Wa kumrithi Hanniyeh, HAMAS wangeuchuna ingewapunguzia nini?

Wa kumrithi Hanniyeh, HAMAS wangeuchuna ingewapunguzia nini?

Huwa na tofautiana sana tu na mleta mada, ila ukimsoma vizuri andiko lake kuna hoja ambayo wengi hamuioni. Katika andiko hili amedhibiti kabisa hisia na ameongea objectively zaidi.

Ukweli mchungu niko objective kila siku, ni mahaba yenu tu; na hapa naandaa jingine la kumnanga mshirika wangu kindaki ndaki dhidi ya dhulma, Iran.

Mbona hapa nampongeza sana tu Nasrallah?

Ni adhabu tosha kwa Israeli

Kukiri upungufu si unyonge wala woga.

Ninasimama dhidi ya Israel:

IMG_20240807_102247.jpg

Lakini si kijinga.

imhotep, Bwana Utam, FaizaFoxy na ndugu dhidi ya udhwalimu, tulindane ndugu zangu.
 
Unajua huyo nduo moyo wa hamas when it comes to secret operations. Israel wamemtafuta huyo jamaa kwa muda mrefu mno
Kuna taarifa zilitolewa kuwa Israel ilifanikiwa kupata location ya huyo jamaa. Ila lengo lilikuwa kuipiga Gaza na pia kwa ajili ya mateka wakaachana nae. Huyo mwamba ndie anajua uhalisia wa Oct 7 maana alikuwa field.
 
Sinwar si mtu wa kuwekwa public, huyu mtu amefanikiwa kujificha kwa muda mrefu now wana mu expose? This guys

Labda alisha kufa kwamba wamechagua kumchanganya zaidi jahudi.

Lakini kama ni mzima kutokea Gaza atafikaje Qatari, Turkey au kwa washirika kindaki ndaki Tehran?
 
Unajua huyo nduo moyo wa hamas when it comes to secret operations. Israel wamemtafuta huyo jamaa kwa muda mrefu mno
Hamas si genge la kihalifu na halipaswi kujiendesha kama genge la kihalifu kwamba akiuawa msuka mipango linaparanganyika genge lote.

Kwa kiasi nazifahamu harakati za vyama vya kiukombozi mfanano na Hamas ambavyo sasa ni vyama vikubwa tu Katika nchi kadhaa havikujiendesha kama magenge ya kihalifu kwamba akifa kiongozi wao muhimu na mkuu basi vinasambaratika haikuwa hivyo.

Vyama vingi vya ukombozi vilifiwa na viongozi kadhaa waanzilishi na muhimu vilifiwa na mageneral waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano lakini vilichagua viongozi wapya na kusonga mbele na mapambano tena vingine viongozi walisaliti kambi.

Kwa msaada kapitie hadithi ya ukombozi au uhuru wa uchina uliopambaniwa na hawa wakomunisti wa sasa katazame namna jeshi lao la ukombozi la watu wa China lilivyopata tabu pia viongozi wao walivyokuwa wakiuawa na kufungwa na namna walivyokuwa wakipata uongozi mpya na kusukuma gurudumu.

Moyo wa mapambano wapaswa kuwa kwa wote sio kwa mtu mmoja adui akikutana na jeshi la namna hii lazima yeye achoke kama ni kinyume chake na hiki basi ni rahisi kupoteza mapambano.
 
We unafikiri hao ni waoga waoga kama wewe?
Wangekuwa sio waoga wasingejificha kwenye mashimo kama panya buku.

Sinwar sijui atakiongoza vipi hicho kikundi maana yuko shimoni 24/7 ambako hakuna network Bora hata yule Haniyeh alikuwa anazunguka huku na kule kuomba uungwaji mkono
 
Ilikua lazima hamas wachague kiongozi tena ndani ya muda mfupi hivi wamefanya lamaana
Kwanza wameonesha kwamba hamas ni taasisi kubwa kifo cha haniye kimeleta pigo ila hakijaifanya hamas kushindwa kuendelea na majambo yake
Pia imeonesha kwamba hamas wana utaratibu wao kwamba akifa fulani ama ikitokea kashindwa kuongoza basi mbadala yupo ama wapo wakutosha
Pia hamas wanatukumbusha kwamba kila sehemu lazima kuwepo na kiongozi ili majambo yaende
Mwisho sio tu hamas hata lingekua kundi jengine lolote kama lingekua na misingi imara na thabiti kama iliyonayo hamas ni lazima wangechagua kiongozi baada ya muda mfupi kama walivyofanya hamas
Mazayuni mpaka yateme bungo safari hii
Umesema vyema.

Taasisi/mamlaka yoyote lazima yawe na kiongozi anayetambuliwa na watu wote.

Kiongozi lazima awepo na afamike kwasababu bila hivyo, utakosa.

1. Muamuzi mkuu ayesimamia vision katika hiyo taasisi/mamlaka.

2. Rahisi kutokea uasi kama hakuna kiongozi anayefahamika.

3. Rahisi adui kupotosha ajenda yenu kwakutumia mwanya wakutokujulikana kwa kiongozi anayefahamika.

4. Kiongozi lazima afahamike kwasababu si tu anasaidia katika kazi za kila siku lakini pia yeye ni CHACHU ya vijana/watu kupata mwamko zaidi wakuendeleza harakazi hizo wanazopigania.

5. Maelfu ya miaka taasisi/nchi/vikundi vya kudai uhuru au hata ugaidi kumekuwepo na KIONGOZI anayejulikana.
 
Kuna taarifa zilitolewa kuwa Israel ilifanikiwa kupata location ya huyo jamaa. Ila lengo lilikuwa kuipiga Gaza na pia kwa ajili ya mateka wakaachana nae. Huyo mwamba ndie anajua uhalisia wa Oct 7 maana alikuwa field.

Hapa nakubaliana nawe 100%.

Kapigwa Hanniyeh Teheran kwenye kambi ya kijeshi. Iwe nani ndani ya Gaza ambayo ni jela ya wazi?

Kwamba nani aliidhinisha Oct 7 kama si yeye?
 
Wangekuwa sio waoga wasingejificha kwenye mashimo kama panya buku.

Sinwar sijui atakiongoza vipi hicho kikundi maana yuko shimoni 24/7 ambako hakuna network Bora hata yule Haniyeh alikuwa anazunguka huku na kule kuomba uungwaji mkono
Kwahiyo we unawaza network tu?
 
Wangekuwa sio waoga wasingejificha kwenye mashimo kama panya buku.

Sinwar sijui atakiongoza vipi hicho kikundi maana yuko shimoni 24/7 ambako hakuna network Bora hata yule Haniyeh alikuwa anazunguka huku na kule kuomba uungwaji mkono

Kutokea nje ili kuwa shabaha rahisi huo ni ujinga si ushujaa.

Nani asiyejua kuwa wakati Palestine hapati hata chakula Marekani inamsaidia Israel Hadi Kuna boots on ground?

Mashimoni ni mbinu ya medani.

Kwani hadi sasa hivi mwisrael au Marekani wanasema je?
 
  • Thanks
Reactions: 511

ISraei imeshasema itamuua muda wowote kuanzia sasa, kwa hiyo usihofu.
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Kwani wangeuchuna ingewapunguzia nini? Sasa wamemtangaza huyo imewasaidia nini?

View attachment 3063542

Au wewe hauko humo? Mbona tulioko humo tuko very proud?
Ili iweje? Hakuna siri ya kiongozi wa Hamas. Viongozi wa hamas wa kisiasa huwezi kuwaficha. Kuna wengi sana wa mambo mengine hawajulikani.

Ngoja nije na uzi.
 
Umesema vyema.

Taasisi/mamlaka yoyote lazima yawe na kiongozi anayetambuliwa na watu wote.

Kiongozi lazima awepo na afamike kwasababu bila hivyo, utakosa.

1. Muamuzi mkuu ayesimamia vision katika hiyo taasisi/mamlaka.

2. Rahisi kutokea uasi kama hakuna kiongozi anayefahamika.

3. Rahisi adui kupotosha ajenda yenu kwakutumia mwanya wakutokujulikana kwa kiongozi anayefahamika.

4. Kiongozi lazima afahamike kwasababu si tu anasaidia katika kazi za kila siku lakini pia yeye ni CHACHU ya vijana/watu kupata mwamko zaidi wakuendeleza harakazi hizo wanazopigania.

5. Maelfu ya miaka taasisi/nchi/vikundi vya kudai uhuru au hata ugaidi kumekuwepo na KIONGOZI anayejulikana.

Tatizo ni uchu wa madaraka.

Mbona Gaddafi aliendelea kuwa colonel cheo kile kile alichokuwa nacho wakati wa mapinduzi?

Vipi Samuel Doe na Sgt wake?

Huu mwendelezo wa kuonja sumu ndiyo unaoyaleta haya ya vyeo hadharani.

Likelihood hata hajakuwa consulted kwenye hii appointment na labda hata Hana habari.
 
Hawa watu wangechagua kuijenga ga,a na kuleta maendelea kwa misaada wanayopata wangekuwa mbali sana.Wao kwa kukosa akili wakachagua kuchimba mahandaki na kufanya harakati.Gaza ingekuwa zaidi ya dubai kama wasingekuwa magaidi
Unaandika tu bila kufanya kiutafiti japo kidogo!
Unajua Gaza imekuwa under siege kwa miaka mingapi?
Yaani Gaza hawakuruhusiwa na Israel kujenga hata kiwanja cha ndege,kwamba wakitaka kusafiri kwenda nje inabidi waende Misri ndio wasafiri kutokea huko!
Kila kilichokuwa kinaingia Gaza,lazima kiidhinishwe na Israel!
Sasa kama taifa,mnapangiwa mambo yenu na taifa lingine,kuna maendeleo hapo?
Ukipata muda,soma hapa;

Ili iweje? Hakuna siri ya kiongozi wa Hamas. Viongozi wa hamas wa kisiasa huwezi kuwaficha. Kuna wengi sana wa mambo mengine hawajulikani.

Ngoja nije na uzi.

Kumficha Sinwar ilikuwa muhimu kama mbinu ya kimikakati.

Kiongozi yupi mkuu wa HAMAS alikufa kifo cha kawaida?

Huoni kuwa Kila anayepewa cheo hicho anakuwa ni WA kuuwawa?

Unadhani Tareq Aziz Iraq alikuwa naibu waziri mkuu?

Kwamba behind the scene Tareq labda ndiye alikuwa #2 nani anaweza kupinga?

Hao ndiyo wapambanaji wenye tija si wagombea vyeo.
 
  • Thanks
Reactions: 511
Tatizo ni uchu wa madaraka.

Mbona Gaddafi aliendelea kuwa colonel cheo kile kile alichokuwa nacho wakati wa mapinduzi?

Vipi Samuel Doe na Sgt wake?

Huu mwendelezo wa kuonja sumu ndiyo unaoyaleta haya ya vyeo hadharani.

Likelihood hata hajakuwa consulted kwenye hii appointment na labda hata Hana habari.
sijui hata umeandika nini!
 
Back
Top Bottom