Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

Waafrika ni muda sasa wa kurudia kuabudu Mizimu yetu

Ana uwezo na ana nguvu halafu binadamu anampinga.... Yani kama mtu na mjomba wake wanachezeana sharubu tu..... Kitu akiumbe mwenyewe halafu kimshinde
Ivi duniani ulikujaje jibu swali hili je pumzi unayovuta inatoka wapi je wew ni nani damu yako inatoka wapi ?
 
Wapinga mungu walikuwepo toka enzi za yesu kristo
Wapinga Mungu hao wali umbwa na nani?

Mungu yeye si ni muumbaji wa vyote, mjuzi wa vyote na anaweza yote, Sasa Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na wapinga Mungu?

Kwa nini, Aumbe binadamu wanao mpinga ilhali hataki apingwe?

Alishindwaje kuumba Binadamu wema tu, watakao mtii daima?
 
Wapinga Mungu hao wali umbwa na nani?

Mungu yeye si ni muumbaji wa vyote, mjuzi wa vyote na anaweza yote, Sasa Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na wapinga Mungu?

Kwa nini, Aumbe binadamu wanao mpinga ilhali hataki apingwe?

Alishindwaje kuumba Binadamu wema tu, watakao mtii daima?
Binadamu wema mbona tupo na mfano ni mimi hapa ambae napinga hoja yako kuna swali nimekuuliza ujanijibu bado na mwenzio kakimbia hapa
 
Ivi duniani ulikujaje
Na Mungu huyo alikujaje?

Huko alikokuwa Mungu huyo kulitoka wapi?
jibu swali hili je pumzi unayovuta inatoka wapi
Kwanza pumzi ni nini?

Mimi ninachojua kuna hewa ya Oxygen.
je wew ni nani
Mimi ni Binadamu.
damu yako inatoka wapi ?
Haitoki mahali popote pale. Ipo mwilini mwangu kama ilivyo.

Si lazima iwe imetoka mahali.
 
Na Mungu huyo alikujaje?

Huko alikokuwa Mungu huyo kulitoka wapi?

Kwanza pumzi ni nini?

Mimi ninachojua kuna hewa ya Oxygen.

Mimi ni Binadamu.

Haitoki mahali popote pale. Ipo mwilini mwangu kama ilivyo.

Si lazima iwe imetoka mahali.
Maneno meeengi point hakuna
 
Rejea kichwa cha habari tajwa hapo juu.

Dini ndio chanzo cha matatizo mengi Duniani. Katika Dunia ya leo raia wanakosa ushirkiano tu kwa sababu wanatofautiana Kidini, Mkristo anambagua Muislamu na Muislamu anambagua Mkristo. Na ubaguzi wa kidini hauzungumzwi sana ila kiukweli ndio unaotendeka kwenye ofisi nyingi na taasisi nyingi, siku hizi ubaguzi wa kikabila unaenda ukipungua, huku ubaguzi wa kidini ukizidi kukuwa.

Je Dini zilianza kuingia Afrika karne zipi;

Dini za Kiislamu na Ukristo zilianza kuingia Afrika muda mrefu uliopita. Ukristo uliingia Afrika kwa mara ya kwanza karne ya 1 BK (Baada ya Kristo) kupitia wamishonari na biashara na Waafrika wa Kaskazini. Ukristo uliendelea kuenea katika maeneo tofauti ya Afrika.

Uislamu ulianza kuingia Afrika katika karne ya 7 BK (Baada ya Kristo) kupitia kazi ya Muhammad na Waislamu wa kwanza. Kupitia biashara na uvumbuzi wa safari za jangwani, Uislamu ulienea kwa kasi katika maeneo mengi ya Afrika, haswa katika Afrika Kaskazini.

Je Kabla ya Dini hizi waafrika tulikuwa tunaabudu nini?

Kabla ya kuingia kwa dini za Kiislamu na Ukristo, tamaduni za Kiafrika zilikuwa na dini na imani za kiasili zilizojumuisha ibada ya miungu ya asili, roho za wafu, na nguvu za asili. Dini za Kiafrika zilitofautiana sana kutoka eneo moja hadi lingine na kati ya jamii tofauti za Kiafrika.

Mara nyingi, dini za Kiafrika zilijumuisha ibada ya miungu au roho za wakubwa wa kale, kama vile mababu au wazee wa kabila. Kwa mfano, jamii nyingi za Kiafrika ziliabudu miungu ya jua, mvua, na ardhi, kwa sababu vitu hivyo vilikuwa muhimu kwa maisha yao ya kila siku.

Dini za Kiafrika pia zilijumuisha ibada ya wazee na mababu waliokufa, kwa kuwa waliona kumbukumbu na heshima kwa wafu kama sehemu muhimu ya utamaduni wao. Imani hizi za kiasili zilikuwa sehemu ya utamaduni wa Kiafrika na zilisimulia hadithi za uumbaji, maisha, na mazishi.

Kwa hiyo, kabla ya kuingia kwa dini za nje, Waafrika walikuwa wanaabudu miungu yao ya asili na walikuwa na imani za kiasili zilizohusiana na maisha yao ya kila siku na utamaduni wao, na maombi yalikuwa yanafanya kazi.

MY TAKE: Ukitizama Dini hizi za Ukristo na Uislamu ni dini zilizoletwa tu Afrika. Walikuja na kutuambia Imani zao ni bora kuliko zetu, hivyo tuache Imani zetu tufate Imani zao. Dini hizi mbili zinaimiza katika Kusameheana, kutokuua, kutokudhuru, na zinaamini katika Kupendana. Inasikitisha sana hawa wenye dini zao wamekuja Afrika na kutuhubiria Amani lakini wao hawafuati hiyo Amani wala hayo mafundisho. Mbona wenye dini zao wenyewe Waisraeli na wapalestina wameshindwa kufuata maandiko na wanauana kama kuku, inakuaje mimi muhaya wa Bukoba ambaye hapo mwanzo nilikuwa naabudu mizimu nifuate maandiko hayo ambayo wahusika wenyewe wameshindwa kuyafuta.

Mimi kwa mtazamo wangu naona walitumia dini zao kama chambo hili kutuweka katika ukoloni miaka hiyo maana waarabu ndio walikuwa walanguzi wa watumwa kisha wanaenda kuwauzia wazungu. Hivyo walitumia mafundisho ya dini zao kutufanya kutufumba akili na uwezo ili iwe rahisi kututawala.

Mbona hatuoni ishara yoyote kutoka juu kwa muumba mwenyewe baada ya mapigano hayo, maana tunaambiwa maeneo yale ni matakatifu, hivyo kwa akili tu lazima kungetokea ishara ya kukataza mapigano, ila naona tu Aliakibar ndio nyingi huko Gaza, huku Shalom zikiwa nyingi huko Israel.
Kila mtu akiomba mwenyezi hamsaidie.

Sasa tumeona ni namna gani Dini hizi za kuletwa vile hazifanyi kazi, ni bora kurudi kwenye kuabudu Mizimu yetu ambayo hapo mwanzo tulikuwa tukiiomba, mwandishi mashuhuri wa vitabu Yericko Nyerere aliwahi kugusia hili, kwamba turudi kwenye Imani zetu za hawali, na mimi sasa naona umuhimu wake
Laiti ungeijua nguvu ya MUNGU usingewaza vibaya.Ukifikia level flani ya kumjua MUNGU huwezi sema hivyo.MUNGU hapendi dhihaka.Kumbuka alikukomboa kwa damu ya thamani ya Mwanae
 
Na Mungu huyo alikujaje?

Huko alikokuwa Mungu huyo kulitoka wapi?

Kwanza pumzi ni nini?

Mimi ninachojua kuna hewa ya Oxygen.

Mimi ni Binadamu.

Haitoki mahali popote pale. Ipo mwilini mwangu kama ilivyo.

Si lazima iwe imetoka mahali.
God is creative na tumeumbwa kwa mfano wake. Ukisoma kitabu cha mwanzo kinaelezea.


Vyote hivyo tulivyotengeneza wanadamu ni sababu tuna utashi wa kufikiri, kubuni na kuumba. Na uwezo wetu mpaka sasa umefikia kwenye kutatua matatizo yetu lakini sio kuongeza siku za kuishi wala kumfanya mtu aishi milele.

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wanadamu anaongezeka maarifa. Wanadamu wa sasa hawana tofauti wa watu wa babilon waliojenga mnara kumfwata muumba wao.
 
Alishindwaje kuumba Binadamu wema tu, watakao mtii daima?
According to bible MUNGU aliandaa mpango wa ukombozi wa binadamu kabla hata ya uumbaji wa binadamu. Inamaana kwamba MUNGU alijua binadamu atafanya mabaya na kwa mapenzi yake akachagua kuacha hayo mabaya yaje. Inamaama hakushindwa kuumba binadamu wema tu ila alichagua ubaya uwepo kwa sababu anazojua yeye na kwa mapenzi yake halafu akauandalia mpango kazi wa kuutokomeza.
 
Kiini cha mafundisho ya dini ya Kikristu ni upendo.
Kiini cha mafundisho ya dini ya Kiislamu ni Amani.

Ukiwa na upendo kutoka moyoni kwa kila mtu na kitu, pia, ukawa na amani ya rohoni. Basi, waweza kuiona pepo hapahapa duniani.

Enyi wanadamu achaneni na mizimu. Mtu akifa amekufa.

Kuabudu jua, hakuifanyi jua liwe Mungu.

Hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako.

Think, talk and act positevely to yourself. Hii ndo ibada ya mwanzo ya kukutenga na vurugu za walimwengu.
 
Back
Top Bottom