Waafrika tuache kulia lia kwa kukosa pesa. Tunaweza wote kuwa mabilionea

Vulmeko

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
388
Reaction score
332
Kila Mwafrika, akidhamiria, anaweza kuwa milionea au bilionea. Mimi nakataa dhana kwamba Waafrika tumelaaniwa. Kama ni laana, kwanini mabilionea hawa wa Afrika hiyo laana haijawaathiri?

Hawa hapa baadhi tu ya mabilionea Waafrika na mali zao (net worth in billions of dollars):

1. Aliko Dangote — $23.9 B — Nigeria

2. Johann Rupert & Family — $14.0 B — South Africa

3. Nicky Oppenheimer & Family — $10.4 B — South Africa

4. Nassef Sawiris — $9.6 B — Egypt

5. Mike Adenuga — $6.8 B — Nigeria

6. Abdulsamad Rabiu — $5.1 B — Nigeria

7. Naguib Sawiris — $5.0 B — Egypt

8. Koos Bekker — $3.4 B — South Africa

9. Mohamed Mansour — $3.4 B — Egypt

10. Patrice Motsepe — $3.0 B — South Africa

11. Issad Rebrab & Family — $3.0 B — Algeria

12. Mohammed Dewji — $2.2 B — Tanzania

13. Michiel Le Roux — $2.2 B — South Africa

14. Othman Benjelloun & Family — $1.6 B — Morocco

15. Anas Sefrioui & Family — $1.6 B — Morocco

16. Aziz Akhannouch & Family — $1.5 B — Morocco

17. Jannie Mouton & Family — $1.5 B — South Africa

18. Femi Otedola — $1.5 B — Nigeria

19. Christoffel Wiese — $1.5 B — South Africa

20. Youssef Mansour — $1.4 B — Egypt

Source: Forbes: Africa’s Billionaires 2025
 
Mkuu,

Unaelewa kuwa wote tukiwa mabilionea ubilionea utakuwa hauna maana?
 
Mkuu,

Inaonekana somo la uchumi hususan inflation limekupita mbali.
Mkuu, una maana turidhike na umaskini wetu kwa kuwa wote tukiwa mabilionea kutakuwa na inflation? If so, mbona hata sasa kuna inflation na mabilionea ni wachache?
 
Ni hivi.

Kila mtu akiwa bilionea, bilioni itakuwa kama ilivyo elfu sasa hivi. Itakuwa haina thamani.

Bilioni ina thamani sasa hivi kwa sababu wachache ndio walio nayo.

Huelewi wapi?
 
Naomba kujua namna ya kutambua dhahabu, almasi na tanzanite bila kwenda kwa sonara
Naomba kujua na bei zake za chini
 
Ni hivi.

Kila mtu akiwa bilionea, bilioni itakuwa kama ilivyo elfu sasa hivi. Itakuwa haina thamani.

Bilioni ina thamani sasa hivi kwa sababu wachache ndio walio nayo.

Huelewi wapi?
Mkuu, kila mtu akiwa bilionea, akawa na nyumba ya dhahabu na magari yenye uwezo wa kuruka juu, hizo mali nazo zitakuwa hazina thamani?
 
Kwanza kabisa hakuna dhahabu ya kutosha kumfanya kila mtu awe na nyumba ya dhahabu.

Pili, hata tukiweza kutengeneza dhahabu leo kila mtu awe na uwezo wa kujenga nyumba ya dhahabu, thamani ya dhahabu itashuka itakuwa sawa na matofali tu.

Thamani ya dhahabu inatokana na uchache wake. Kuna sababu zilizofanya dhahabu iwe na thamani kubwa. Dhahabu ni kati ya vitu ambavyo ni vigumu sana kuvitengeneza artificially. Ina u hache katika kutokea naturally na ina gharama sana kuitengeneza artificially.

Katika uchumi price inapatikana kutokana na nguvu za demand and supply.

Ukizidisha supply ikazidi demand price inashuka.

Dhahabu ikipatikana bwerere kila mtu awe nayo, bei yake itashuka.

Kitu kinachofanya dhahabu iwe na thamani ya juu ni uchache wake.

Mkuu, nafikiri wewe ndio hujanielewa. Mimi nimejaribu kuthibitisha kwamba umaskini tulio nao Waafrika wengi hautokani na laana. Vinginevyo hao mabilionea Waafrika wasingekuwepo; na wao laana ingewapata. Hivyo badala ya kulia lia, tutafute kujua jinsi ya kuupata ubilionea.

Nimekuuliza pia swali hujanijibu: Mbona kuna nchi nyingi zina inflation? Is it because kila mtu ni bilionea?
 
Endelea kutafuta maarifa mkuu, bado uko nyuma sana.
Mkuu, wewe uliye mbele sana, kwanini umeshindwa kutusaidia Waafrika wenzako tusibakie nyuma?

Huo ni udhihirisho kwamba hakuna mtu mwenye maarifa yote. Ukiwa na PhD ya uchumi, unaweza kuwa nyuma sana kwenye maarifa ya Public Relations. Elimu ni bahari. Endelea kutafuta maarifa utukwamue ndugu zako tunaolala hoi.
 
Mkuu, nafikiri wewe ndio hujanielewa. Mimi nimejaribu kuthibitisha kwamba umaskini tulio nao Waafrika wengi hautokani na laana. Vinginevyo hao mabilionea Waafrika wasingekuwepo; na wao laana ingewapata. Hivyo badala ya kulia lia, tutafute kujua jinsi ya kuupata ubilionea.

Nimekuuliza pia swali hujanijibu: Mbona kuna nchi nyingi zina inflation? Is it because kila mtu ni bilionea?
Suala la laana ni ujinga tu. Ni ujinga unaotokana na imani za kidini na zinazofanana na hizo.

Swali lako kwamba mbona kuna nchi nyingi zina infalation, je, zote hizo zimepata inflation kutokana na wananchi wake wote kuwa mabilionea nalo ni la kutokuelewa hoja tu.

Ni la kutokuelewa hoja kwa sababu limejengwa katika msingi kwamba njia pekee ya kufikia inflation ni nchi kuwa na mabilionea wengi sana.

Jambo ambalo si kweli na mimi sijasema hivyo. Hiyo ni logical non sequitur fallacy.

Si lazima nchi iwe na watu wote mabilionea ili kuwa na inflation.

Ila, nchi ikiwa na wananchi wote mabilionea, hapo kanuni za uchumi zinasema lazima kutakuwa na inflation.

Hizi si kanuni zangu, ni kanuni za uchumi. When too much monwy is chasing the same goods, prices go up, when this happens consistently across the board, you get inflation.

It is a matter of demand and supply.

Yani mimi nakuambia ukiwa upo Dar es salaam ni lazima uwe Tanzania, lakini ukiwa Tanzania si lazima uwe Dar esalaam.

Halafu wewe unaniuliza sasa mbona kuna watu wapo Nzega na wapo Tanzania halafu hawapo Dar es salaam?

Hujaelewa somo, umechanganya madawa.
 
Mkuu, bado unazunguka tu mbuyu. Hujajibu maswali yangu: Una maana tuache kustruggle kutafuta ubilionea kwa sababu tukiwa mabilionea wote kutakuwa na inflation?

Na je tukipata pesa nyingi tukazitumia kununua chakula cha kutosha na kukihifadhi kwenye maghala, tukajenga nyumba nzuri za kuishi(hata kama sio za dhahabu), tukawa na magari ya kifahari, hizo mali zitakosa thamani?

Wale wenye imani ya kwenda mbinguni, huwa wanasema kwamba mbinguni hakutakuwa na maskini. Watu wote huko watakuwa na raha. In other words, huko pesa haitakuwa na thamani lakini kila mtu ataishi vizuri. Ndio hoja yangu kuu. Kwamba kila mtu atafute ubilionea kwakuwa uwezekano wa kuupata upo. Tukiwa mabilionea wote, hata kama pesa haitakuwa na thamani, it doesnt matter, kama wote tutakuwa tunaishi kw raha. Kulialia hakuwezi kutusaidia. Zaidi sana tutajiletea stress na magonjwa ya pressure/moyo. Hapo vipi?
 
Sijasema tuache ku struggle kutafuta ubilionea.

Ila inaonekana una tatizo na msingi la uelewa wa uchumi.

Ubilionea utakuwa hauna maana ikiwa kila mtu atakuwa bilionea.

Leo ubaiona bilioni kubwa kwa sababu si kila mtu anayo, kila mtu akiwa nayo bilioni utanunua chupa ya maji tu.

Kila mtu akiwa bilionea, bilioni itakuwa kama elfu kila mtu atatafuta mamia ya matrillioni.

Mbona huelewi somo dogo tu la uchumi?
 
Back
Top Bottom