1. Naungana nawe kushangaa tabia ya ajabu ya watu wanaojiita wamesoma kujisifia vyuo walivyosoma badala ya uwezo binafsi. Mwisho wa siku (generally speaking) hutaheshimika kwa jina la chuo chako isipokuwa quality ya unachokifanya/sema. Vinginevyo, labda utembee na label itakayokutambulisha ulikotoka (which is nonesense).
2. Je, ni kweli mfumo wa elimu unapendelea shule za serikali? Swali hili lina pande nyingi za shilingi. Hivi tunaposema serikali inapendelea shule zake tunaaminisha nini? Selection? Au mazingira ya ufundishaji na hamasa ya walimu kufanya kazi?
Kuhusu selection, mambo yamebadilika siku hizi. Zamani, ukienda shule za binafsi ilionekana huna uwezo kwa sababu mazingira ya shule za umma yalikuwa bora na hivyo watu walikimbilia mazingira bora. Siku hizi, kwa sababu ya ubovu wa shule za umma (sijui kama ndio kupendelewa?) mambo yamebadilika. Wazazi wengi wenye uwezo wa fedha wanawapeleka watoto wao shule binafsi. Ushahidi wa hili ni kwamba shule nyingi nzuri za binafsi hufanya selection kabla ya shule za serikali. The best brains (wengi) wenye uwezo kifedha wanaenda shule za binafsi, waliobaki (wasio na uwezo au kwa sababu za kiuchumi) wanaenda shule zetu za kata kusubiri kufeli.
Hivyo utaona kuwa upendeleo unaosemekana kufanywa na serikali kwa shule zake kwa maana ya selection ni nadharia tu. Wengi "wanaopendelewa" kwenda kwenye shule za umma, na wenywe nafasi kiuchumi, hawaendi labda wakipangwa shule zenye nafuu kama zile za serikali (za zamani) kwa imani kwamba kule kuna walimu na wnaafundisha.
3. Kwa nini shule za binafsi zinafanya vizuri?
Well, sababu ni nyingi. Moja, nyingi (hasa zile zenye majina) zinawalipa walimu wake vizuri na zina mifumo inayowabana wafundishe kwa ufanisi. Kwa mfano wakati mwalimu mpya mwenye Shahada anaweza kulipwa 400K serikalini, mwenzake anaweza kulipwa mpaka 1,500K kwenye shule binafsi. Wakati mwalimu wa serikalini hana morali ya kufundisha na hajawekewa mfumo wa kumdhibiti kufundisha, mwenzake wa shule binafsi ana morali na anadhibitiwa afundishe.
4. Hali ikoje vyuo vikuu (private v/s public).
Ili tuone kama yanayoendelea sekondari ndiyo yanayoendelea Vyuo Vikuu, ni vyema kujiuliza ubora wa elimu unategemea nini? Ubora wa elimu ya juu unategemea mambo mengi. Lakini kwa uchache kuna mambo matatu manne makubwa.
Moja, ni mitaala/curriculum bora inayotafsiriwa kwa ufanisi kazini. Mtaala bora ni ule unaomnoa mwanafunzi wa elimu ya juu kumwelezesha kuboresha maisha ya jamii katika eneo alilosomea kwa ufanisi.
Pili, ubora wa members of the Faculty/wanataaluma waliobobea kwenye maeneo yao. Kuanzia ngazi ya chini kabisa ya TA mpaka juu, ni lazima Chuo Kikuu kihakikishe kuwa kina watu wenye uwezo kitaaluma kwa maana ya ufundishaji makini na kufanya tafiti zenye kuchangia katika body of knowledge kwa maeneo yao. Ndio maana kigezo cha kupanda madaraja kwa Walimu/Academicians wa vyuo vikuu si muda kazini bali idadi na kiwango cha tafiti walizofanya.
Tatu, ubora wa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Hapa tuna maana ya vifaa, vitabu, maabara zenye viwango, mfumo mzuri wa kuwezesha wanafunzi kujenga tabia ya kutafiti na kadhalika.
Nne, ni ubora wa wanafunzi wanaochaguliwa. Hatuzungumzii matokeo/grades (ambazo nyingi zina maswali mengi kuliko majibu) bali uwezo halisi wa wanafunzi (thinking, reasoning, originality, imagination, talents na kadhalika).
Baada ya kuangalia vigezo hivyo, sasa tuvigeukie vyuo vyetu kwa swali la jumla: Je, vinakidhi vigezo vya kutoa elimu bora? Je, vina teaching staff wenye sifa? Je, vina mitaala bora? Je, vina mazingira bora ya ufundishaji na kujifunzia?
Huenda tukatofautiana. Lakini kwa mtazamo wangu, huwezi kuchora mstari ulio wazi/clear wa ubora kati ya vyuo vya serikali na vile vya umma.
Nchi hii kwa sasa ina vyuo vikuu ishirini na sita (26) ukiacha vile vishiriki. Katika hivyo 26, ni tisa (9) tu ndivyo vilivyo vya serikali. Vilivyobaki vyote ni vya umma.
Pamoja na ukweli wa mambo kuwa ni vyuo vichache sana vya umma vyenye advantage ya umri/ukongwe (Mlimani, Muhimbili SUA etc) vilivyoanza tangu uhuru, vyuo vyetu vingi vya binafsi vinakabiliwa na changamoto ya uchanga kwani vingi vilianza miaka ya 2005 na vichache vikianza miaka ya 1997/8.
Kwa hiyo ni kweli kuwa Mlimani wana advantage kubwa. Kwa mujibu wa Mkandala (VC, chuo kina zaidi ya Walimu/Faculty Members 600 wenye PhD (waliobaki ni au wanasoma au wanatarajia kusoma), na wanafanya sana tafiti zinazopatikana mtandaoni. Kwa upande wa ufundishaji, kwa kweli waliosoma pale mtakubaliana nami kuwa inategemea na Shule/College/Faculty. Lakini kimsingi ufundishaji sio kivile ingawa kina advantage ya resource nyingi za kumwezesha mwanafunzi kuelimika. Nenda East Africana pale Library unakutana na kila takataka inayoitwa desa kuanzia thesis za tangu miaka na miaka, vitabu, machapisho na kadhalika. Hali hii haipo kwenye vyuo vingi vigeni. Na advantage nyingine ni aina ya wanafunzi wanaochaguliwa, wengi wao wana uwezo wa kujisimamia na kusoma. The same to Muhimbili/SUA.
Lakini vyuo vingine vilivyobaki, hali ni tofauti kidogo. Kwa upande wa faculty members (moja wapo ya kigezo) unaweza kukuta kuna chuo kina hadi watu watano wenye PhD (na ni maadministrators mfano SMMUCo, MUM, TEKU nk) na waliobaki ni ndugu zangu. Tena unaweza kushangaa hata mwenye Bachelor ndio Dean wa Faculty. Kwa upande wa mazingira ya kufundishia unaweza kukuta Chuo kina kajengo kamoja (UoA) na mambo yanaenda.
Kwa hiyo tukizungumzia ubora, tutasema uongo kuwa vyuo hivi vinatoa elimu inayotegemewa. Ingawa naelewa vyuo hivi vingi vinatumia wahadhiri wa vyuo vikongwe kufundisha wanafunzi wao. Mfano wanafunzi wa Masters Makumira wanafundishwa kozi nyingi na wahadhiri wa Mlimani (ambao huenda pale kwa muda mfupi) na wanafundisha kwa bidii kuliko wanavyofundisha kwenye ajira zao.
Hata hivyo huwezi kusema ni vyuo vya serikali peke yake. Constituent colleges za Mlimani na SUA nk nazo zinakabiliwa na hali hiyo hiyo. Nenda MUCE, MUCCOBS utakutana na yale yale unayokutana nayo TEKU, MWUCE, Mount Meru na kadhalika. Kwamba vigezo halisi vya kutoa elimu shindanishi havipo.
Hitimisho langu ni kwamba, huwezi kuja na sweeping statement ya "vyuo binafsi ni hovyo" kwa ushahidi nilioutoa hapo juu. Hata hivyo changamoto hizi tunazoziona katika vyuo vyetu vichanga (vya umma na binafsi) zinaweza kukabiliwa kadri muda unavyokwenda. Kama ushahidi wa manufaa ya umri, leo ukienda SAUT (kilichoanza mwaka 2003) utashangaa kinavyojitahidi kwenye ubora na kamwe huwezi kukibeza (na hadhi yake ni kubwa kuliko Mzumbe). Kina wahadhiri wengi seniours na waliobaki wanasoma, na kinajitahidi kwa resources. Nenda Kariuki (private) utaona kinavyojitahidi. Lakini kwa upande wa pili, vyuo vyote vichanga (UDOM, SJUT pamoja na colleges kama Ushirika nk) utakuta yale yale iwe ni public au private.
REFERENCES (Kwa wasio na allege ya kusoma):
Makulilo, V. B. (2012). The proliferation of private universities in Tanzania: Quality compromised?: University of Bayreuth, Germany: Wudpecker Journal of Educational Research Vol. 1(4), pp. 51 - 66, October 2012
Sifuna, D. N. & Sawamura, N. (2010). Challenges of Quality Education in Sub-Saharan African Countries: New York, Nova Science Publishers, Inc.,
Mosha, H. J. (2000). Conceptualizing Quality of Education. In Galabawa, J.C.J, et al. The Quality of Education in Tanzania: Issues and Experiences: Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam.