Naona tulichokosea ni tumeridhi/kubali mfumo ambao hautaki sisi tuendelee, mfano kwenye DINI kila Jumapili Wakatoliki wanaoenda kanisani ni Mil 1 kwa DSM, wakitoka sadaka kila Mmoja Tsh 1,000/= ina maana kanisa linakusanya Bilioni moja na kuzipeleka wanapojua. Je, tungekuwa tunachanga hizo hela kila Jpili kujenga shule, hospital, kuboresha sayansi, Kilimo tungekuwa hivi?
Mfumo wa kielimu-ni mzuri lakini hauna manufaa kwa mazingira yetu. Mfano, leo hii Wanafunzi wanaomaliza vyuo wanakimbilia kuuza nguo (outfit) , simu, earphone, perfumes, je walitumia rasilimali nyingi na muda mwingi kuja kuuza nguo? Au matatizo ya WaTZ aliyoyaoainisha Mwl Nyerere wanayafanyia kazi?watakujibu hakuna ajira lakini hawajatafuta ajira zinazoendana na taaluma zao.
Ulafi(Umimi) wa viongozi wanaopewa fursa kuongoza baadhi ya Idara.
Kubeza ulichonacho na kuamini cha mwingine (mfano Mzungu) ni kizuri kuliko chako, sio kweli.