III kwenye mazingira mabovu lakini kichwa kimetulia kuliko mwenzake mwenye Division I ya kukaririshwa na mwalimu.

Baada ya kuangalia vigezo hivyo, sasa tuvigeukie vyuo vyetu kwa swali la jumla: Je, vinakidhi vigezo vya kutoa elimu bora? Je, vina teaching staff wenye sifa? Je, vina mitaala bora? Je, vina mazingira bora ya ufundishaji na kujifunzia? Je, ni kweli kuwa Vyuo vya Umma ni bora kuliko vile vya Binafsi?

Huenda tukatofautiana mitizamo (na mara nyingi watu hutetea vyuo walivyosoma/biases). Lakini kwa mtazamo wangu, huwezi kuchora mstari ulio wazi(clear) wa ubora kati ya vyuo vya serikali na vile vya umma. Nitajieleza.

Nchi hii kwa sasa ina vyuo vikuu ishirini na sita (26) ukiacha vile vishiriki. Katika hivyo 26, ni tisa (9) tu ndivyo vilivyo vya serikali na vilivyobaki vyote ni vya binafsi kwa maana ya kumilikiwa na mashirika ya kidini, wafanyabiashara binafsi.

Pamoja na ukweli wa mambo kuwa ni vyuo vichache sana vya umma vyenye advantage ya umri/ukongwe (Mlimani, Muhimbili SUA etc) vilivyoanza siku nyingi, vyuo vyetu vingi vya binafsi vinakabiliwa na changamoto ya uchanga kwani vingi vilianza miaka ya 2005 na vichache vikianza miaka ya 1997/8.

Kwa hiyo ni kweli kuwa Mlimani wana advantage kubwa. Kwa mujibu wa Mkandala (VC), chuo hicho kina zaidi ya Walimu/Faculty Members 600 wenye PhD (waliobaki ni au wanasoma au wanatarajia kusoma), na wanafanya sana tafiti zinazopatikana mtandaoni. Kwa upande wa ufundishaji, kwa kweli waliosoma pale mtakubaliana nami kuwa inategemea na Shule/College/Faculty. Lakini kimsingi ufundishaji sio kivile ingawa kina advantage ya resource nyingi za kumwezesha mwanafunzi kuelimika. Nenda East Africana pale Library unakutana na kila takataka inayoitwa desa kuanzia thesis za tangu miaka na miaka, vitabu, machapisho na kadhalika. Hali hii haipo kwenye vyuo vingi vigeni. Na advantage nyingine ni aina ya wanafunzi wanaochaguliwa, wengi wao wana uwezo wa kujisimamia na kusoma. The same to Muhimbili/SUA.

Lakini vyuo vingine vilivyobaki, hali ni tofauti kidogo. Kwa upande wa faculty members (moja wapo ya kigezo cha ubora) unaweza kukuta kuna chuo kina hadi watu watano wenye PhD (na wote ni maadministrators mfano SMMUCo, MUM, TEKU nk) na waliobaki ni ndugu zangu wenye shahada za mtaji. Tena unaweza kushangaa hata mwenye Bachelor ndio Dean wa Faculty (nenda TEKU, SMMUCo, UoA, MUCCOBs etc). Kwa upande wa mazingira ya kufundishia unaweza kukuta Chuo kina kajengo kamoja (UoA) na mambo yanaenda.

Kwa hiyo tukizungumzia ubora, tutakuwa tunakurupuka kudai kuwa vyuo hivi vinatoa elimu inayotegemewa. Ingawa naelewa vyuo hivi vingi vinatumia wahadhiri wa vyuo vikongwe kufundisha wanafunzi wao, lakini bado kuna walakini wa ufanisi. Mfano wanafunzi wa Masters Makumira wanafundishwa kozi nyingi na wahadhiri wa Mlimani (ambao huenda pale kwa muda mfupi) na wanafundisha kwa bidii kuliko wanavyofundisha kwenye ajira zao (lakini muda wa wiki mbili kufundisha kozi ya ya units 4-6 ni sawa?).

Hata hivyo huwezi kusema ni vyuo vya serikali peke yake. Constituent colleges za Mlimani na SUA nk zilizofumuka miaka ya majuzi nazo zinakabiliwa na hali hiyo hiyo. Nenda MUCE, MUCCOBS utakutana na yale yale unayokutana nayo TEKU, MWUCE, Mount Meru na kadhalika. Kwamba vigezo halisi vya kutoa elimu shindanishi havipo (havina wahadhiri wa kudumu wenye sifa, vinafundisha kwa mtindo wa zima moto, vina shida za utawala/ukabila/udini na matatizo mengine).

Hitimisho langu ni kwamba, huwezi kuja na sweeping statement ya "vyuo binafsi ni hovyo" kwa kuzingatia ushahidi nilioutoa hapo juu. Hata hivyo changamoto hizi tunazoziona katika vyuo vyetu vichanga (vya umma na binafsi) zinaweza kukabiliwa kadri muda unavyokwenda. Kama ushahidi wa manufaa ya umri, leo ukienda SAUT (kilichoanza mwaka 2003) utashangaa kinavyojitahidi kwenye ubora na kamwe huwezi kukibeza (na hadhi yake ni kubwa kuliko Mzumbe). Kina wahadhiri wengi seniours na waliobaki wanasoma, na kinajitahidi kwa resources. Nenda Kariuki (private) utaona kinavyojitahidi. Lakini kwa upande wa pili, vyuo vyote vichanga (UDOM, SJUT pamoja na colleges kama Ushirika nk) utakuta yale yale iwe ni public au private.

REFERENCES (Kwa wasio na allege ya kusoma):

Makulilo, V. B. (2012). The proliferation of private universities in Tanzania: Quality compromised?: University of Bayreuth, Germany: Wudpecker Journal of Educational Research Vol. 1(4), pp. 51 - 66, October 2012

Sifuna, D. N. & Sawamura, N. (2010). Challenges of Quality Education in Sub-Saharan African Countries: New York, Nova Science Publishers, Inc.,


Mosha, H. J. (2000). Conceptualizing Quality of Education. In Galabawa, J.C.J, et al. The Quality of Education in Tanzania: Issues and Experiences: Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam.
 
sawa tumekupata mkuu lakii kwenye education ya juu bado private uiversities hazijawa na uwezo mkubwa wa kiushindani na publick universities ndio maana wanaweka vigezo nafuu.kama wanauwezo kiushindani basi wakeke vigezo kama vya vyuo vya public universities/vivyo kwa upande wa sekondary private schools zimesha jijengea advantage but kuanzia advance kwenda juu not yet
 

Na dhani amepata somo hyo. Atuachie vyuo vyetu vya private
 

Inawezekana ni kwa sababu ya muda mfupi tangu vianzishwe kama nilivyoeleza, hali ambayo ni hiyo hiyo kwa vyuo vya umma vilivyoanzishwa miaka ya 2000.
Mfano huwezi kulinganisha mfumo wa utoaji wa elimu SAUT (Private) na UDOM (Public). Difference ni muda [Reference ukitaka utapata]. Na huwezi kutofautisha yanayoendelea MUCCOBS (Public) na Mwenge (Private). Vyote hivyo vinashirikiana matatizo yanayotokana na uchanga wake na vyote viko Moshi [reference ni uchunguzi wangu uliodumu kwa miezi miwili mwaka 2011].

Hoja inayojengwa hapa ni kwamba matatizo ya vyuo vyetu hayako categorized kwa misingi ya umiliki. Ingawa naelewa pia kuwa vyuo vya private vimekuwa vikisukumwa na motive ya kuifanya elimu kuwa biashara zaidi kuliko huduma. Ndio maana vingi haviwalipi vizuri watumishi wao, hali inayofanya wafanye kazi huku wakitafuta pa kwenda.
 
Wewe halafu MANAGEMENT nyingi za vyuo vya private wanawakomand WAHADHIRI wawape G.P.A kubwa


Kuna Lecturer wa Mathematics (Foundation analysis) anaitwa Sembuche alikamata nusu ya darasa Tumaini University ya Iringa, Management ikamfukuza, SUA walimchukua na wakampa mkataba mpaka amestafu na kushika ni kama kawaida.
 

Hizo sio propaganda, ndio ukweli uliopo! Hakuna haja ya kutajana majina, ila vyuo vingi private havina wakufunzi wenye sifa! Ishu ya TCU ipo lakini reality ni tofauti! Wanajua wenyewe wanachofanya
 
Kuna Lecturer wa Mathematics (Foundation analysis) anaitwa Sembuche alikamata nusu ya darasa Tumaini University ya Iringa, Management ikamfukuza, SUA walimchukua na wakampa mkataba mpaka amestafu na kushika ni kama kawaida.
kama ni kweli basi walijua ataharibu soko maana inawezekana ni kanuni ya kubembeleza wateja."sababu ukiwapa masup mengi wateja wanaweza shift udom.so udom imefanya kuwe na competition kubwa ,vyuo vya private vingi vinakubwa na hili janga.
 
kama ni kweli basi walijua ataharibu soko maana inawezekana ni kanuni ya kubembeleza wateja."sababu ukiwapa masup mengi wateja wanaweza shift udom.so udom imefanya kuwe na competition kubwa ,vyuo vya private vingi vinakubwa na hili janga.

hata udom hawawezi kuwachukua hao kwa sababu niliangalia cut off point za udom kwa upande wa masomo ya biashara unatakiwa upate kuanzia cut off ya point 5 na kuendelea it means uwe na div 2 au div 1 ya form 6.
 
hata udom hawawezi kuwachukua hao kwa sababu niliangalia cut off point za udom kwa upande wa masomo ya biashara unatakiwa upate kuanzia cut off ya point 5 na kuendelea it means uwe na div 2 au div 1 ya form 6.
mara ya mwisho udom zilishushwa point mpaka 2.5 ndugu .walishindwa kupata watu wakashusha,so wakapata watu wengi bila hivyo walikuwa wanakosa watu,na watu wengi nawajua wameenda kusoma pale na 2.5 cut off point kwa course za busness
 

MIMI SIJAWAHI KUFELI,ila sikuchaguliwa kujiunga form one shule za serikali lakini si kwa sababu nilifeli bali uchache wa shule wakati ule,pamoja na hayo hapa nchini kuna shule kama nne hizo special school na moja ilikuwepo kwenye kanda yangu ambayo ni tabora boys,

lakini niliweza kuwaburuta kibao hao unaowaita special students waliotokea tabora boys nilipotinga top ten kikanda kati ya mikoa mitatu wakati ule necta form two,na huko ndo kufeli kwangu,form four nako nilizidi wanafunzi wengi tu ambao unawaita ni special waliokuwa hapo tabora boys,na hata form six sikufeli na chuo nilichokuwa napenda nisome kilikuwa UDOM pamoja na upya wake wakati ule ila niliamua kubadili chuo baada ya kupata ushauri,na hata hiyo form six nimezidi mamia ya wanafunzi kimatokeo waliowahi kusoma hizo special school,sasa ucream unaouzungumzia ni upi?ama unafikiri nilikuwa nafanya NECTA ya kwangu peke yangu?

naona umeshindwa kujibu hoja na unataka kuhamisha mjadala uwe wa kunijadili mimi na si kuijadili topiki uliyoianzisha mwenyewe, huo ni uwezo mdogo tu unakusumbua.

nakushauri ufungue topiki ya kunijadili mimi kama umeshindwa kujadili na kutetea hoja zako,ili huko ndiko unijadili kwa wigo mpana lakini hapa naona tayari umeelemewa mpaka unataka kuikimbia mada na umekuwa mtoa mitusi kama kawaida ya watu wasio na uwezo wa kujadili kwa hoja.
 
,Mshinga mimi nimesomea TABORA SPECIAL SCHOOL(TABORABOYS)! ngoja nikuulize swali umesomea shule gani O-LEVEL,A-LEVEL ,Umesoma chuo gani na mwaka gani? nikukamate vizuri uabike humu jamvini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…