Waafrika tulipotoshwa kuhusu Chifu Mangungo wa Msovero sio mjinga, Watanzania tuiombe familia yake msamaha na tumuenzi kama shujaa wa uwekezaji

Chifu mimi nimetumia Thesis yangu kuonesha Mangungo sio mjinga alichokifana kugawa ardhi kwa wawekezaji ndio kinafanywa saiv na viongozi wa Afrika. Nikiamini uwekezaji sio ujinga. Sa unanifokea wakati katika hiyo mikata sijaweka dole gumba mimi.
 
Hata ukisoma historia Mjerumani alidhamiria kuifanya tanganyika ifanane na ujerumani. Check mfano ramani ya mji wa tanga imekopiwa toka moja ya mji wa ujerumani, ni kichaa tu cha Hittler ndicho kilichoiponza ujerumani.
 
Maisha ya mwafrika yalikuwa bora Sana enzi ya ukoloni kuliko baada ya UHURU, kwa maana wakulima awakuwaza kuhusu soko wao jukumu lao lilikuwa ni kulima tu ishi ya soko sio wao, wafanyabiashara wa kiafrica walifanya biashara pasipo bughudha, ajira zilikuwa tele viwandani na mashambani, elimu na afya ilikuwa bora.
Ni tamaa tu ya wapigania UHURU ndio imeleta shida zote hizi, wao walipigania maslai yao binafsi kwa kuwahadaa waafrika wawape sapoti lakini lengo lilikuwa wao ndio walambe asali.
 
Hata ukisoma historia Mjerumani alidhamiria kuifanya tanganyika ifanane na ujerumani. Check mfano ramani ya mji wa tanga imekopiwa toka moja ya mji wa ujerumani, ni kichaa tu cha Hittler ndicho kilichoiponza ujerumani.
Sure kabisa.
 
Watakupinga ingaw ndio ukweli.

Hata kuwarudisha kwao hatukua sahihi. Mana kama sasa bado tunaangaika kuwasha waje kututembelea kwa kigezo cha utalii
Kuna watu watasema ugaguzi ungekuwa mwingi . Binafsi naona hata sasa tunabaguana wenyewe kwa wenyewe
 
Nachopendea ungwini unaweza kuufirimba upendavyo kujenga hoja; hauna kanuni za kueleweka. Kesho wewe mwenyewe au mwingine anaweza akajenga hoja on the same character kuonesha jinsi alivyokuwa mpumbavu na hoja zikakubalika vile vile!

By the way huwa najiuliza how comes mkataba kati ya Chief wa kaeneo kadogo kama Msowero uliepelekea territory kubwa kama Tanganyika iliyokuwa na thousands of chiefdoms kutwaliwa yote na Germans?

Je, wote wiliingia mkenge kama Mangungo? Au mkataba wa Mangungo ulitumiwa na Germans kuonesha machifu wengine "you see, others have surrendered their chiefdoms; you don't have other options but to abide"?

In short, sijawahi kuelewa mkataba wa Mangungo "kuuza" Tanganyika yote.
 
Watakupinga ingaw ndio ukweli.

Hata kuwarudisha kwao hatukua sahihi. Mana kama sasa bado tunaangaika kuwasha waje kututembelea kwa kigezo cha utalii
Kuna watu watasema ugaguzi ungekuwa mwingi . Binafsi naona hata sasa tunabaguana wenyewe kwa wenyewe
Mwafrika zamani alichukuliwa utumwani tena kwa msaada wa mwafrika mwenzake kwa nguvu kwenda utumwani leo hata kesho maelf ya vijana wa kiafrica wakishinda kwenye ofisi mbalimbali za ubalozi wakililia viza huku maelfu kwa maelfu wakihatarisha maisha yao baharini wakililia kwenda utumwani kwa hiari. SAsa UHURU una maana gani kama vijana wa kiafrica wanazikimbia nchi zao zenye fursa ya raslimali tele na kwenda kuwa ma cheap labour utumwani. Zamani waliitwa watumwa siku hizi jina limeadvance wanaitwa diasporas.
 
Kosa kubwa Sana la Mwalimu Nyerere ni kuacha mazuri ya mkoloni yaani alimchukia mkoloni na mazuri yake yote. Kwa hali ya SAsa Ili kumaliza tatizo la ajira nchini mfumo wa elimu wa mkoloni ndio jawabu, na sio mfumo huu wa elimu siasa. Mwalimu alikosea Sana kuingiza siasa kwenye mfumo wa elimu matokeo ni kuzalisha Jamii ya blah blah angalau Wakenya wao mfumo wao wa elimu ni ule tangu mkoloni kwa kufanyia maboresho tu.
 
KATIBA ya eneo alilokuwa anatawala Mangungo ilikuwa inasemaje juu ya umiliki wa ardhi?, Kama hakukuwepo katiba utambanaje mwekezaji akikiuka masharti?,
KIFUPI: Mangungo aliingia chaka, ingawa hasitahili kulaumiwa sana, Kwasababu hakuwa na uelewa juu ya hilo jambo ( mkataba). Ila inasikitisha Sana siku hizi watu wamepata elimu na wanaingia mikataba ya ajabu.
 
Mangungo alikuwa genius kama hawa mageneus wetu wanaotuletea wawekezaji na maelfu ya watalii, Chief Mangungo kumbe aliliona hili kitambo na kumleta Mzungu mwekezaji, bila shaka Mangungo naye alitengeneza filamu ya Royal tours zama hizo wakaja akian Karl Peters na Bwana Ramzani dalali.
 
Akili ya Bwana Ramzani haina tofauti na akili ya Mhindi aliyepo Tanzania na sisi kumuona mzawa, Bwana Ramzani zama zile alikuwa Dalali hawa ndugu zake kwa sasa ni madali wa resources zetu na wengine wameenda mbali nao kuwa slave master in foreigner land and disgusing as natives.
 
Hapa naona kuna afrocentric historians na Eurocentric historians mchuano ni mkali. Nani yupo sahihi na Nani hayupo sahihi ni kama Imani za dini, kila mtu abakie na kile anaamini
Wewe kama umesoma hiyo mitazamo yote miwili ilitakiwa uwe na point ya kufanya decision ya usahihi na ukosefu. Huwezi kusema kila mtu abaki na mtazamo wake. Hii siyo dini, hata dini inakosolewa.
Chief alizingua. Ethiopia walipigana kuanzia 1800 mpka 1930s. Yeye alishindwa nini mpka akubali kutoa ardhi na miliki ya watu wake?

Na kama Mangungo alikuwa sahihi maana yake harakati za Uhuru hazikuwa sahihi?
 
Shida watu hawaelewi kitu kimoja. Concept nzima ya kuwekeza ni ubepari. Ubepari haujawai kuwa mfumo sahihi kwa maendeleo ya waafrika duniani.
 
Hata ukisoma historia Mjerumani alidhamiria kuifanya tanganyika ifanane na ujerumani. Check mfano ramani ya mji wa tanga imekopiwa toka moja ya mji wa ujerumani, ni kichaa tu cha Hittler ndicho kilichoiponza ujerumani.
Mkuu ulishawaisikia mjerumani anamponda Hittler popote pale?
Bila Hittler Ujerumani ingekuwa shithole kabisaaa
 
Watakupinga ingaw ndio ukweli.

Hata kuwarudisha kwao hatukua sahihi. Mana kama sasa bado tunaangaika kuwasha waje kututembelea kwa kigezo cha utalii
Kuna watu watasema ugaguzi ungekuwa mwingi . Binafsi naona hata sasa tunabaguana wenyewe kwa wenyewe
Hivi umesema hii mada ni thesis yako?
Yaani unafanya research ya historia. Kwamba wewe ni historian, mwafrika, kutoka Tanganyika na haya ndiyo mawazo yako? Au unasapoti ili mada yako ipate wachangiaji?

Excuse my language. No offense intended.
 
Mkuu nisamehe kwa kutumia lugha vibaya
Thesis niliyoisemea hapo sijamanisha research proposal au desertion inayowasilishwa na mwanafunz atakae master au PhD.

Nilimanisha ile maana hii

Thesis

a statement or theory that is put forward as a premise to be maintained or proved.
"his central thesis is that psychological life is not part of the material world"
Synonyme: theory, contention, argument, line of argument, proposal, proposition, premise, assumption, presumption, hypothesis, postulation, surmise, supposition, belief, idea, notion, opinion, view, theme, subject, topic, text, matter, theorem
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…