Fine. Tuondoke kwenye neno billionaire.
Hata hiyo wealth creation inaweza kuwa na maana kama unaongelea kuwatoa watu kwenye abject poverty na kuwapatia kazi, kuwapatia uwezo wa lishe nzuri, elimu nzuri na afya bora. Yani kusiwe na ombaomba, watu waweze kutumia resources vizuri. Hapo tuko pamoja na hiki ndicho kinatakiwa kufanyika.
Tena hili linaweza kufanyika hata kwa ku bypass uchumi wa pesa, kwa government subsidies, credit, insurance, incentives, scholarships, squaring off industry deals etc.
Lakini the moment ukitaka kila mtu awe wealthy kwa maana ya daraja la juu sana, hususan kuwa na pesa nyingi mfukoni, unarudi kulekule kwenye tatizo la economic sustainability whether unatumia neno billionaire au hutumii.
Pesa itakosa thamani kwa sababu ipo nyingi katika uchumi.
Uchumi utataka watu wengine wawe wafanyakazi na wengine wawe wamiliki wa hizo kazi, industrialists and business owners. Hili jambo huwezi kuliepuka. Wak9nunisti walitaka kuliepuka na kutengeneza a classless society wakashinswa mpaka Soviet Union ikaanguka. Mpaka sasa China washakubali market economy kwa kiasi kikubwa.
Ukitaka kila mtu awe tajiri kipesa, by any definition ya utajiri, na ukafanikiwa kila mtu akawa na utajiri huo wa kioesa, huo utajiri utakuwa si utajiri tena, utakuwa ndiyo umasikini mpya.
Matajiri watakuwa ni wale waliovuka hiyo equilibrium level mpya na kwenda kwenye next stage.