Mkuu,Kila Mwafrika, akidhamiria, anaweza kuwa milionea au bilionea. Mimi nakataa dhana kwamba Waafrika tumelaaniwa. Kama ni laana, kwanini mabilionea hawa wa Afrika hiyo laana haijawaathiri?
Hawa hapa baadhi tu ya mabilionea Waafrika na mali zao (net worth in billions of dollars):
1. Aliko Dangote — $23.9 B — Nigeria
2. Johann Rupert & Family — $14.0 B — South Africa
3. Nicky Oppenheimer & Family — $10.4 B — South Africa
4. Nassef Sawiris — $9.6 B — Egypt
5. Mike Adenuga — $6.8 B — Nigeria
6. Abdulsamad Rabiu — $5.1 B — Nigeria
7. Naguib Sawiris — $5.0 B — Egypt
8. Koos Bekker — $3.4 B — South Africa
9. Mohamed Mansour — $3.4 B — Egypt
10. Patrice Motsepe — $3.0 B — South Africa
11. Issad Rebrab & Family — $3.0 B — Algeria
12. Mohammed Dewji — $2.2 B — Tanzania
13. Michiel Le Roux — $2.2 B — South Africa
14. Othman Benjelloun & Family — $1.6 B — Morocco
15. Anas Sefrioui & Family — $1.6 B — Morocco
16. Aziz Akhannouch & Family — $1.5 B — Morocco
17. Jannie Mouton & Family — $1.5 B — South Africa
18. Femi Otedola — $1.5 B — Nigeria
19. Christoffel Wiese — $1.5 B — South Africa
20. Youssef Mansour — $1.4 B — Egypt
Source: Forbes: Africa’s Billionaires 2025
Mkuu,Wote tukiwa mabilionea, ni faida sana; hakuna atakayelia njaa. Hata siasa za kugombea ubungo zitakoma.
Ni hivi.Mkuu, una maana turidhike na umaskini wetu kwa kuwa wote tukiwa mabilionea kutakuwa na inflation? If so, mbona hata sasa kuna inflation na mabilionea ni wachache?
Mkuu, kila mtu akiwa bilionea, akawa na nyumba ya dhahabu na magari yenye uwezo wa kuruka juu, hizo mali nazo zitakuwa hazina thamani?Ni hivi.
Kila mtu akiwa bilionea, bilioni itakuwa kama ilivyo elfu sasa hivi. Itakuwa haina thamani.
Bilioni ina thamani sasa hivi kwa sababu wachache ndio walio nayo.
Huelewi wapi?
Kwanza kabisa hakuna dhahabu ya kutosha kumfanya kila mtu awe na nyumba ya dhahabu.Mkuu, kila mtu akiwa bilionea, akawa na nyumba ya dhahabu na magari yenye uwezo wa kuruka juu, hizo mali nazo zitakuwa hazina thamani?
Mkuu, nafikiri wewe ndio hujanielewa. Mimi nimejaribu kuthibitisha kwamba umaskini tulio nao Waafrika wengi hautokani na laana. Vinginevyo hao mabilionea Waafrika wasingekuwepo; na wao laana ingewapata. Hivyo badala ya kulia lia, tutafute kujua jinsi ya kuupata ubilionea.Kwanza kabisa hakuna dhahabu ya kutosha kumfanya kila mtu awe na nyumba ya dhahabu.
Pili, hata tukiweza kutengeneza dhahabu leo kila mtu awe na uwezo wa kujenga nyumba ya dhahabu, thamani ya dhahabu itashuka itakuwa sawa na matofali tu.
Thamani ya dhahabu inatokana na uchache wake. Kuna sababu zilizofanya dhahabu iwe na thamani kubwa. Dhahabu ni kati ya vitu ambavyo ni vigumu sana kuvitengeneza artificially. Ina u hache katika kutokea naturally na ina gharama sana kuitengeneza artificially.
Katika uchumi price inapatikana kutokana na nguvu za demand and supply.
Ukizidisha supply ikazidi demand price inashuka.
Dhahabu ikipatikana bwerere kila mtu awe nayo, bei yake itashuka.
Kitu kinachofanya dhahabu iwe na thamani ya juu ni uchache wake.
Huelewi wapi?
Mkuu, wewe uliye mbele sana, kwanini umeshindwa kutusaidia Waafrika wenzako tusibakie nyuma?Endelea kutafuta maarifa mkuu, bado uko nyuma sana.
Suala la laana ni ujinga tu. Ni ujinga unaotokana na imani za kidini na zinazofanana na hizo.Mkuu, nafikiri wewe ndio hujanielewa. Mimi nimejaribu kuthibitisha kwamba umaskini tulio nao Waafrika wengi hautokani na laana. Vinginevyo hao mabilionea Waafrika wasingekuwepo; na wao laana ingewapata. Hivyo badala ya kulia lia, tutafute kujua jinsi ya kuupata ubilionea.
Nimekuuliza pia swali hujanijibu: Mbona kuna nchi nyingi zina inflation? Is it because kila mtu ni bilionea?
Mkuu, bado unazunguka tu mbuyu. Hujajibu maswali yangu: Una maana tuache kustruggle kutafuta ubilionea kwa sababu tukiwa mabilionea wote kutakuwa na inflation?Suala la laana ni ujinga tu. Ni ujinga unaotokana na imani za kidini na zinazofanana na hizo.
Swali lako kwamba mbona kuna nchi nyingi zina infalation, je, zote hizo zimepata inflation kutokana na wananchi wake wote kuwa mabilionea nalo ni la kutokuelewa hoja tu.
Ni la kutokuelewa hoja kwa sababu limejengwa katika msingi kwamba njia pekee ya kufikia inflation ni nchi kuwa na mabilionea wengi sana.
Jambo ambalo si kweli na mimi sijasema hivyo. Hiyo ni logical non sequitur fallacy.
Si lazima nchi iwe na watu wote mabilionea ili kuwa na inflation.
Ila, nchi ikiwa na wananchi wote mabilionea, hapo kanuni za uchumi zinasema lazima kutakuwa na inflation.
Hizi si kanuni zangu, ni kanuni za uchumi. When too much monwy is chasing the same goods, prices go up, when this happens consistently across the board, you get inflation.
It is a matter of demand and supply.
Yani mimi nakuambia ukiwa upo Dar es salaam ni lazima uwe Tanzania, lakini ukiwa Tanzania si lazima uwe Dar esalaam.
Halafu wewe unaniuliza sasa mbona kuna watu wapo Nzega na wapo Tanzania halafu hawapo Dar es salaam?
Hujaelewa somo, umechanganya madawa.
Mkuu,Mkuu, bado unazunguka tu mbuyu. Hujajibu maswali yangu: Una maana tuache kustruggle kutafuta ubilionea kwa sababu tukiwa mabilionea wote kutakuwa na inflation?
Na je tukipata pesa nyingi tukazitumia kununua chakula cha kutosha na kukihifadhi kwenye maghala, tukajenga nyumba nzuri za kuishi(hata kama sio za dhahabu), tukawa na magari ya kifahari, hizo mali zitakosa thamani?
Wale wenye imani ya kwenda mbinguni, huwa wanasema kwamba mbinguni hakutakuwa na maskini. Watu wote huko watakuwa na raha. In other words, huko pesa haitakuwa na thamani lakini kila mtu ataishi vizuri. Ndio hoja yangu kuu. Kwamba kila mtu atafute ubilionea kwakuwa uwezekano wa kuupata upo. Tukiwa mabilionea wote, hata kama pesa haitakuwa na thamani, it doesnt matter, kama wote tutakuwa tunaishi kw raha. Kulialia hakuwezi kutusaidia. Zaidi sana tutajiletea stress na magonjwa ya pressure/moyo. Hapo vipi?