Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

Hamkatazwi kuwa na imani zenu za Mungu.

Ila mnapo anza kusema tusio na imani na Mungu wenu huyo eti tuna matatizo hapo ndio mabishano huanza.
 
Yupo ila ni katili au hayupo? Unashika kila kitu boss.
Kwa kuyapitia maandiko yenu ya Biblia na Quran kwa jinsi mlivyo mpa sifa huyo Mungu wenu kwamba ni mwema sana, mwenye huruma na upendo. Kwenye dunia hii iliyo jaa uovu na ukatili wa kila aina Mungu wenu huyo hayupo.

Hayupo.
 
Binafsi naamini ibada za mababu zetu wa kale hazikuwa na tofauti yoyote na UCHAWI!

Kwahiyo wewe kama ni poa kwako, kwa sisi wengine ni BIG NO!
 
Huu ni mwaka wa6 sijaenda kanisani naona kabisa ni hatua nzuri niliyofikia!!
Yajayo yanafurahisha.ova
 
Well said, uliyoyasema yote ni ya maana ila ujinga wetu Waafrika ndiyo unatufanya kufuata dini za watu bila hata kufikiri. Iweje mimi Mwafrika nimuabudu Myahudi ama Mwarabu, kwa sababu gani wakati mimi ndiyo mwanadamu wa kwanza hapa duniani na Mungu ameniumba kwa mfano wake? Ndiyo maana Waafrika hatuishiwi laana za njaa, vita vya kijinga (Yes, ukiangalia vita vingi hapa Afrika haswa huko Magharaibi ni Waislam kuua Wakristo kutaka taifa la Kiislam), changamoto za kiafya nakadhalika. Yote hii ni kwa sababu mizimu yetu imekasirika, mtu unaisusa DNA yako kwenda kuabudu vitu vya watu wengine si ujinga huu jamani? Wacheni tuchekwe tu na wenzetu kwa ujinga wa kujitakia.
 
Wewe dini imeleta nini zaidi ya Vita huko palestina na Israel... Wenye dini zao wanauana alafu wewe unajikuta ndio mfia dini
Siyo huko tu, hata hapa Afrika. Angalia huko Afrika Magharibi watu wanatekana na kuuana kisa dini za Wapelestina na Wayahudi ambazo hazituhusu hata kidogo. Tatizo kubwa la Waafrika ni kwamba wamechanganywa akili muda mrefu sana na hawataki kujitathmini, dunia ya leo ni ya utandawazi, usiposoma na kujuwa ukweli basi ni wewe mwenyewe ni wa kujilaumu. Utamuaduji Mwarab au Myahudi wakati wewe ni Mtanzania? Yaani tunalishwa ujinga bila hata kujionea huruma.
 
Nina YESU anayekaa ndani yangu...

Dini hiyo ni njia tu...
Siyo wewe tu, wengi hapa Afrika wanajidanganya kama hivi usemavyo ila jiulize, katika majanga yote haya tunayopata hapa Afrika ni lini Yesu alikuja kutuokoa? Chukulia mfano wa vita vya kindugu vya Rwanda na Burundi, wananchi wengi walikimbilia makanisani wakiamini kule ndipo kulikuwa na amani, mbona Yesu HAKUTOKEA kuwasaidia wafuasi wake? Afrika Magharibi wanafunzi wengi wanatekwa na kubakwa na magaidi wa Kiislam mbona si Mtume Mohammed wala Yesu alikwenda kuwaokoa? Hizi dini ni mikakati tu iliyotungwa na watu ili kuwatia hofu wanadamu na ndiyo maana wale wasiojitambua bado wanaendelea kulaanika na hizi dini.
 
Chifu Mpwawa katika vita vya maji maji aliwapaka wenzake Maji ya upako lakini risasi Mjerumani zilikuwa zinaingia na mizimu yote ilidunda.Hebu weka mzimu wenu wa Bukoba tuone.
 
Mkuu wale hawakutuambia dini zao ni bora kuliko Imani za babu zetu bali walitumia Mapanga, majambia na bunduki kutulazimisha kufata mila zao zingatia biashara ya utumwa waliouzwa ni wale waliokataa uislamu na ukristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…