Waafrika tuache kulia lia kwa kukosa pesa. Tunaweza wote kuwa mabilionea

acha kuishi kwenye nadharia, kila nchi ina kiasi maalumu kilichopo kwenye mzunguko kwa makusudi sio bahati mbaya, na kiasi icho kwa mahesabu ya haraka iko ivi, ikiwa kila mwananchi atapewa pesa taslim cash basi kila mtu atapata kiasi kisichozidi mil 40, hivo basi mtu kama dewji mwenye dola bil 2 (Trillion 6 za kitanzania) tayar ameshachukua pesa za wtu million peke yake ukijumlisha na matajiri wengine kina rostam, bakhresa basi uchumi wa nchi nzima unashikiliwa na watu wachache ndo kanuni hii inatumika dunia nzima, hivo basi hakuna kiasi cha ziada kilichobaki wewe kupata matajiri wakishabeba pesa, jitahidi kujifunza uchumi bila ivo vitu vyako vikienda kombo utaishia kujilaumu bila sababu
 
Hapana.

A billionaire has a specific and narrow numerical meaning.

You are distorting it.

I can't continue this discussion with you because you have no respect for specificity.
 
Siri ya kuwa bilionea ni kuanzisha au kubuni kitu cha kipekee ambacho binadamu watakua na uhitaji nacho.

Na ili kizazi chako kiweze kuendelea kuwa tajiri, yakupasa kulinda formula ya hicho kitu......
 
Hapana.

A billionaire has a specific and narrow numerical meaning.

You are distorting it.

I can't continue this discussion with you because you have no respect for specificity.
Fair enough my friend; you’re very right that ‘billionaire’ has a strict numerical meaning. But the conversation was never about worshiping the word itself; it was about the possibility of broad wealth creation.

If you prefer to end the discussion over terminology rather than substance, I respect your choice. But my point about widespread prosperity remains valid regardless of what label we attach to it. Thank u sana. Karibu tena, mkuu
 

Fine. Tuondoke kwenye neno billionaire.


Hata hiyo wealth creation inaweza kuwa na maana kama unaongelea kuwatoa watu kwenye abject poverty na kuwapatia kazi, kuwapatia uwezo wa lishe nzuri, elimu nzuri na afya bora. Yani kusiwe na ombaomba, watu waweze kutumia resources vizuri. Hapo tuko pamoja na hiki ndicho kinatakiwa kufanyika.

Tena hili linaweza kufanyika hata kwa ku bypass uchumi wa pesa, kwa government subsidies, credit, insurance, incentives, scholarships, squaring off industry deals etc.

Lakini the moment ukitaka kila mtu awe wealthy kwa maana ya daraja la juu sana, hususan kuwa na pesa nyingi mfukoni, unarudi kulekule kwenye tatizo la economic sustainability whether unatumia neno billionaire au hutumii.

Pesa itakosa thamani kwa sababu ipo nyingi katika uchumi.

Uchumi utataka watu wengine wawe wafanyakazi na wengine wawe wamiliki wa hizo kazi, industrialists and business owners. Hili jambo huwezi kuliepuka. Wakomunisti walitaka kuliepuka na kutengeneza a classless society wakashindwa mpaka Soviet Union ikaanguka. Mpaka sasa China washakubali market economy kwa kiasi kikubwa.

Ukitaka kila mtu awe tajiri kipesa, by any definition ya utajiri, na ukafanikiwa kila mtu akawa na utajiri huo wa kioesa, huo utajiri utakuwa si utajiri tena, utakuwa ndiyo umasikini mpya.

Matajiri watakuwa ni wale waliovuka hiyo equilibrium level mpya na kwenda kwenye next stage.
 
Hii speech uli paswa ulipwe, ili uipige pale harvad mkuu.
 
scarcity creates value.
 
Safi, sasa tuko kwenye reli moja. Asante kwa kudadavua hoja zako. Hata hivyo bado siafiki kwamba kila mtu akipata wealth ya juu, pesa lazima ipoteze thamani. Actually hiyo siyo economic law, ni assumption. Inflation hutokea pale ambapo money supply inaongezeka bila ongezeko la real goods and services. Kama productivity, teknolojia na efficiency vinaenda sambamba, society inaweza kuwa na high per-capita wealth bila bei kupanda hovyo.

Mfano mzuri ni Luxembourg, Norway, Singapore au Switzerland: median income yao iko juu sana lakini inflation iko stable, kwa sababu output per person inakua sambamba na pesa kwenye uchumi. Hata concepts kama universal basic income na sovereign wealth funds zinajengwa juu ya principle hii: resources zisambazwe widely huku productivity ikilindwa.

Mfano wa Soviet Union na China unahusu central planning na suppression of market incentives, siyo kwamba wananchi walikuwa na pesa ‘nyingi sana.’ Wao Walishindwa kwa sababu walikandamiza innovation na uzalishaji, sio kwa sababu watu wengi walikua wealthy. Key variable ni productive capacity, siyo scarcity ya watu matajiri.

Kwa hiyo, kiuchumi inawezekana kabisa majority ya watu wakawa kwenye high-income bracket bila kuua value ya pesa, mradi tu wealth hiyo inatokana na real productivity na innovation, na siyo kuchapisha hela tu. Hapo vipi, mkuu
 
Ukishasema watu wengi wawe na high income, hiyo high income inakuwa si high income tena inakuwa average income.

Kwa sababu watu wengi wanayo.

Huelewi wapi?
 
Haiwezekani wote hapa duniani tukawa matajiri au maskini

NEVER!
Hakuna ‘NEVER’ kwenye uchumi. Historia inaonyesha maisha ya watu yamekuwa yakibadilika sana. Kipato cha dunia kimepanda mara nyingi na mamilioni ya watu wameondoka kwenye umaskini uliokithiri.
 
Cha maana ni wote kuwa na disposable income na sio kuwa bilionea ikiwa hivyo mfanyakazi wako wa ndani utamlipa ngapi wakati na yeye ni bilionea kama wewe; nani atakusafishia garden yako ? Je mchimba kaburi nae atalipwa sana ili awe bilionea au yeye itabidi awe trilionea sababu atakuwa anafanya kazi ambayo kila mtu hataki kufanya ?

Utatambua kwamba issue sio pesa ziwepo kiasi gani bali sustainability ya watu kuweza kupata basic needs unless wote tuwe tunakula bata na robots watufanyie kazi zote.....

Ila hapo utagundua kuna kazi ambayo robots huenda akashindwa kuifanya vema (entertainment na social care) kwahio hao huenda ndio wakawa kina Dangote wa nyakati hizo zijazo; sababu watakuwa wanaweza ku-sustain the Wants of others
 
haiwezekan, kila mtu akiwa producer katika hio hio sekta moja lazima ilalie kwa mmoja, haiwezekan tue na mitandao ya simu laki 1
 
Hakuna ‘NEVER’ kwenye uchumi. Historia inaonyesha maisha ya watu yamekuwa yakibadilika sana. Kipato cha dunia kimepanda mara nyingi na mamilioni ya watu wameondoka kwenye umaskini uliokithiri.
Na mara zote hizo kumekuwa na madaraja, haijawahi kutokea muda ambao watu wote wamekuwa matajiri.
 
Ukishasema watu wengi wawe na high income, hiyo high income inakuwa si high income tena inakuwa average income.

Kwa sababu watu wengi wanayo.

Huelewi wapi?
Aisee, unafaa sana kuwa lawyer. Unajua kucheza na maneno ili kumbana mtu.

Mkuu, high income inafafanuliwa si kwa wingi wa watu bali kwa purchasing power na kiwango cha uzalishaji. Ikiwa uzalishaji na teknolojia vinaendelea kupanda, kipato cha juu cha watu wengi kinaweza kubaki ‘high’ kwa sababu kina uwezo halisi wa kununua zaidi ya basic needs. Ukiona kimekuwa average, basi definition ndiyo imebadilika, sio kwamba ustawi umeondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…